UshauriSEHEMU INAYOFUATA..
TULIA, Tulia Kaa kimya, Leo ni zamu ya watu ishirini mnaenda mahakamani , haya na wewe mwizi hebu pita huku.
Huku nikisukumwa sukumwa kwenye moja ya mahakama fulani ya wilaya, nilimuona mke wangu akiwa kashikana mikono na Shedy ambaye nilimuona ni rafiki yangu kabisa, wakiwa wananicheka pale mahakamani.
Licha ya kuomba sana watu wanidhamini Tena nawafahamu lakini wote walinitolea lugha Kali kwamba hawaamini kuwa walikuwa wanaishi na mtu au jambazi.
Niliita mke wangu ,mke wangu, lakini nilimuona akipanda gari la yule rafiki yangu Shedy wakapotea.
Upande mwingine nilimuona mama yangu mzazi akiwa ananiangalia, niliona huyu ni msaada kwangu kwa Sasa lakini Cha ajabu aliniambia mwanangu nakupenda sana, Tena sana ila kwa hili ulilofanya acha Sheria ifuate mkondo wake.
Mama, mamaaa, niliongea mpaka kilugha chetu lakini mama hakusikia,
Ina maana wamejisumbua kutoka mkoani kuja kuniangalia ninavyopekekwa jela, nilijiuliza ni Bora wasingekuja maana wameniongezea maumivu ya hali ya juu mno,
Hakimu, alionesha ni mtu wa huruma akaniambia pole sana ndugu zako wameshindwa kukudhanini, ila tutafanya mpango wa kuwabembeleza wakupe dhamana japokuwa kwa Leo utapelekwa gerezani, utakaa siku kumi na nne kulingana na date yako inavyosema Kisha kesi itakaposomwa utahitaji wadhamini jua kuwa ukikosa wadhamini utarudishwa Tena jela.
Nikawaza kama Mama yangu mzazi,mke wangu wamenitelekeza
Nani Tena atanisaidia,halafu Shedy wewe did rafiki mzuri yaani unanichukulia MKE WANGU.
Naenda jela nikitoka nitalipa KISASI nakwambia nilifokaa wakaja maaskari magereza wakanivuta kwa nguvu kusudi nipande gari lao wakati yule Askari akinisukuma,
Nilizinduka,toka kwenye usingizi mzito kumbe aliye kuwa ananisukuma siyo Askari ni mke wangu alikuwa ananitingisha.
Pole mume wangu,najua una haki ya kuendelea kulala baba,lakini ni saa nne asubuhi hii,nilitaka nikuache upumzike lakini nishaandaa kifungua kinywa hapa wewe ni kuoga tu,Kisha njoo tupate break fast .
Mbona kama unalia mume wangu,pole baba hayo yameisha familia nzima ilikuwa inakuombea lakini omba sana MUNGU akutie nguvu katika hiki kipindi kigumu.
Mimi ni mke wako wewe ni mwanaume ninayekupenda kwa dhati.
Aliongea kwa hisia huku akinifuta machozi yaliyokuwa yametua kwenye ndevu ambazo zimekaa vibaya mno.
Nilifikiria ile ndoto,nilimwangalia my wife huku nikiwaza ndoto ile ilikuwa na maana gani,
Mbona ilionesha Kuna usaliti mkubwa kwenye ule ulimwengu kuliko hiki nachokiona kwa mke wangu.
Mke wanguu,niliita unasema Shedy alikutongoza? Shedy huyu huyu
Mume wangu fanya kwanza niliyokueleza nenda kaoge Kisha unywe chai haya yote nilishindwa kukumalizia Jana kwakuwa nilikuona
Una usingizi mzito ,nilimkumbatia kwa upendo
Niliamka nikajimwagia maji nikaja pale sebuleni nikakuta majirani wengi wamekuja pale wengi wakinipa pole kwa mkasa ulionipata
Huku wale ambao sikuwa karibu nao sana kirafiki wakinishangaza kwa pole zao ambazo zilionesha kujali huku elfu kumi kumi na elfu tano zikiwa zikiwa nyingi.
