0713417189
Senior Member
- May 12, 2021
- 115
- 201
- Thread starter
- #81
RIWAYA : Usilie Rehema.... 01
MTUNZI : Lovi Pius Kijogoo
. 0757238304, ( whatsap )
0713 417 189
0622 738 310
Tanga.
_ SEHEMU YA KWANZA _
( 01 )
Issa akiwa ameikunja sura yake iliyogubikwa na hasira alimuita mkewe...
" Rehema"
" Abee Issa mume wangu!"
" Hivi wewe Rehema ni mwanamke wa aina gani? au una moyo wa chuma! pamoja na mateso yote haya nayokufanyia lakini bado unavumilia. kwanini hutaki kurudi kwenu! sasa nakwambia lazima nikurudishe kijijini kwenu Buseresere. Mwanamke mpuuzi sana" alifoka Isaa.
"Mimi nimekuchoka, umezeeka hufai kuwa na kijana kama mimi. Muone kwanza kifua chake kimesinyaa kama nyasi msimu wa kiangazi. Nakwambiaje usipoondoka kwangu nitakuuwa. Alafu tuone utanishitaki wapi masikini mkubwa wewe usiye na haya."
Rehema alikuwa kimya, asiamini kwamba maneno yale ya kejeli yanatoka kinywani kwa Issa ambaye ndiye mumewe. Uvumilivu ulimshinda akaamua amjibu mumewe...
"Issa mume wangu, kwanini unatoa maneno makali kiasi hicho! nami nina moyo wa nyama, maumivu nayasikia. Leo unasema nimezeeka! asante sana. Nani aliyenizeesha kama sio wewe? unaniona mimi kinyago, tahira nisiye na faida kwako. Kumbuka ni wapi uliponitoa! umesahau ni mambo mangapi nimekusaidia mpaka hapo ulipofika."
"Issa mume wangu, ukitaka salama ya Dunia chunga ulimi wako, hata kama umenichoka sio kwa manyanyaso haya. Tazama nina mtoto mdogo ndio kwanza ana miezi mitatu na ulimuita jina la mama yako ambalo ni Rabia. Lakini leo unanifukuza mimi pamoja na mwanao."
Rehema alimbeba mwanaye akamuweka kifuani kwake, huku machozi yakiwa yanamdondoka, hakuwa na lakufanya zaidi ya kusubiri aone mume wake atafanya nini.
Issa alivimba kwa hasira kama puto, hakutaka kabisa kumuona Rehema mbele ya macho yake. Akamsogelea karibu kisha akamshika mkono huku akimwambia...
"Wewe mwanamke, una matatizo ya masikio eeeeh! nimekwambia kwamba sitaki kukuona katika nyumba yangu. Niondolee mkosi shetani mkubwa wewe. Nimekufadhili vya kutosha, kwanini unaniganda kama kupe?. Narudia tena siwezi kukaa na takataka kama wewe, kama kukutumia nimekutumia sana ila kwa sasa umeisha muda wako, ondoka hapa uende ukatafute wazee wenzako"
Issa alipoona kwamba amezungumza maneno mengi yenye vitisho ndani yake, lakini Rehema alikuwa ametulia tuli. Kitendo hicho kiliuponda sana moyo wa Issa, akamzaba Rehema kibao kizito katika shavu lake. Hakuishia hapo alimzoa ngwala, Rehema akadondoka chini mzima mzima yeye pamoja na mwanaye.
Rehema aliumia sana kichwani damu zikaanza kumchuruzika, kwa bahati nzuri alimkumbatia mwanaye. Issa alimvuta na kumchukua yule mtoto kisha akamning'iniza juu huku akisema...
