EMMY...... 05
Lovi Pius Kijogoo.
0757 238 304.
SEHEMU YA TANO.
ILIPOISHIA.........
Mage alimfata Emmy na kumwambia, "Tufanye tuondoke, muda umekwenda, kwani kaenda wapi huyo mzee?"
"Kaenda msalani, ngoja arudi tua..!"
Kabla hata hajamaliza kuzungumza, mzee Don alirejea, wakamwambia akawakubalia. Wakaongozana mpaka nje. Wakakuta kuna gari mpya aina ya Range Rover rangi nyeupe. Watoto wakike walipagawa, wakaingia ndani, chuma likatembea. Dakika tano tu zilitosha kuwafikisha Sahare. Mage alishuka wa kwanza kutoka ndani ya gari.
"Emmy..!"
Mzee Don aliita.
"Abeeee.!"
"Unaweza nipa namba yako, tukaendelea wasiliana hata siku nyingine!"
"Haina shida chukua!"
"Ok, ni 07..."
"Niwatakieni usiku mwema"
Aliaga mzee Don, akiwa anaisevu namba hiyo kwa umakini wa hali juu. Kisha akaondoa gari kuelekea nyumbani kwake maeneo ya Kange uzunguni.
"Sasa nachukua hatua nyingine"
Alizungumza Peter, akaichukua kalamu na karatasi. Kabla ya kuanza kuandika chochote kile, machozi yalimnyemelea machoni pake.
ENDELEA NAYO......
Kiza kinene kilikuwa kimetanda, huo ndio usiku wa manane. Waliolitawala anga ni wachawi labda na popo. Ulikuwa wasaa wao wa kujivinjari katika kumbi mbali mbali za starehe. Vibaka pia ni wakati wao wa kuiba vile visivyo vya kwao. Mahospitalini napo usiku wa manane wapendwa wetu wengi uiaga dunia.
"Huyo si ndo yule binti aliyeitwa Emmy"
"Ni kweli ndio mwenyewe"
"Loo! macho yake yamevimba na kukolea wekundu wa damu. Ishara kuwa alikuwa akilia sana. Aidha, kutokana na baridi iliyomkumbatia, hakuwacha kutetemeka. Ala!"
"Yaani shoga nilivyomuona, michirizi ya machozi ilikaukiana kwenye mashavu yake, alishiba njaa na kudondokea kinywani. Alitia huruma."
"Hahahahahahahahahahha...!!"
Wasichana hao wawili walicheka huku wakiigonga mikono yao kwa pamoja.
"Yaan Emmy, kazeeshwa na makuruhu ya ulimwengu. Alikuwa kadiri wa kimo. Ngozi yake yenye weusi uliokoza,imepauka kutokana na matatizo yaliyomsibu. Urembo wake aliokuwa nao angali bado hajaingia kwenye kinamasi cha matatizo, ulimtoroka. Japo alionekana mdogo, moyo wake uliyabeba mazito ambayo mtoto wa umri kama wake, asingeweza kamwe kuyasweka na kuyafichama moyoni. Yangelimuua kama sio kumbwaga."
"Shoga kwani kapatwa na nini" msichana wa kwanza aliuliza.
"Watu walipomuona walikisia labda kawa mwenda wazimu. Taswira hii ilijengwa na mwonekano wake. Afya yake iliyodhoofu, nywele zake zilizotumka ovyo na kujisokota kwa kukosa kusitiriwa, mavazi chakavu yaliyoshiba viraka vya kila nui, miguu yake iliyojaa magombo na kuparara mithili ya nyong’inyo ya mganga, vilikuwa ishara tosha kwa wenye fikra hasi kukata kauli kwamba Emmy karukwa na akili. Usilolijua wanasema siku zote ni kama usiku wa kiza."
"Shoga mbona wazungumza kwa mafumbo?" yule msichana alidakia huku akihoji.
"Maumivu aliyopitia Emmy, yalituama katika moyo wake. Moyo wake ulikuwa kata ya kujua siri ya mtungi. Maumivu yale kama maji yalipojaa pomoni, yalifurika. Moyo nao ulichoka kuvumilia. Neva zilipitisha ujumbe akilini. Akili nayo ilirusha waraka kwenye milizamu ya macho. Kekevu na shake. Machozi njia nnenne hayakuwacha kumbubujika kivoloya. Alikinai furaha, akajazwa huzuni ya milele. Hayo ndiyo yalikuwa majaaliwa ya Emmy binti mdogo aliyepigwa na maisha."
"Unakere bana, kama hutaki kunisimulia uache!" awamu hii yule msichana alifoka sana.
. "Hahahahahah..!"
Msichana wa pili alicheka huku akisema,
"Nawe shogaangu kwa kupenda umbeya mpaka unakasirika sasa sikia nikueleze!"
