0713417189
Senior Member
- May 12, 2021
- 115
- 201
MALKIA WA KUZIMU..... 01
MTUNZI: LOVI PIUS KIJOGOO
WHATSAP: 0757 238 304.
0622 738 310.
TANGA.
SEHEMU YA KWANZA
Baada ya miaka mingi kupita, bado alizidi kuikumbuka historia Mbaya na Chungu, Katika Maisha yake. Achia mbali alivyosumbuliwa na maradhi ya ajabu akiwa shule ya msingi.
Akavuta Picha Jinsi wazazi wake walivyopambana kuhakikisha anapata mahitaji yake. Alitabasamu Kidogo, alivyowakumbuka wale mabinti waliomkataa kipindi kile akiwa anasoma chuo kikuu cha Dar -es- Salaam.
Ni kijana mtanashati, mwenye kujua kupangilia mavazi yake. Mwenye urefu wa futi sita na nchi moja, mweusi kiasi ndio sifa yake kubwa, kifua chake kipana kutokana na mazoezi ya kuinua vyuma vizito. Alifahamika kwa jina la Desmund.
Kwa wafanyabiashara wakubwa wa Jijini Dar - es - Salaam, jina ilo sio geni katika masikio yao au wakazi wa mtaa wa masaki.
Kumbukumbu hiyo ya kuumiza ilipenya katika kichwa cha Desmund, akiwa ameketi sebuleni akitazama runinga.
"Mmh! Unawaza nini kipenzi changu? " aliuliza Janeth ambaye ni mkewe Desmund.
"Mmh" aliguna kidogo kisha akazungumza, "Unajua sisi wanaume tuna mambo mengi, hakika maandiko hayakukosea kwamba tutakula kwa jasho, na kuna wakati Dunia inatuelemea, pia zipo nyakati tunakata tamaa kabisa ya kuendelea kuwa hai. "
"Sasa mume wangu! Jumba lote ili bado unayawaza maisha kweli? " alidakia Janeth ila Desmund hakujibu neno lolote lile, bali aliachia tabasamu uku akitikisa kichwa.
Janeth nae aliponyokwa na tabasamu pana lisilo kifani. Akambusu mumewe katika paji la uso, akaelekea jikoni kuendelea na majukumu yake.
"Hakika nilipata mwanamke, siishiwi hamu ya kumtazama, kila siku anazidi kuwa binti mdogo, tazama hata kifua chake kilivyo chanua, kimepambwa na titi changa. Aisee ndio maana wivu hauniishi" alinon'gona Desmund kwa sauti ya chini, akacheka mwenyewe kana kwamba alikuwa akizungumza na mtu.
Ukiachilia mbali uzuri wa sura yake nyembamba, urefu wa sentimita 160, rangi yake nyeupe inamtambulisha vyema Janeth kwamba ni toto la kinyatulu kutoka mkoani singida. Ukiitazama pua yake ndogo imejichonga vizuri kama kito cha dhahabu, akikutazama usoni ni kama anakukonyeza, ilo ni jicho lake la hudhurungi, kubwa kiasi na la mviringo, lenye mng'aro wa aina yake ukifananisha na golori utakuwa hujamtendea haki Janeth.
Kwa wacheza pulutebo mnajua ulaini wa kitambaa kile basi ndivyo ilivyo ngozi yake, yaani ni nyororo, maji yanatereza tu kana kwamba yanatoka kilimani. Makalio yake sio madogo wala makubwa, ila mtikisiko wake nafuu ya tetemeko la ardhi, kwa uzuri huo wa Janeth ni haki Desmund awe na wivu kwa mkewe.
"Janeth!"
"Abee mume wangu! "
"Naona kiubaridi kinapuliza sana leo? "
"Siunaona huu ni msimu wa mvua.! "
"Kweli mke wangu joto lilizidi. "
Janeth alitabasamu kidogo kisha akasema..
"Sasa jamani joto kwa hapa Dar -es- salaam ni kawaida kabisa. "
"Ndio natambua ilo lakini ili lilizidi mpaka nikadhani uko juu angani kuna watu wanachochea kuni aisee. "
Jibu ilo kutoka kwa Desmund lilimfanya Janeth aangue kicheko mpaka akajikuta amekaa chini.
"Sasa mke wangu andaa chakula nile nilale."
"Usijali una njaa sana eeh? "
"Sio sana, ila chakula chako kitamu. "
"Hahahahahahah!!," alicheka sana Janeth kisha akazungumza ..
"Mwanamke mapishi, nisipopika vizuri ukapikiwa uko nje unaweza ukaniacha."
" Wee! Siwezi kukuacha Malkia wangu wa pekee, jinsi wanaume wengi wanavyokutamani, mimi ni wako yaani Daima na hata Milele. "
Janeth alianza kuzipiga hatua kuelekea jikoni, alipofika aligeuka nyuma ili aone mumewe anafanya nini. Akaona Desmund kainamisha kichwa chake akisoma gazeti la habari za michezo, basi Janeth alisimama katikati kisha macho yake yakabadirika ghafla na kutoa mwanga mweupe, ndipo wakatokea wasichana wanne wenye sura kama ya Janeth. Wakaanza kumsaidia kazi ya kupika, mmoja alikaanga samaki, mwingine akapeta na kuosha mchele, lakini mmoja alisimama mlangoni na kutazama kule alipokuwa ameketi Desmund.
Baada ya dakika ishirini chakula kilikuwa tayari, wale wasichana wengine wakasogea pembezoni mwa ukuta kisha wakatoweka, akabaki Janeth mwenyewe anabeba vile vyakula vilivyopikwa na kupeleka katika meza ya chakula.
"Aisee ndio maana nakuaminia!," alizungumza Desmund.
"Kwanini mume wangu? "
"Unakwenda na muda sana kana kwamba umefungwa mashine katika mikono yako."
"Hahahahahahah..!!!!" alicheka sana Janeth kisha akajibu " Natambua wajibu wangu kama mwanamke," "Hapo sibishi mahabuba wangu." alidakia Desmund.
"Mmh! mbona chakula cha leo kitamu hivi?," aliuliza Desmund. "Na kati ya siku ambazo sijapika vizuri ni leo." alijibu Janeth uku akitabasamu.
"Una mbwembwe mke wangu, chakula kitamu hivi kisha unasema hujapika vizuri" alizungumza Desmund uku akiwa anabugia kipande cha samaki aliyekaangwa.
Desmund hakuelewa nini kinachoendelea, wingu zito lilikuwa limetanda katika mboni za macho yake. Penzi la Janeth lilimlevya, alikuwa asikii wala haoni.
Hatimaye Desmund alikuwa amemaliza kula chakula, akaelekea bafuni akaoga kisha akajitupa kitandani, ni sababu ya uchovu wa siku nzima. Janeth nae alielekea kitandani kwaajili ya kwenda kupumzika.
Wakiwa kitandani walizungumza uku wakicheka, Janeth akatumia muda huo kumpapasa Desmund hasa katika kile kifua kikubwa na kipana, akakilaza kichwa chake juu ya kifua hicho, hakika mahaba moto moto yalitawala juu ya kitanda.
Janeth aliinua kichwa chake akampuliza Desmund usoni, na hapo ndipo usingizi mzito ulimpitia akaanza kukoroma. Janeth alianza kubadirika taratibu mpaka akawa joka kubwa lenye rangi nyeusi. Joka ilo likaanza kujikunja katika mwili wa Desmund.
------------- ITAENDELEA ---------------///