Kama maisha yetu ya kiswahili yalivyo,
Baada ya kumaliza kupata kifungua kinywa huku wageni wakipungua na wenyeji wakitawala mama alitaka tuzungumze, tukiwa watatu tu yaani,
Mimi,mama na dada,
Kweli mke wangu alikuwa bize kupendezesha chumba huku mtu mzima nikiwa nishajua malengo yake maana Kuna baadhi ya salamu tulikuwa hatujapeana.
Tulitoka nje sisi watatu tuliongea mengi sana ya kinyumbani hususani Mimi nikionywa kuwa mpuuzaji wa mambo mengi hasa kujizindika,
Wewe ni mwepesi mwanangu,ndiyo maana vijimatatizo havikuishi likiisha hili linatokea hili likiisha hili unaangukia huku,haya siyo maisha mwanangu wewe una familia lakini unaishi kitoto mno ilhali una familia.
Lazima upate mtaalamu akufanye uwe mzito matatizo ni sehemu ya maisha lakini tambua Kuna vitu haviji vyenyewe .
Mwanangu una elimu nzuri ambapo huwezi kukosa kazi ki rahisi Lakini nimekuwa nikisikia kuwa upo kwenye wakati mgumu Kila Mara hujioni kuwa hiyo ni shida?
Hata huko makazinj Kuna ushindani mkubwa mno jambo ambalo we hulioni,alimalizia mama
Halafu kaka unakumbuka kipindi kile Ukiwa na kazi yako ya kwanza jinsi ulivyoshauriwa kuwa unatakiwa kujizatiti kwa kumtafuta mtaalamu lakini ukawaita hao ni matapeli hawana maana.
Dada yangu aliongea kwa uchungu.
Sikuwa na la kuwapinga maana muda ule nilikuwa nawasikiliza zaidi wao na chochote walichoamua nilikubaliana nao.
Ila mwanangu Dani mke ulipata , yaani huyu mtoto wa watu alivyopambana sikufikiria kuwa yupo hivi yaani anatupikia Chakula lakini hali licha ya kumbembeleza lakini alikuwa anakula kwa shida sana pia sisi siyo wenyeji wa hili jiji lakini ameonesha umahiri mkubwa japo tulikosa tu sapoti tu kutoka kwa walio kushikilia.ni yeye amesababisha utoke kwa kuweza kufanya upelelezi wa kina juu ya upotevu wa mzigo
Tulizungumza mengi huku wakinitaka nisahau mambo mengi,nihesabu ni mitihani tu,
Waliniambia nipumzike na mke wangu Huku wao wakiongozana na dada wa kazi kwenda sokoni,
Nilirudi ndani ,swali la kwanza likawa
Hivi mke wangu kwani mzigo ulijuaje kama ni ule na uliupataje
Mume wangu,
Baada ya mama mkwe kufika hatukuelezana ni mzigo gani umepoteza Kila mmoja alikuwa kanyeshewa kutokana na wewe kuwa ndani
Ila Kuna siku kutokana na stori za hapa na pale dada aliweka wazi kuwa wakati unapakia mizigo aliona ni machuma fulani,
Lakini Mimi mwenyewe siku nawapokea pale ubungo nilimsikia mzee aliyekuwa analalamika kuhusu kubadilishiwa mzigo
Hivyo ikafanya nifikirie kuwa wewe mzigo uliopoteza tunaambiwa umepotelea stendi hivyo nikaunganisha nukta.
Kwakuwa hayo niliyapata usiku hivyo saa moja kamili ilinikuta stend ya mkoani ubungo, nilisubiri mpaka saa tatu nikaenda pale kituo kidogo nikakutana na maafande wawili nikawaeleza kisa kizima na aina ya mzigo uliopotea afande mmoja akasema anazo detail zako na yeye ni mmoja wa wa Askari waliokuweka chini ya ulinzi
Hivyo akaamuru,tuwatafute wasimamizi wa wa stoo za pale hatukukagua sana kufika tu stoo ya pili tuka kuta vyuma viwili kimoja Cha njano
Ila hakuna ambaye alithibitisha kwa asilimia mia moja kama mzigo ndiyo wenyewe kwahiyo maaskari walitoa maagizo kwa walinzi wa pale kuwa wawe nao makini
Niliwaaga na kushika barabara kuelekea kwenye kampuni ya bosi wako ambapo licha ya baadhi ya watu wa mapokezi kunizuia ila tayari bosi wako yule mwanamke alikuwa anatoka aliniita kwa ukali akiuliza nimefuata Nini
Bila hata salamu,nikamjibu mzigo aliopoteza mume wangu umepatikana.
