MALKIA WA KUZIMU..... 12
MTUNZI: LOVI PIUS KIJOGOO
WHATSAP: 0757 238 304.
0622 738 310.
................................................................
SEHEMU YA KUMI NA MBILI.
( 12 )
ILIPOISHIA.....
Deus aliminina uji akaanza kunywa, akafunua masufuria akachukua ugali na kuanza kula bila hata mboga, alikuwa analia nyuma ya viganja vyake. Nywele zilikuwa chafu na ndefu kama mwendawazimu. Alipomaliza kula alisiamama akaelekea mpaka jikoni akanywa maji ndoo nzima, alivyomaliza alipotelea ukutani na taa ikazima ghafla.
Mama Desmund akiwa bado anatetemeka kwa hofu alisikia mishindo wa viatu vya mtoto wake akikimbia, pa! pa! pa! mlio huo ulimuumiza sana.
Mama Desmund alikuwa haoni tena, isipokuwa giza lililomgubika. Alijitahidi akapapasa akakaa kwenye sofa, "Deusi rudiiiiiiii" alipaza sauti lakini mtoto wake hakuitika, kitendo hicho kilimshtua sana, akaamini kumbe mwanaye hajafa ila kachukuliwa na watu wanaotegemea nguvu ya giza. Machozi yalianza kumbubujika upya yakalowanisha mashavu na kudondoka sakafuni.
ENDELEA NAYO...
Saa kumi na mbili za alfajiri Mama Desmund alikuwa amedamka tayari, kiubaridi kikawa kinapuliza kwa mbali, akafunga vimbuzi vyake vitatu pembezoni mwa nyumba yake, akashika ufagio na kuanza kukusanya uchafu uliokuwa umedondoshwa na miti ile ya matunda aliyokuwa ameipanda pale nyumbani kwake, pamoja na maradhi yake ya uzeeni hakupenda kukaa bila ya kufanya vikazi vya hapa na pale.
Alitandika mkeka wake, akaketi na kuinyoosha miguu yake, wakati akilisubir jua ambalo nalo lilikuwa likichomoza kwa maringo sana katikati ya mawingu ambayo yalikuwa yametanda katika anga. Akiwa bado ameketi pale mkekani, alimuita yule binti wake wa kazi kisha akaanza kumsimulia yote aliyoyasikia na kuyashuudia kwa macho yake japo yalikuwa yanaogofya usiku wa kuamkia siku hiyo.
Mdada uyo wa kazi alishangaa sana, hakuwahi kusikia kitu kama hicho kwamba mtu alizikwa lakini kaonekana tena akimimina mpaka uji na kunywa.
"Pole sana Bibi!" Mdada wa kazi alinena.
" Asante sana, Dunia ina mengi sana!" alijibu Mamake Desmund.
Mama Desmund alishangaa ghafla alipomuona mdada wa kazi machozi yakimdondonda,
"Umepatwa na nini tena?" Mama Desmund aliuliza kwa mshangao sana.
"Nimekumbuka mambo ambayo uwa yanauchoma na kuuralua moyo"
"Mambo gani hayo?" alihoji Mama Desmund.
Mdada wa kazi aliyafuta machozi yake kisha akaanza kusimulia.
"Nilikuwa na miaka kumi na miwili wakati vita vilipotokea pale kwetu Tarime mkoani mara. Baba yangu sikuwahi kumuona wala kumjua, sina uhakika kama nae aliuwawa katika mapigano hayo au laa..! Mama yangu alikuwa akifanya biashara ya kutembeza ndizi mbivu kichwani, jua na mvua vilikuwa vitu vya kawaida kwake. Nyumbani kwetu tulikuwa jumla ya watoto watano.
Kumbe ilikuwa ni vita ya makabira, koo kwa koo, hasa wafugaji na wakulima, sisi tulikuwa ni wakulima pamoja na ving'ombe kama vitano tu."
"Amani ilitoweka, mifugo ilikuwa ikiuliwa ovyo mashamba yakifyekwa bila ya huruma. Nakumbuka ilikuwa siku ya jumamosi jirani zetu walishambuliwa, nyumba zao zikachomwa moto, mali zao zikaporwa, watoto wakachinjwa, kiukweli ilikuwa vigumu kutembea, kula au kufanya jambo lolote lile." alisita kidogo kuendelea kusimulia, akajinyoosha na kuketi vizuri katika mkeka kisha akaendelea kuzungumza.
__________________________________________
KUPATA sehemu ya 13 mpaka MWISHO, lipia 2500 tu kwenda namba 0622 738 310. Jina lovi kijogoo. Sapoti kalamu ya mtunzi, azidi kuandika.
___________________________________________
"Baada ya majuma kama matatu kupita nyumba yetu ilishambuliwa, Mama aliuwawa katika vurugu hilo, nilisikia akilia kwa uchungu, "Mama ee! Msiniue! Nitafanya lolote mlitakalo!"
