Simulizi: Mchawi


Stori nzur sana nipo naisoma leo mpk nifike mlipofika inavutia kutaka kujua mwisho wake
 

Huyu mwanamke duuh muuaji kupeleka mwanaume kwake
 

Simon kamchana makavu nimependa duu mwanaume bushoke anaafadhali
 
SEHEMU YA 28:

“Kwa kweli kuachana na mke wangu siwezi labda unipe njia nyingine ya kumtuliza.”
“Utamtuliza vipi?”
“Kwa vyovyote vile hata kwenda kumueleza yule jamaa aachane na mke wangu.”

“Mimi siwezi kufanya hiyo kazi, labda ukamueleze mwenyewe kwani mbaya wako si unamjua?”
“Basi nakuomba kitu kimoja.”
“Kitu gani,” kauli ile ilinifanya nikae vizuri kumsikiliza.

“Kuanzia sasa hivi amri zote za nyumba utoe wewe, kurudi nyumbani asikuwekee amri, mweleze mwenye uamuzi wa mwisho ni wewe. Kila kitu kitakuwa chini yako, pia omba mkopo ukatafute chumba ili mhame nyumba ile ya mwanaume mwenzio ili uweze kumdhibiti mkeo, bila hivyo utatwanga maji kwenye kinu.”

“Sawa nitafanya hivyo.”
Nilikubaliana na Simon, kwa vile muda wa kutoka ulikuwa umefika tulitoka kazini na mimi kurudi nyumbani nikiwa na mawazo tele jinsi ya kumueleza mke wangu. Nilijiuliza atapokeaje uamuzi wangu mpya? Lakini niliamini njia ile ya kuvunja amri pia kuhama nyumba ya mwanaume mwenzangu na kuhamia kwangu huku nikiweka amri mpya itaweza kunifanya nimdhibiti mke wangu.

Nilipofika nyumbani, kama kawaida mke wangu alinipokea kwa heshima zote huku akionesha upendo kwa kuongeza baadhi ya vitu kama kunichemshia maji ya kuoga na kula pamoja. Vitu vile ndivyo vilinifanya nipiganie kwa nguvu zangu zote kuhakikisha mke wangu anabaki mikononi mwangu.

Baada ya chakula cha usiku tukiwa kitandani nilimuuliza mke wangu kwa sauti ya chini. “Mke wangu.”
“Abee mume wangu,” aliitika huku akifumbua macho yake makubwa kidogo ambayo nilipenda kuyatazama kila wakati.

“Mimi nani?”
“Mume wangu.”
“Nani mwenye amri huku ndani?”
“Mbona umeniuliza hivyo?” swali langu lilimshtua.

“Naomba unijibu swali langu siyo kuulizwa swali,” nilikaza sauti.
“Mmh! Mume wangu mbona leo mkali hivyo?”

“Mke wangu naomba unijibu swali si kuniuliza swali,” nilijikakamua mwanaume huku mapigo ya moyo yakinidunda na kusema kwa ukali kidogo. “Wewe mume wangu.”

“Basi kuanzia leo mimi ndiye nitakayekuwa natoa amri humu ndani.”
“Mume wangu maneno gani hayo, lini ulitoa amri ikapigwa?” mke wangu aliniuliza huku akinitazama kama hanioni vizuri.
 
SEHEMU TA 29:

“Sijawahi kupingwa, lakini kuna mambo yanayoendelea humu ndani sikubaliani nayo.”

“Mambo gani mume wangu?”
“Ya kupangiwa kuwa nikitaka kurudi mapema nyumbani lazima nitoe taarifa.”
“Sasa hapo kuna ubaya gani?”

“Upo, kwa vile huwezi kunipangia nikirudi nyumbani mapema lazima nikutaarifu.”
“Sasa hapo kuna ubaya gani?”
“Upo, kwa vile siwezi kurudi kwangu kwa kutoa taarifa.”

“Nia yangu ilikuwa kuhakikisha ukirudi niwepo nyumbani.”

“Unakwenda wapi?”
“Labda naweza kuitwa na mama.”
“Nani wa kumtaarifu mwenzake kwamba anaondoka nyumbani.”

“Mimi.”
“Pia hata nisipokukuta nyumba haiondoki.”

“Sasa ulikuwa unatakaje?”
“Nataka nirudi bila kukupigia simu.”
“Ni hilo tu mume wangu?”
“Ndiyo.”

“Basi, fanya uwezavyo, kwa nini tugombane kwa jambo dogo?”
Nilikubaliana na mke wangu ambaye niliamini tungebishana hata kutishiana kuachana, lakini alikuwa mwelewa kitu kilichonifanya niwaze labda wameachana na yule mwanaume.

