0713417189
Senior Member
- May 12, 2021
- 115
- 201
- Thread starter
- #61
MALKIA WA KUZIMU..... 17
MTUNZI: LOVI PIUS KIJOGOO
WHATSAP: 0757 238 304.
0622 738 310.
0713 417 189.
TANGA.
Janeth hakushtuka wala kujali kwa kile kilichotokea bali aliendelea na shughuli zake, wakati huo Desmund akiwa amekata tamaa pale Kitandani akisubiri roho yake kutengana na mwili muda wowote ule.
Mama Desmund alikuwa katika hali ya upweke ndani ya jumba kubwa lililotazamana na Barabara. Aliamua achukue kitabu cha picha akaanza kufunua akakutana na picha yake ya ndoa, alitikisa kichwa, akaitazama pete yake ya ndoa katika picha ile, ambayo pete hiyo akumbuki ilipotea katika mazingira gani.
Alipofunua tu ukarasa uliofuata mwili wake ulianza kuwa wa baridi. Aliogopa kutazama picha iliyokuwa mbele yake. Akiwa bado anatazama picha hiyo alisikia mdada mpya wa kazi akimuita kwamba chakula tayari, Mama Desmund alifata chakula kile kisha akarejea kuketi alipokuwa mwanzo.
Aliporudi picha ile ilikuwa bado ikimkodolea macho kwa huruma.Ilikuwa picha ya mtoto wake aliyeitwa Deus alikuwa na tabia ya kuwapa watoto wake majina ya ukoo na ubatizo pia.
Mtoto huyu alifariki miezi kadhaa iliyopita, kifo chake kilikuwa ni cha ghafla sana, hakupata hata muda wa kuzungumza na Mamake kabla ya kufikwa na umauti, alizima ghafla na kuiacha familia yake ikilia kilio kikuu,kilio kisicho na mwisho.
Mama Desmund hakutaka kuitazama tena ile picha ilimsikitisha sana. Alifunika upesi buku lile la picha. Akaamua achukue kitabu kimoja kilichoandikwa na mwanasaikolojia wa Nchini Marekani "Wiley and sons 1960" akafunua ukurasa wa mia moja tisini na moja na kuanza kusoma.
"Sikumbuki mama yangu alinibusu mara ya mwisho lini. Yawezekana jambo hilo lilifanyika nilipokuwa mtoto mchanga, kwani hakika alinibusu mara nyingi nilipokuwa ninakua. Wakati sikumbuki busu lake la kwanza, nakumbuka busu lake la mwisho."
"Miaka inapita kwa kasi, na kila uhusiano wa binadamu huleta misongo na kero. Hili si jambo la kutisha au kufedhehesha bali ni la kawaida. Lakini tukiwa na kanuni ya heshima pekee ya utii mioyoni mwetu, upendo utatawala. Kisha, kadiri misongo inavyotutisha, pengine kutusababishia maumivu na hata uchungu, tungekumbusha lile busu la mwisho maana hakika litakuja.Unataka ukumbuke nini unapowaaga wazazi wako mara ya mwisho?"
"Rafiki yangu alinisimulia kwamba baba yake alipozeeka, si wakati wote akili yake ilikuwa ikifanya kazi vyema. Hata hivyo, siku yake ya kuzaliwa ilipokaribia, rafiki yangu aliamua kumpigia simu. Alimwambia, "Heri ya siku ya kuzaliwa ( Happy Birthday, Day )" "na Mungu akubariki."
"Siku hiyo akili ya Baba ilimrudia kwani alijibu mara, "Hapana, mwanangu. Mibaraka ni yako. Mungu akubariki kwasababu siku zote umekuwa ukiniheshimu." Miezi miwili baadaye rafiki yangu alimzika baba yake. Ilikuwa faraja ya kiasi gani kwake, kuyakumbuka maneno ya marehemu baba yake!"
"Nimehudhuria mazishi machache ya kusikitisha, lakini kamwe sijashuhudia machungu zaidi na kilio kuliko wakati majuto yalipofanya huzuni ya kutengana kuwa chungu zaidi."
"Tafakari suala hili wakati bado unayo fursa, wakati bado unaweza kufanya kitu au kusema kitu kinachoweza kuleta tofauti. Tafakari busu la mwisho kwasababu litakuja. Waheshimu baba yako na mama yako na siku zako duniani hazitakuwa nyingi tu ila zitakuwa za kuridhisha zaidi zilizojaa amani, furaha na ufanisi." ( New York: Wiley and Sons 1960 ), p. 191.
Mama Desmund alizivuta pumzi zake kwa fujo kisha akazitoa nje taratibu sana.
"Nilitamani mwanangu apate kitabu hiki akisome hasa ukurusa huu kwamba " Waheshimu baba yako na mama yako na siku zako duniani hazitakuwa nyingi tu ila zitakuwa za kuridhisha zaidi zilizojaa amani, furaha na ufanisi."
"Ni kweli nimekubali kuwa mbali na mwanangu! Damu yangu, hapana, nafsi yangu inaniuma, Desmund ni mwanangu, alinyonya kifuani kwangu, leo niwe adui yake, mwanangu ananiuma sana, kama yeye haoni umuhimu wangu ila mimi bado nahitaji kuwa karibu na mwanangu" alizungumza mama Desmund huku akiwa anatazama jarada la kile kitabu, mkono wa kushoto akiwa ameuweka shavuni, na kujitahidi kulizuia chozi lisimdondoke tena.
"Furaha yangu imekanwa na ulimwengu, moyo wangu umelainika sababu ya maumivu, siamini kama kumlea Desmund ilikuwa ni sawa na muda kupoteza, nguvu nyingi kutupa. Nimesikia mwanangu anaumwa lazima niende, mimi ndie mama yake, maamuzi yangu sitakuja kuyajutia kamwe, akiamua kuniua ni sawa, ulimwengu umenichosha." Mama Desmund alizidi kunong'ona mwenyewe kwa sauti ya chini yenye kuongozwa na machungu, machozi na uzito wa moyo.
ITAENDELEA....

☆