Hivyo akatuma vijana wake ambao ndiyo walioufungua huko mkoani tukarudi mpaka stendi wakathibitisha
Kuwa ni wenyewe Kisha maaskari wakauchukua wakakaa nao
Huku wakiniambia Mimi nirudi nyumbani wao wanajua ulipo.
Ni kweli siku ya Jana tukakuona unarudi. Kwani ulikuwa gereza gani?
Aliuliza,
Hata sikuwa jela ni waliwaficha labda waliona mnawasumbua,
Sasa yule afande mjinga aliyejifanya mpelelezi uchwara, akiniambia yeye ndiyo kauona mzigo alikuwa na maana gani wakati kumbe ni mapambano ya mke wangu.
Halafu yule OCS aliyejivika ushemu na ukuwadi kwa yule Amina akidai eti Amina aliamuru nitoke yeye, walikuwa na maana gani malaya wakubwa wale, anadhani Mimi naweza kuwa na Amina mtu asiyekuwa na sura Hadi akakimbilia kuwa polisi, nilitukana kimoyo moyo baada ya wao kujipa umuhimu wakati kumbe ni washenzi tu.
Itaendelea,,,....
Bado ni mbichi hii usikose
Sawa itaendelea, itakua siku gani?SEHEMU INAYOFUATA.......
Nilitulia siku hiyo na familia yangu huku nikipanga na kupangua mambo mengi, licha ya kuwa nilianza kuhisi homa ambapo sikuwa na nguvu nikaona hapa sipaswi kuwa mzembe lazima niende hospital.
Kwakuwa tangu nifike sijawahi kuhangaika na simu nikaona huu ni muda sahihi wa kuwa hewani , nikaiweka simu yangu chaji, huyoo mpaka zahanati ya jirani nikamtafuta daktari mzuri ambaye nilimweleza kuwa nilikuwa sehemu isiyoridhisha kwa takribani wiki mbili, huku nikiwa sili kabisa na nikila basi ni Chakula ili mradi tu.
Daktari alinielewa na pia akanishukuru akidai nimemrahisishia kazi, maana Kuna watu huwa wanajua kabisa namna mazingira anayoishi kuwa huenda yakasababisha mabadiliko ya kimwili lakini huwa wanaficha , Kwanza mtu hataki aonekane alikuwa mahabusu.
Akanichukua vipimo fulani, na kuniandikia dawa fulani kama kawaida yao zikiwa pale hazipo Bali zinapatikana pharmacy.
Huku akinisisitiza kuhakikisha nakunywa maji mengi pia Nile Kila napohisi kula nisifuate ratiba,
Nikakamilisha Kila kitu huku nikiiwasha simu yangu ili mambo mengine yaendelee, ndiyo ilikuwa lazima kumbuka familia nzima inanitegemea Mimi kazi yao wao ni kuniombea tu niwe sawa
Huku Mimi nikiwa na jukumu la kuhakikisha natimiza yale mahitaji muhimu.
Wakati nawasha simu, nilikutana na jumbe nyingi mbalimbali, huku zingine zikilaumu kwa kutokuwa hewani, huku moja ikiwa inatia kinyaa inakera, ikiwa inatoka kwa Shedy eti, ananipa pole na yeye,
Huku akisisitiza ana mazungumzo na mimi
Maanina zako Shedy taarifa zako ninazo,
Nilitukana.
Nyingine kubwa zaidi ilitoka kwa namba nisiyoijua ikisomeka hivi,
Kampuni ya(jina kapuni)inakupa pole na matatizo yaliyo kukuta,
Kila Jambo hutokea kwa sababu maalum, karibu Tena kwenye kampuni yetu.