"Enhe!" akadakia msichana wa kwanza kwa umakini sana.
***
"Nafikiri shoga unakumbuka jinsi Emmy alivyokuwa mrembo?".
"Naam, mrembo wa kupigiwa mfano na kushinda tuzo zote duniani bila ushindani mkuu" alijibu msichana anayesimuliwa. Kisha mwenzie akaendelea kuzungumza.
"Sijamaliza kumbuka macho yake mazuri. Macho ya kikombe yaliyikaa lahiki kwenye vishimo vyake. Nywele zake za singa zilizokolea weusi wa kizimwili kabla ya yote kumfika. Nisikilize unakumbuka mashavu yake yalivyotutumka kutokana na lishe. Alikuwa akila vinono. Masiko yake ya mpunga yalivyokuwa yamekita vyema kwenye kichwa na kumpa tambo la kupendeza. Shingo yake ya upanga ilijikita na kukibeba kichwa chake."
"Unakumbuka tumbo lake la mlazo. kiuno chake cha nyigu na miguu yake ya cherehani iliyoviringwa kwa ustadi na Mungu. Hivyo ni jumla ya vitu vyote vilivyomfanya awe mrembo. Tofauti na sasa. Amenyauka kama mche uliokosa maji. Midomo yake imekaukiana. Ikakonda. Mashavu yake yamekondeana. Kichwa kilikonda kutokana na njaa. Mabega yake yalimpanda. Akatisha kama shetani."
"Tumbo lake lilijitokeza, sio kwa kushiba chakula bali njaa. Mikono yake ya mbinu za Mungu, ilikondeana. Ikawa kama mikwiro ya kucharazia ngoma. Akawa kama kimbaumbau mwiko wa pilau. Parafujo za mwili wake zikamlegea. Akawa zaidi ya utumbo wa samaki. Mtuo mmoja tu wa nzi, popote pale kwenye kiwiliwili chake, usingembakisha tisti. Ungembwaga kwa kishindo. Alitia huruma mtoto wa watu.
"Mamamamamam!"
Emmy alipiga kelele na kukurupuka usingizi alikuwa akiota.
"Ni ndoto gani hii, mbona sielewi!"
Ni maswali aliyojiuliza Emmy lakini hakupata majibu.
Aliota kwamba kuna rafiki zake wawili wa kike wamekaa wanamsema.
"Kwamba ipo siku ntakuwa nimeisha, na kubaki kimbaumbau, washindwe. Mwenyezi Mungu atanipigania"
Baada ya kuzungumza maneno hayo, alishuka kitandani na kuanza usafi, ile anashika tu fagio anasikia mlango unagongwa, kufungua anakuta ni Mage akiwa kambeba mwanaye mgongoni.
"Eeeh shoga asubuh yote hii, je kwema?" aliuliza Emmy.
"Kwema huyu kivuruge leo kanisumbua usiku hata sijalala!"
"Vipi anaumwa?" Mage aliuliza.
"Analia tu, nipeleke kwa Baba, namtaka Baba!"
"Hahahahahaha alooo unalo bibi weye!" Emmy alicheka huku akimpiga na fagio kwenye mguu. Wote wakajikuta wanacheka.
"Eenhe shoga, vipi lile jizee limekutafuta, sijui mzee Don!" Mage aliuliza.
"Hata hajanitafuta kipenzi, kila simu ikiita naikimbilia nikijua ni yeye lakini, nikipokea nasikia sauti nyingine"
"Kuwa mpole atakutafuta tu, wanaume ndivyo walivyo, wanajifanya hawana haraka kumbe wanajikaza tu" Mage alimpoza Emmy.
Emmy alimsimulia Mage juu ya ile ndoto. Mage akamsihi tu aipuuzie hiyo ni kama ndoto nyingine tu.
Mage alimuweka mwanaye chini kisha akaanza kuzungumza kwa utulivu kabisa.
"Rafiki yangu, japo yule mwanaume nilimkosea sana, ila nataka nimpigie simu, kupitia namba yako, huenda akapokea. Niweze kumuomba msamaha kwaajili ya huyu mtoto. Sio kwamba nataka anirudie hapana ila akitaka hivyo nipo tayari"
"Wazo zuri sana!" alijibu Emmy akachukua zile namba na kupiga simu ikapokelewa. Akaanza mazungumzo.
"Mama Ester anaongea!" alijitambulisha mage kwasababu alitumia namba ngeni.
"Nishasikia sauti yako, nakusikiliza malaya wewe" alifoka Lovi ambaye ni mzazi mwenziye na Mage.
"Sina amani katika nafsi yangu. Moyo wangu wote umepigwa na barafu la huzuni, umekufa ganzi. Najua kwamba nimekosea ila hukupaswa kuchukua hatua hiyo uliyoichukuwa."