Siku ya pili niliporudi kazini, nilikwenda kwa mkuu wangu wa kazi na kumuomba mkopo kwa ajili ya kuhamia nyumba nyingine.

Ilikuwa ajabu nilipofika tu alinikaribisha kitini kwa uso wa tabasamu lililojaa huruma iliyoonesha yupo tayari kunisaidia.

“Karibu Kazala,” alinikaribisha kwa sauti ya upole.

“Asante bosi.”
“Ndiyo, nikusaidie nini?” bosi aliniuliza huku akinitazama usoni.
“Bosi nilikuwa naomba mkopo wa kulipia nyumba ili nihame nilipokuwa nakaa, nina imani kila kitu unajua.”

“Najua, lakini hukutaka kuniambia.”
“Tusameheane mkuu wangu si unajua kuelemewa kubaya.”
“Najua, kwa hiyo hii itakuwa tiba ya matatizo yako?”

“Nina imani nipo katika mkakati huo kuhakikisha ninadhibiti kila sehemu.”
“Mmh! Sawa, unataka kiasi gani?”
“laki mbili na arobaini.”

Baada ya kusema vile bosi aliinama na kuandika kwenye kikaratasi na kunieleza nikipeleke uhasibu.
“Kampe mhasibu.”

“Asante bosi,”nilikipokea na kushukuru.
“Kawaida tu, chumba umeishapata?”
“Simon alinieleza nikipata mkopo kuna sehemu anaijua ina vyumba.”
“Unataka uhamie lini?”

“Ikiwezekana hata leo.”
“Basi una nafasi ya kuondoka kwenda kulipia ikiwezekana leo hii uitumie kwa ajili ya kuhama kabisa.”
“Nashukuru sana bosi.”
 
SEHEMU YA 30:

Nilitoka hadi uhasibu na kumpa kikaratasi mhasibu aliyekisoma kisha alivuta droo ya fedha na kuhesabu laki mbili na arobaini na kunipa.

Baada ya kuipata ile fedha niliamini kabisa kila kitu kitakwenda kama kilivyopangwa.

Nilijishangaa kujiona nimekuwa na nguvu za ajabu, hata hali yangu ya uchangamfu ilirudi kama zamani kitu kilichowashangaza watu wengi walioniona muda ule.
Wa kwanza kunifikia alikuwa Simon na kuniuliza:

“Vipi mwenzangu?”
“Aisee mambo yamekwenda kama ulivyoyapanga jana, huwezi kuamini kila ulichokisema kimekwenda vilevile.” Nilimweleza huku nikionesha uso wa furaha.

“Mkopo umepata?”
“Ndiyo, yaani nilipomuomba hakuniuliza kitu chochote zaidi ya kuniandikia karatasi kwenda kuchukua uhasibu.”

“Na nyumbani?”
Nilimueleza yote niliyokubaliana na mke wangu kitu kilichomshtua.

“Yaani mkeo kakubali kirahisi tu.”
“Hata mimi nimeshangaa japo mwanzo alitaka kupinga lakini kauli ya kiume ilimfanya akubaliane na matakwa yangu.”

“Japokuwa kazi ni nzito, lakini mwanzo unaonekana mzuri, vipi umemtaarifu mnahama?”

“Nimtaarifu ili iweje, yeye alipohamia kule alinitaarifu?” nilimjibu kwa kujiamini.

”Kwa hiyo?”
“Bosi katoa ruhusa ya kwenda kulipia na kuhamia leo.”

“Sasa mimi nitatokaje?”
“Nimekuombea ruhusa kabisa.”
Niliondoka na Simon hadi sehemu iliyokuwa na hicho chumba na sebule, kwa kweli kilikuwa katika hali nzuri sana. Nililipia miezi kumi ili nibakie na fedha ya kubebea mzigo.

Baada ya kutoka kulipia chumba tulipita kwenye magari ya mizigo na kukodi gari hadi nyumbani. Nilipofika nilimkuta mke wangu akifua nguo, aliponiona naingia nimo ndani ya gari alishtuka sana.

“Vipi mume wangu?”
“Leo tunahama.”
“Na hapa?”
“Tunamuachia mwenyewe.”

“Mwenyewe nani?”
“Mke wangu huu si muda wa maswali, tupakie mizigo tuhamie makazi mapya.”
“Mume wangu mbona kodi yetu ndiyo ina miezi saba tu.”