Hii kampuni nilijua niliwahi kutuma maombi kipindi Sina kazi nikaambiwa kwa nafasi yangu, hakuna kazi wakataka kunipa kazi ya udereva nikakataa licha ya kuwa Nina uzoefu kuwaendesha mabosi.
Hii nyingine ilisomeka hivi,,
Ukipata ujumbe huu fika ofisini, pia washa computer yako,
Hii ilikuwa inatoka kwa waajiri wangu walioniweka ndani, ilinikasirisha sana Tena mno . Sikutaka kuwasiliana nao Hawa, watu wasio na utu hata kidogo,
Eti niwashe computer, ili iweje Kwanza hii router yenyewe ni mbovu, nikapuuza,
Simu ikaanza kuita huku wanafiki mbali mbali wakinipa pole za hapa na pale,
Kama Nina watu kiasi hiki kwanini hawakunipigania niweze kutoka Hawa mafala Nini.
Nikaiweka simu pembeni nikiwaza juu ya hii kampuni mpya ambayo imenitumia ujumbe wakiwa wananihitaji nikaona lazima kesho niende maana kwenye kampuni ya mwanzo sikuwa na hamu Tena
Nikawaza namna nilivyofanya ujinga pale stendi nikashindwa kuwa makini Hadi mzigo ukapotea, nikajua ni ESTA aliisababisha yote haya.
Hapana (nikajicheka mwenyewe)
Wala ESTA hahusiki Bali ni tamaa zangu mwenyewe, hata hivyo Kila jambo Lina wakati wake hata ingekuwaje lazima ningeonja joto la mahabusu tu.kwakuwa MUNGU akipanga amepanga
Mke wangu alirudi huku akiwa na matunda mbalimbali na yenye kuvutia nilifurahi sana, nikaona ni wakati wa kutengeneza router yangu maana watu wananitafuta naona.
Maana hii computer kubwa ndiyo ya muhimu zaidi kuliko hii ndogo
Nikatoka kwenda kuangalia huko mtaani upepo unavumaje huku Mama akiniasa kuwa makini kwamba Mimi kwa wakati ule nilikuwa kwenye zone ya mikosi kwahiyo ningeweza hata kuitiwa mwizi nikapigwa na kuuawa kwakuwa tu nafsi inakuwa vibaya,
Nilitoka nilitembea kama mita hamsini tu kutoka nyumbani nikapigiwa simu kuwa Nina mgeni wangu, sikuwa na jinsi nilirudi huku nikiwa makini maana aliyeng'atwa na nyoka.......
Nikakuta Kuna Prado ya nguvu imepaki huku lango wa dereva Ukiwa umefunguliwa,
Aaaa rafiki yangu Daniel habari za siku nyingi mr , lakini pia pole kwa matatizo, tumesikia kisa kizima kuhusu mkasa wako lakini lazima maisha yaendelee kaka njoo ufanye kazi kwenye kampuni yetu,
Aliongea bila breki yule jamaa mwenye ngozi ya hela, ambaye sijawahi kumuona japo kampuni anayoisema naifahamu ni moja ya sehemu nilikuwa naziota ni watu wanao pewa tenda kubwa kutoka serikalini huku ile kampuni ikiwa na shareholder ambaye ni mwanasiasa mkubwa na maarufu(jina kapuni)
Nikawa njia panda,
Jamaa nahisi alitambua mawazo yangu
Akanisihi niache yaliyopita,
Ndugu yangu, Mimi nilikuwa na kampuni yangu kubwa kuchukua vifaa vya magari kutoka Japan na kusambaza hapa East Africa lakini niliyakanyaga baada ya kuwaletea utapeli wazulu wa south Africa kwa kuwapelekea matairi feki, walinimaindi sana , hawakuwa na la kunifanya kwakuwa nipo kwenye nchi yangu
Lakini waliniwekea mtego Kuna dili wamelipata kwao SA hivyo twende, nilivyofika kule walinigeuka kidogo waniuwe, nikaishiwa kubambikiwa kesi iliyoniweka karibu mwaka kabla sijatolewa na huyu bosi ambaye anakuhitaji,alimalizia yule jamaa
Akaendelea,,, Mr Daniel ni heshima kubwa mtu kukufuata nyumbani, nafasi uliyonayo Kuna watu chungu mzima wanaihitaji kwahiyo uamuzi ni wako tuna masaa 48 ya kusubiri kama upo tayari karibu ofisini
Akawasha ndinga lake akaondoka,
Mwanangu Dani tumesikia Kila kitu kuhusu huyu baba aliyekuja, na Mimi niseme tu kuwa wanaanzaga hivihivi halafu mwisho unaangukia kwenye matatizo, nasema Bora turudi mkoani ukalime wewe hapa mjini hapakufai matatizo uliyopata yanatosha mwanangu.