"Lakini haikuwa hivyo kilio chake hicho hakikuwagusa wala kuwaathiri ilikuwa kama dua ya kuku isiyompata mwewe. Mimi nilikuwa nimejificha upenuni na kujifunika kwa guo kubwa kuukuu ambalo mama alikuwa akianikia mihogo. Woga na hofu kubwa vilinifanya kujikunja mle kama nyoka."
"Ndugu zangu wote waliuwawa wakati huo, ni mimi tu niliyesalia, wauwaji hao waliondoka mara tu baada ya kuumaliza ukatili huo, niliondoka upenuni hapo nikatembea katika nyumba yetu iliyokuwa wazi, milango yote ilikuwa imevunjwa, niliweza kuiona miili ya ndugu zangu pamoja na ule wa mamangu mpendwa.Mama alikufa kwa uchungu mwingi, alikuwa ameuuma mdomo wa chini kwa meno! Macho yake yalimtoka kama ambaye alikuwa anagombana na ulimwengu uliompa mgongo!"
"Mwili mzima ulinizizima kutokana na hisia za kuiona mili ile, niliduwaa kwa muda, nililia Bibi! Nililiaaa Bibi, nikatamani kitokee kiumbe kitoweka nami, sikuwa na ndugu tena, kila nilipoyatazama mapanga yaliyowauwa ndugu zangu niliumia nililia kilio kisicho na mwisho, sina Baba, sina mama, wadogo zangu wote wameuawa, Bibi niliona Dunia imenibana."
Maumivu yalikuwa makali kuzungumza hakuweza tena, machozi njia mbili mbili aliyaachia yamwagike yakalowanisha mashavu yake na kudondoka kwenye mkeka.
"Pole sana! Usilie hayo ni mapito japo yanaumiza!" Mamake Desmund alijaribu kumtuliza binti yake wa kazi.
"Asante Bibi, baada ya ndugu zangu kuuwawa nikajipa moyo kwamba kwa vile mimi ni mtoto wa kike, ipo siku nitazaa watoto kisha nitawapa majina ya ndugu zangu ili ukoo uanze upya. Lakini Dunia haikupendezwa na wazo ilo, nilimpata kijana aitwae Marwa, akiniomba niwe na mahusiano naye nikakubali nilikuwa na miaka kumi na tano,"
"Baada ya muda alinipa ujauzito, akaanza sababu kwamba hajajipanga kimaisha, hayuko teyari kulea, mara nyumbani kwao hawajui kama anamahusiano na mtoto wa kike, akalazimisha nitoe mimba"
"Kwa vile nampenda nilimkubalia nikaenda kuitoa mimba, yaaani Bibi! Bibi!Bibi acha tu Bibi. Nilitokwa na damu nyingi sana, niliugua manusura nife, kijana yule alinikataa hakutaka kuniona tena, baada ya kusikia nimepoteza mfuko wa uzazi sikuwa napata hedhi tena kama mwanamke, mirija ya uzazi iliziba, Bibi nilipoenda hospitali niliambiwa nimekuwa tasa kwasababu ya kuziba mirija na kupoteza kizazi, nililia sana Bibi yangu, ndoto zangu za kuwa na familia zikaota mbawa ghafla, sitamsahau Marwa mpaka siku naingia kaburi, nilishamsamehe ila kumsahau nimeshindwa."
"Sikuwahi kukanyaga shule, hata darasa la kwanza sikuwahi kusoma, shule yangu ilikuwa ni shambani kwenda kulima basi, ningejuaje madhara ya utoaji mimba mimi?, nijibu Bibi ningejua vipi kwamba naweza kuchanika mdomo wa kizazi?, kutobolewa kizazi au majeraha ya kibofu cha mkojo na sehemu za haja kubwa!. Jamani niacheni nilie mimi, urembo wangu pasi kuwa na mtoto ni maumivu! sikujua kwamba najitafutia majuto yasiyokwisha na kukosekana kwa amani."
"Dada zangu, wadogo zangu au wanawake wenzangu kumbukeki kwamba, Maumbile tuliyonayo tumepewa na Mungu wetu, tuepuke kuyatumia maumbile yetu kwa njia imchukizayo Mungu, wapo wanawake na wanaume wengi wanaopita duniani bila kupata mtoto huku wakiutamani na kuulilia uzazi. Kama ninavyoulilia mimi hivi sasa! Lakini! nimechelewa."
Machozi yalizidi kumbubujika, ndipo Mama Desmund akamkumbatia na kumtuliza, Wingu la majonzi lilitanda nyumbani hapo, mvua ya maumivu ikazidi kucharaza! huku radi kali za mateso zikawa zinapiga na kuiunguza mioyo yao kwa simanzi. Mama Desmund alishindwa kulizuia chozi lake akaamua aliachie limdondoke aliguswa sana na maisha ya binti wake wa kazi.