“Hiyo iliyobaki atakaa mwenyewe.”
“Mume wangu mwenyewe nani, mwenyewe si sisi?”

“Mke wangu, hebu nyanyuka tuondoke.”
“Mume wangu mbona toka jana sikuelewi kuna nini?”
“Hebu kwanza tuhame kwanza muda si mrefu utanielewa.”
 
SEHEMU YA 31

“Mume wangu mwenyewe nani, mwenyewe si sisi?”
“Mke wangu, hebu nyanyuka tuondoke.”
“Mume wangu mbona toka jana sikuelewi kuna nini?”

“Hebu kwanza tuhame kwanza muda si mrefu utanielewa.”

Tulikubaliana kuhama japo kwa shingo upande, tulipakia mizigo nikisaidiana na Simon, baada ya kupakia tuliondoka na kuhamia sehemu nyingine kwenye nyumba yenye wapangaji watatu na sisi kuwa wa nne. Baada ya kupanga vitu huku mke wangu akionekana kulazimishwa sikuiangalia ile hali.

Kwa vile siku ile nilikuwa na ruhusa, nilipumzika na Simon aliondoka kwenda kwake. Tukiwa tumebaki wawili mke wangu aliniuliza:

“Sasa ndiyo unafanya nini? Tumetoka kwenye nyumba kubwa tunakuja kwenye vyumba viwili?”

“Ndiyo uwezo wetu.”
“Sasa kwa nini tumehama kule?”
“Ile siyo nyumba yetu.”
“Si tulikuwa tumepanga?”
“Na hapa tumepanga.”

“Kama tumepanga huoni tunapoteza fedha bure, si heri tungerudi kwenye nyumba yetu kuliko kuja huku?”
“Hatujapoteza ila yeye ndiye kapoteza.”
“Mume wangu mbona sikuelewi nani kapoteza?”

“Mke wangu, we mkubwa si kila kitu nizungumze unatakiwa kutumia akili.”
“Una maana ile nyumba nilipangiwa na mwanaume?” mke wangu aliuliza macho yamemtoka pima.

“Wewe ndiyo unasema,” nilijifanya sijui kitu. “Lakini mume wangu kwa nini unapenda kusikiliza maneno ya watu?”
“Mke wangu tumia akili, utajua sababu gani imetufanya tuhame kule na tusirudi kwenye nyumba yako.”

“Najua tu watu wameshaanza kupenyeza umbea, nina imani nyumba hii muda si mrefu itanishinda.”

“Haiwezi kukushinda kama utanisikiliza.”
“Nikusikilize nini, kila siku unasikiliza maneno ya nje.”

“Kwani uongo?”
“Uongo nini?” mke wangu alishtuka.
“Yote yaliyotokea siku za nyuma?” nilimueleza ya nyuma sikutaka kumueleza niliyoyashuhudia mwenyewe yaliyosababisha nitake kutoka roho.

“Basi mume wangu, lakini kumbuka kusikiliza maneno ya watu tutaachana tunapendana.”

“Unanipenda?” nilimuuliza swali ambalo naamini hata wewe utaona la kijinga. Nilimuuliza kwa makusudi pamoja na kunifanyia yote bado mke wangu niliamini bado ananipenda, nilikuwa nina imani hata yeye ananipenda.

“Nakupenda sana mume wangu.”
“Kweli?”
“Tena sana, hebu nieleze toka tuhame Uswahilini nimekukosea kitu gani kibaya.”
 
SEHEMU YA 32

“Hujawahi ila nakuomba iheshimu ndoa yetu,” niliamua kufunika kombe ili mwanaharamu apite kwa kuamini mke wangu hakuwa anajua lolote juu yake.

“Nimekuelewa mume wangu.”
Tulianza maisha mapya kwenye makazi mapya, kama ilivyokuwa kawaida ya mke wangu muda wote alikuwa mpole bila kuonesha mabadiliko yoyote mabaya.

Kila nilipokuwa kazini alipoomba ruhusa ya kwenda kwa mama yake nilimkatalia na yeye hakulalamika japokuwa aliona kama nimemnyima uhuru. Nilimueleza yeye ndiye wa kunishawishi kumpa uhuru bila hivyo nilimhakikishia safari yake kubwa ni dukani na sokoni tu.

Mke wangu alionekana kunielewa kwa kufuata yote niliyomueleza, ili kupata uhakika kuna siku nilitoroka kazini na kurudi nyumbani bila taarifa na kumkuta mke wangu kapoa kama maji mtungini.
Hali ile ilizidi kunijengea imani kwa mke wangu kuwa amebadilika.