Aliongea mama kwa ukali Hadi mke wangu akaogopa, nadhani hajawahi kumuona akiwa vile,
Hapana Mama yangu siyo hivyo, matatizo niliyopata ni ya kawaida sana nachojivunia ni kuwa sikuiba Wala sikufanya utapeli kwahiyo ni lazima maisha yaendelee
Huko mkoani unakosema Mama nilikuwa na mpango wa kulima kweli, lakini siyo kilimo Cha jembe la mkono hicho ni kilimo Cha zamani mi nataka kilimo Cha kulima ekari nyingi na mpando wa kisasa huku nikihusisha wataalamu, Haina maana nakudharau mama yangu,
Hebu fikiria Mama, unanilinganisha na akina fulani kuwa wenzangu wametulia, lakini hebu linganisha hata vibanda vyetu mama, nikiwa namuonesha mama kuzunguka nyumba yangu, pale kijijini Kuna mtu Ana nyumba kama hii mama,
Halafu Mimi nina Elimu ambayo bado napaswa kuitumikia ili inisaidie zaidi Mimi na familia yangu,
Je, nikiwa kijijini nani ataniona Mimi mama yangu?
Niliongea kwa uchungu,
Hapana mwanangu Mimi nakupenda ndiyo maana nimesema hivyo,ni lazima uwe makini,nakupa baraka zote za kutafuta na uendelee kuishi hapa,hata hivyo nilisema kwa uchungu kutokana na yaliyokukuta lakini una msaada mkubwa mno kwenye familia yetu.
Sawa mama ni jukumu langu kuwaweka katika wakati mzuri wazazi wangu,
Mjukuu wako Jack hayupo hapa anasoma high school,je kule kijijini atasoma shule gani,
Mbona we ulisoma shule zilezile,aliongea mama kiutani huku tukicheka.
Yakaisha hayo huku mama alishauri lazima nipate mtaalamu ili anitengeneze ili niwe ngangari.
Nikawaza ushirikina Tena,
Wakati nikiwaza hayo,simu kutoka kwa aliyekuwa rafiki yangu na Sasa mbaya wangu shedy iliita kwa fujo
Itaendelea....
Aiseee ,, nlkua nacheka tu comment za watu wanavosema arostooo ilaa namii nimefikaa apa sasaa kweliiii ni arostooo aiseee ,,,,bwana mkubwaaa em fanya maajabu basi..............SEHEMU INAYOFUATA.......

Tunasubiri mkuuSEHEMU INAYOFUATA........
Niliipokea simu ya Shedy, na kuiweka sikioni,
Halo kaka u mzima, pole na matatizo, lakini ni kwamba naomba tuonane, chonde chonde kaka ni mazungumzo na wewe
Aliongea bila kunipa nafasi Wala sikumjibu kitu.
Ila huyu ananitafuta Tena ananitafuta haswa, nilijitahidi kutokuonesha dalili za unyonge huku nikirudi kwenye kikao chetu na kuwaaga Mama, mke wangu kuwa najipumzisha ndani kidogo,
Mama akaniambia nipumzike ila muda kidogo ana mazungumzo na mimi.
Niliingia chumbani nikiwa kwenye PC yangu na search vitu mbalimbali ambavyo pengine sikuwa na vielewa kutokana na mawazo kuhusu tabia aliyoionesha Shedy.