"Huyu mtoto naitoa roho yake leo, atakuwa sio mwanangu, mwanaharamu mkubwa huyu. Damu yangu haiwezi kutoa sura ya hivyi! hapa kwangu umechemsha nenda ukatafute Baba wa huyu Mtoto. Kuanzia leo mimi nimemkana mnataka kuniletea ushetani katika nyumba yangu? sitaki kusikia tena huyu mtoto akiitwa jina la mama yangu yaani Rabia, ikiwezekana huyu mtoto nitachukua panga nimkate vipande vipande kisha nimpikie mbwa wangu, washenzi wakubwa ninyi."
Issa alimuinua yule mtoto juu kabisa kisha akamuachia ili ajipige chini afariki papo hapo. Rehema alijitosa na kumdaka mwanaye huku akipiga kelele ..
"Jamani Issa unauwa mwanangu! niachie Rabia wangu, amekosa nini malaika wa Mungu huyu mpaka unamtupa chini! muogope Mungu wako, na kila siku unaswali wewe! Leo unaikana damu yako! unamkataa Rabia tazama mpaka mbingu na ardhi vinakushangaa. Sikuwahi kufanya mapenzi na mwanaume yeyote zaidi yako! ni wewe uliyeitoa bikra yangu nikiwa kidato cha nne mwanzoni, ni wewe pia uliyenilaghai niingie katika mahusiano na wewe, nilimaliza kidato cha nne huku nikipata daraja la tatu nilifaulu vizuri masomo ya sayansi nikaona mwanzo wa kutimiza ndoto zangu za kuwa Daktari zimeanza vizuri."
"Wewe Rehema nakuomba ufunge mdomo wako mchafu huo." alipaza sauti Issa.
"Hapana siwezi kunyamaza mume wangu, ni wewe uliyenitorosha nyumbani nikashindwa kuendelea na masomo yangu. Nilikusaidia vitu vingi sana, lakini leo unaniona mimi mpuuzi. Nilikutolea damu ulipougua, hakuna hata ndugu yako aliyekuja kukuona nikakuuguza mpaka ukapona. Unaniona sifai naiachia Dunia ikuhukumu. Ni mimi niliyekutafutia kazi katika kampuni hiyo ya kusafirisha mizigo nchi za nje, nimegeuka takataka kwako! Unaniita Malaya."
"Rehema nimekwambia ufunge huo mdomo nitakukata makofi Mshenzi mkubwa Wewe!"
"Wewe nipigie tu Issa!. Wazazi wangu walinitafuta kwa muda mrefu pasipo mafanikio na, siku walipofariki kwa ajari ya basi ulinizuia nisiende msibani, ama kweli uliamua kunitesa na kunitenganisha kabisa na ndugu zangu! saizi ni yatima mimi sijui nitaenda wapi na kijijini kabaki bibi mwenywe nasema ubarikiwe sana Issa."
Rehema alishindwa kupambana na hisia za moyo wake, hata kuzungumza hakuweza tena, akabaki analia. Lakini mumewe alikoswa hata chembe ya huruma, akaamua kumshika Rehema mkono na kuanza kumvuta mpaka nje ya geti kisha akamsukuma akadondoka chini Pamoja na mtoto wake,
_ ITAENDELEA _
OFA... OFA... OFA ....OFA
Usikose vitabu vyangu ( nakala laini ) unatumiwa kwa njia ya email au whatsap Navyo ni:- ________________====_________
Narudi Songea... 5,000/= tu!
Yolanda.....4,000/= tu!
Malkia wa kuzimu... 4,000/= tu!
Hadithi ya Suzi..... 2,500/=
Usilie Rehema.... 5,000/= tu!
________________====_________
PIA NAFUNDISHA MASOMO YA JIONI KWA WALE AMBAO WANARUDIA MITIHANI YA KIDATO CHA NNE. KIDATO CHA TANO NA SITA KWA MICHEPUO YA, HKL NA HGL.
KAMA UNAHITAJI KUANDIKIWA KITABU CHA HISTORIA YA MAISHA YAKO UNAKARIBISHWA...
NAPATIKANA TANGA MJINI,....
0622 738 310.
0713 417 189.
( 0757 238 304, whatsap )
MWL, LOVI PIUS KIJOGOO.