"Nayazungumza maneno haya huku wingu kubwa la simanzi likiwa limegubika anga ya maisha yangu, huku mvua kubwa ya masika ya machozi, ikiwa inamwagika na kulowesha kichwa cha mashavu yangu." alizidi kulalamika mage.
"Mpuuzi huna la maana eeh" Lovi aligomba.
"Hapana Lovi wangu, Machozi ya kwikwi na kekevu za hapa na pale, zimeulemaza uwezo wangu wa kupumua, achia mbali uwezo wangu wa kuona. Bali na hayo, mashavu yangu yamegeuka nyanya mbivu. Najionea imani. Nilikosea sana, na kosa langu lilikuumiza sana, maana hukutarajia kama mimi, mtu wako wa karibu, ningeweza kukufanyia vile japo ukweli ni asilia ndogo sana."
"We mse.... nini? nakata simu!"
"No, usifanye hivyo Ba Ester, Kumbuka kwamba wewe ndiwe chaguo la moyo wangu. Wewe ndiye ua la moyo wangu. Kumbuka kwamba, wewe ndiwe baba wa wa mtoto wangu. Naomba hilo uliafiki kisha, tafuta sehemu katika moyo wako uweze kunisamehe. Mwanao, Ester ,analia kila uchao. Kila uchao ananighilibu kwa maswali aula ambayo mwisho wa yote, yananipa huzuni na majonzi. Nimeona siwezi kuvumilia."
"Huyo mtoto mpeleke kwa mahawala zako" awamu hii Lovi aliporomosha matusi mazito. Ila Mage aliendelea kuomba msamaha.
"Hakuna binadamu aliyetimia mme wangu. Binadamu wote waliumbiwa udhaifu na udhaifu wao ndio huwaangusha. Unajua jinsi navyokupenda mme wangu. Kumbuka chimbuko la penzi letu. Rudisha kumbukumbu zako nyuma. Naomba makosa yote uyafute na kuyatupilia mbali ili tuanze upya mchezo wetu wa mapenzi. Nipe nafasi ya pili. Nipe nafasi niungame makosa yangu. Nipe nafasi niweze kukuonyesha jinsi navyokupenda. Mme wangu, naomba... Naomba tafadhali. Nipo chini ya miguu yako huku nikiomba unisamehe, kosa langu ambalo kila uchao halinipi amani wala usingizi. Limekuwa kama dunia. Kuzunguka akilini pangu pasi na kuondoka mahali lilipo."
"Wee mbwa naona ka unanipigia kelele maskioni mwangu!"
"Sikupigii kelele Lovi, Najutia sana. Najutia ushawishi. Najutia sana. Laiti nisingeliwasikiza alwatani. Wamenipotosha na kunifanya nende kinyume na kaida zako. Lovi wangu.. Ewe baba wa mtoto wangu. Ewe kiyeyushi cha barafu ya moyo wangu. ,maji ya kitala changu. Rutuba ya penzi langu. Naomba uje umwone mkeo. Njoo umkumbatie kama zamani. Njoo umpe busu. Njoo um'papase. Njoo uwe karibu naye. Njoo tafadhali. Njoo maana ukaribu wako, utanipa ufunuo kwamba umeshanisamehe. Njoo lovi wangu."
"Sasa nakaa kimya ongea mwenyewe, si unasalio la kutosha fala weweeh!"
"No! usikae kimya. Njoo nidanganye basi unanipenda. Njoo unilaghai kwamba umeshanisamehe. Njoo unambie kwamba bado nina thamani katika maisha yako. Njoo unambie kwamba,mimi ni maisha yako na huwezi ishi bila mimi. Njoo unidanganye tu maana nimeona maisha yangu bila wewe, kama kinywa bila meno."
"Njoo uniweke karibu na USO wako. Niwe kama kitabu kizuri cha kupendeza. Njoo unichukue. Unifukie na penzi lako ninukie vizuri kama UA LA rahani. Njoo unichukue Mme wangu. Njoo tukae pamoja ili mtoto wetu aweze kupata mapenzi yote ya wazazi."
"Mwanao anakuhitaji. Analia kila siku,'baba... Baba... Babaa..." Sina cha kumwambia maana nikimweleza kwamba tumeshakosana,basi itakuwa kosa kubwa. Mwanetu ataugua kisaikolojia."
"Sitosita kukwambia asante kwa mapenzi uliyonipa. Hakika penzi lako,sitolisahau kamwe ndani ya maisha yangu. Lakini Mme wangu,jua kwamba,kila ninapokukumbuka,machozi hunidondoka. Pindi napolia,machozi huwa si machozi tena. Yanakuwa machozi ya ishara ya hatari."
"Malaya mkubwa wewe!"
Alijibu Lovi, kisha akakata simu.
************* ITAENDELEA***************
_____________________________________________