Ni rafiki yangu, tuna historia nzuri tangu utotonj, tumeshirikiana mambo mengi,
Ni mdogo kwangu nikiwa nimemzidi miaka minne, kipindi nasoma shule fulani ya seminary kule mkoani kipindi wazazi wakiwa wamelenga niwe padri, niliishindwa ile shule nikiwa form three,
Nikarudi nyumbani hapa nikatafutiwa shule nyingine ya kawaida ya serikali nikaanza kidato Cha kwanza upya tukiwa na Shedy, nilikuwa nafanya vizuri sana kwenye masomo ukizingatia from form three to form one, nilitesa sana huku nikipata marafiki wengi kulingana na kuonekana genius.
Kama ni suala la mademu ilikuwa rahisi sana kiasi Cha Kila mtu kunitaka nimtafutie demu,
Lakini rafiki wa kweli alikuwa Shedy, kwanza hakuwa na akili kivile, halafu alikuwa mvivu sana, hali iliyopelekea niwe nakuwa naye sambamba kwenye discussion mbalimbali.
Kubwa aliloliweza pale shuleni ni biashara alikuwa anauza vitu huku vidogo vidogo Kama vyakula akakuza mtaji wake Hadi kufikia kuuza madaftari ambayo yalikuwa adimu sana kuanzia mtaani Hadi shuleni lakini yeye alikuwa nayo
Nakumbuka aliwahi kupewa kichapo toka kwa wanafunzi wa form six baada ya kuwapelekea mzigo fulani na wao kwa ubabe wakata kumdhulumu dogo akawa hajakubali wakampa kichapo , kama si Mimi niliyemuamulia sijui ingekuwaje.
Familia yangu ilikuwa ya kanisani, kwahiyo Kila jumapili hakuna aliyekosa kwenda kanisani huku mshua akinihimiza zaidi Mimi labda kwakuwa nilikuwa mtoto pekee wa kiume,kwahiyo nilichungwa kiaina
Na Mimi nikaona isiwe tabu nitakuwa naenda na Shedy kanisani ,kwa Mara ya kwanza Shedy anaingia kanisani aligundua fursa kibao hasa biashara zinazoendelea kule nje,miwa,na vitu vingine kibao.
Ikawa jumapili iliyofuata alikuwa na mazaga kibao ,asitambue kwanza hairuhusiwi
Lakini yeye alikomaa licha ya kupigwa mkwara lakini akawa anauza kwa Siri.
Nakumbuka tukiwa form four ,ile ya zamani siyo ya Sasa bado watoto
Nilienda nyumbani kwao nikamkuta ana baiskeli mbili aina ya swala .
Akinambia Kuna mzee mmoja kampa amuuzie kwakuwa yule mzee alistaafu kazi yake ya udaktari akaamua kuuza baadhi ya vitu ili aende kwao, lakini kabla Shedy hajauza yule mzee aliondoka na familia yake , hatukuwaona Tena.
siku si nyingi baiskeli zikauzwa na hakukuwa na simu kwamba angewapa taarifa kwaiyo ikawa imekula kwao, nakumbuka alikuwa na vijihela kiasi Cha kumzalisha mmoja wa mabinti pale kijijini kwetu
Ambaye ndiye mke wake Hadi leo
Mitihani ilikaribia, wakufaulu tulifaulu tukaendelea mbele ya safari huku Mimi nikimfurahisha sana baba yangu mkubwa aliyeko huku mjini kiasi Cha kunitafutia shule nzuri kiasi chake tofauti na kayumba za mkoani,
Nikaachana na Shedy kwa kipindi kirefu kwakuwa yeye alifeli
Cha ajabu tukakutana hapa mjini nikiwa form six yeye akiwa kajikita zaidi kwenye vijibiashara ambapo kwanza nilikuwa namuonea huruma sana nilimuona akiteseka tu
Lakini MUNGU si mwanadamu, alianza kung'ara huku mtaji wake ukikua huku Mimi nikiendelea na Elimu ya juu,
Alikuwa wa kwanza kuoa baada yakujiona mambo yake safi akaamua kumfuata mwanamke aliyemzalishaga huko mkoani, ilafungwa ndoa safi ya kanisani huku Mimi nikijitoa kwa asilimia Themanini kuhakikisha Kila kitu kipo sawa,
Na nilikuwa mmoja wa viongozi wa moja ya makanisa ya hapa mjini kulingana na historia yetu kuwa watu wa kanisa,
Maisha yaliendelea nikawa natafuta kazi Sasa, ili na Mimi niwe kwenye ramani ya maisha nikafanikiwa kupata kazi ya kumuendesha boss fulani wa kiarabu.