Nami kidogo mwili ulirudi taratibu na kuonekana mtu mbele ya watu. Japo si tabia nzuri ya kumchunguza mkeo lakini sikuwa na jinsi, siku mojamoja nilimdodosa Simon juu ya tabia ya shemeji yake.

Jibu lilikuwa hata yeye hajasikia lolote baya, hata mtu aliyekuwa akimpa taarifa zile alimweleza sasa hivi kweli mke wangu ametulia. Nilimshukuru Simon rafiki yangu kwa mpango wake uliomrudisha mke wangu kwenye mstari.

Kweli moyo ukipata furaha, hata kama huna kitu maisha utayaona mazuri. Nilipendeza na kuanza kupata kitambi kwa mbali, kila mmoja aliyeniona alinishangaa nilivyopendeza kwa muda mfupi. Niliamini kero za moyo na mateso mazito yanapoutikisa mwili lazima upukutike.

Siku zilikatika huku nikifurahia maisha, kingine kilichonipa faraja ni kusamehewa deni langu na kampuni kutokana na ufanisi wangu wa kazi uliokuwa umelega na kurudia uwezo wangu wa zamani wa kujituma.

Waswahili wanasema la kuvunda halina ubani, miezi sita baada ya kubadili makazi yaliyotawaliwa na utulivu na amani, siku moja nilirudi nyumbani majira ya saa moja na nusu usiku kama kawaida baada ya kazi.
 
SEHEMU YA 33

Nilipofika nilikuta mlango umefungwa, nilikwenda kuuliza kwa jirani chumba cha pili, alinieleza kuwa mke wangu ameondoka katika gari ambalo nilielezwa lilivyo na kuufanya moyo wangu upasuke! Lilikuwa ni lile gari la mwanaume aliyekuwa akimzuzua.

Kwa kweli nilichanganyikiwa na kubakia nimesimama kama zuzu.
“Kwani vipi shemu, mbona hivyo kuna nini?”

“Hataa,” nilikataa mikono ikiwa kiunoni.
“Hapana shemu nilipokuelekeza gari lililomchukua mkeo umeshtuka na kupoteza hali yako ya kawaida na kutawaliwa na hali ya kutaharuki, kwani lile gari lina nini?”
“Ameondoka saa ngapi?”
“Saa tano asubuhi.”

“Alikueleza anakwenda wapi?” nilimuuliza huku nikiwa na shauku ya kujua.
“Hakuniambia ila aliniletea ufunguo na kunieleza ukirudi nikupe.”
“Na mtoto?”
“Ameondoka naye.”

“Alibeba nini?”
“Alikuwa na mkoba wa kawaida tu.”
“Mmh!” niliguna huku nikiinamisha kichwa na kukitikisa.
“Kwani kuna nini shemeji, mligombana?”
“Jirani si ungesikia?”

“Sasa mbona umeshtuka, msubiri akirudi umuulize, hakukuaga?”
“Asante shemeji,” niliachana na mke wa mpangaji mwenzangu na kuelekea ndani mwangu.

Nilipofika nilijitupa kwenye kochi na kutazama juu huku nikijiuliza yule bwana kampeleka wapi mke wangu.

Moyo mwingine uliniambia huenda kapewa lifti tu hakuna kingine, labda amekwenda kwa mama yake. Nilipanga akirudi nisimuulize chochote kuhusiana na kupanda kwenye gari la mwanaume ambaye alionekana shida yake kubwa ni kuivunja nyumba yangu wakati na yeye ana familia yake.

Kupanda gari lile halikuwa tatizo bali kuondoka bila kuaga kama tulivyokubaliana. Kwa upande mwingine sikumlaumu sana mke wangu kutokana na msimamo wangu wa kumkatalia kutoka hata alipoomba ruhusa.

Kingine kilichonishangaza kilikuwa kuacha nyumba bila kufanya usafi wa kitu chochote. Vyombo tulivyolia jana yake vilikuwa havijaoshwa, nyumba ilikuwa haijasafishwa, chumbani kitanda kilikuwa hakijatandikwa, mashuka yalikuwa yamekaa ovyo pia hata chakula kilikuwa hakijapikwa.

Nilijiuliza mke wangu atakuwa amepatwa na nini kilichomfanya atoke haraka na kushindwa kufanya majukumu ya ndani. Nilijikuta nikiingiwa na wasiwasi. Nikapigia simu ya mke wangu, nilichanganyikiwa baada ya simu ya mke wangu kutopatikana.
 

Ahhhhhhhh. Wanawake hatari snaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…