Kutokana na kuwa sikuwa na familia hela niliyokuwa nalipwa ilitosha kufanya vitu vingi sana, huku nikijua kabisa lazima nitafute kazi ya heshima ili nikaitendee haki taaluma yangu
Tatizo tulilopishana na mwarabu yule ni udini, alilazimisha niingie msikitini wakati Mimi mkiristo niliyesimikwa licha ya ndugu zake kumshauri kuwa aachane na Mimi tufanye kazj iliyotuunganisha bado ye alikomaa kiasi Cha kuniahidi eti nitamuoa Binti fulani walikuwa wanakaa naye alikuwa shombeshombe fulani
Kama nisingekuwa na msimamo ningesilimishwa lakini nilivizia nikambandua yule Binti Kisha nikaendelea na kazi zingine tuliachana na yule mzee baada ya kuumwa akapelekwa huko kwao
Nikatafuta kazi nyingine ya maana kabisa, nikirudi kwa Shedy ni kwamba ni rafiki yangu wa kitambo ila sasa aliyakanyaga hayawani yule.
Kwahiyo yeye kuwa na hela na magari ndiyo aje kumtongoza mke wangu,?
Usikute alifanikisha analotaka sema labda tu mke wangu anajitetea Lakini sipaswi kumhukumu mke wangu Hawa wanawake ni dhaifu sana
Yaani kukaa wiki mbili tu ndani rafiki yako wa damu anakuharibia kama ningekaa mwaka ndani,
Si angehamia kwangu kabisa.
Sema nitamkomesha ila napaswa kuwa makini kwakuwa naweza kuharibu nikaishia pabaya wakati wamenichokoza.
Sikutaka kukutana naye,
Mume wangu unawaza Nini taani unawaaaaaza baba Jack achana na hizo habari zimepita tuangalie mengine, aliongea mke wangu Huku akiwa anachagua nguo fulani toka kwenye kabati akidai zingine zinambana kwakuwa tumbo lilishakuwa kubwa,
Hivi ni miezi mingapi niliuliza
akajibu ni miezi sita, hata hivyo nimemuomba mama wifi abaki,
Hamna kwani si tunaye dada wa kazi Kila kitu kitakuwa poa wewe hao waache waende tu mkoani,
Mume wanguuuuuu, kwanza ungejua huyu dada wa kazi kanikera basi tu sema nilikuwa kwenye heka heka ya tatizo lako nikawa sijapata muda wa kumsema, na kwa Sasa Bora aende tu kwasababu Kuna siku nilikuwa natoka mjinj kwa bosi wako nikamkuta kamkaribisha Shedy mpaka ndani wakati nilishamkataza ni marufuku kuwakaribisha marafiki wa mume wangu Kama yeye hayupo. Lakini pia alipewa laki moja na Shedy eti itatusaidia mimi nilishajua lengo lake nikanwambia airudishe na sidhani kama kairudisha
Cha ajabu shemeji Shedy akawa anakataa kutoka nje mpaka nilipotishia kumuitia mjumbe ndiyo akatoka, kwanza ngoja nimwite dada wa kazi akuelezee
Na ukionana na Shedy ana alama au kidonda usoni Mimi ndiyo nilimpiga na kibao Cha Nazi baada ya kuwa mbishi hataki kutoka nyumbani kwangu,
Sikutaka kusubiri nikampigia simu tukutane baa fulani lakini siyo kwake nadhani alinielewa sikutaka kuonesha utofauti,
Tulikutana akiwa yupo na mkewe.
Kabla hata Shedy hajaanza kuongea ,
Mkewe akaanza kuwaka, kwanza shemeji pole na matatizo, wewe ni ndugu yetu tumetoka mkoa mmoja ila mkeo alichomfanyia mume wangu sikupenda Tena sijapenda haswaaa
Hebu mtazame, mume wangu si angemsababishia upofu,/ukilema
Nilimtuliza Kisha nikataka nimsikilize mwanaume mwenzangu.
Ujue braza Dani ilikuwaje,
Siku uliyopata matatizo wewe hakuna aliyejua upo wapi mkeo akawa na mashaka huku wivu ukimjaa akihisi labda upo kwa wanawake
Akanipigia simu nifanye upelelezi+kusaidia utafutwe ila baada ya masaa mawili alipiga simu mwenyewe kuwa kapata taarifa kuwa umeshikiliwa na maaskari baada ya wewe kupoteza mzigo hata hivyo , ila hakujua upo kituo gani
Hata hivyo mke wangu aliniruhusu nije nyumbani kwako, ili nipate kuzungumza naye kwa kina zaidi.
Je, ulimpigia simu kuwa unahitaji kuonana naye?
Niliuliza.
Hapana, nilitambua wazi ni namna gani shem alivyochanganyikiwa nikaona isiwe tabu ngoja nifike tu.
Kwani mume wangu si ulidai ulipiga simu, mkewe alimuhoji,
Ndiyo ila haikupatikana.
Nikanote kitu,.
Akaendelea
Nilipofika nyumbani kwako nilimkuta dada wa kazi akanikaribisha,
Ukaingia mpaka sebuleni, niliuliza
Hapana nilikuwa kwenye gari langu
Sawa halafu ikawaje,
Baada ya muda kidogo kama saa mbili usiku, shemu alirudi alifurahi kuniona tukaongea mawili matatu Cha ajabu sijui Nini kilimpata akaanza kunisukuma , eti nitoke nikashangaa Nini kimempata shemu matatizo yako yamemchanganya namna hii
Nilipojaribu kumtuliza alichukua kitu ambacho si kukijua nahisi ni chuma akanipiga nacho usoni nilikimbilia kwenye gari huko nikiwa naomba MUNGU nisije sababisha ajali maana damu zilikuwa zinavuja sana.
Ndiyo mimi nahisi yule mdogo wangu mimba inampeleka vibaya maana kama kuzaa wote tumezaa Tena ye ndo kwanza anatafuta mtoto wa pili watu wengine tunakaribia kuacha kabisa.
Hawezj kuniumizia mume wangu yule kujifanya kachanganyikiwa ili ionekane anakupenda sana au vipi
Mbona Mimi mume wangu na kazi zake za udalali huko mahabusu kukaa ni kama kwake lakini sijawahi kujifanya naumizwa kiuwendawazimu kama alivyofanya mkeo, Tena nikwambie shemu urafiki wako na mume wangu atakaye uwa ni mkeo wewe kabla hata hujaoa ulikuwa unakuja hapa tunakula, tunafurahi, lakini mnaenda kuachana na mume wangu kisa ni huyo mkeo nikwambie ukweli,
Aliongea yule mke wa Shedy kiukali kiasi Cha kufuta lipstick zake,
Lakini nilimtuliza huku, nikiwa njia panda Ina maana mke wangu alinidanganya, au kweli mimba yake inampa hasira, niliwaza moyoni.
Nikauliza, lakini Shedy wewe laki moja mke wangu ulitaka kumpa ya Nini?
Tena ulimpa dada wa kazi ili aifikishe kwa boss wake,
Haaa Mimi nilikuwa namsaidia tu, alijibu,
Weewe mume wangu, we siku ile nilikuomba elfu thelathini tu niongezee nipeleke kwenye marejesho ukadai hauna, hiyo laki uliitoa huko ya Nini?
Haya tufanye una huruma sana, mbona hukunishirikisha kama ambavyo tulishauriana mambo mengine, alifoka mke wajamaa
Ambaye ana mdomo sana na namjua suku nyingi.
Tena Mimi kifupi niwe mkweli mke wangu ndo akaunti yangu ndogo ukiacha akaunti zingine,
Hela ya kula tu mpaka Mimi napata matatizo alikuwa na zaidi ya milioni tatu, niliongea kwa ukali kidogo baada ya kunote jambo lingine.
Unajua mume wangu sikuelewi, aling'aka mke wa jamaa.
Itaendelea........