Simulizi: Malkia wa kuzimu-01

Simulizi: Malkia wa kuzimu-01

MALKIA WA KUZIMU..... 06
MTUNZI: LOVI PIUS KIJOGOO
WHATSAP: 0757 238 304.
0622 738 310.

................................................................
SEHEMU YA SITA. .
( 06 )

ILIPOISHIA.....

Ghafla mzee Matiku ambaye ndie mganga aliona mwanga mkali pembezoni mwa kale kajumba alikokuwa anamtibia Desmund, ila Desmund na rafiki yake wao hawakuweza kuona kinachoendelea isipokuwa mganga tu.
Katika mwanga ule akatokea binti mweupe na mrembo sana, anakadiliwa kuwa na urefu wa futi tano na nchi moja, macho ya kuvutia yenye rangi ya hudhurungi. Binti uyo alikuwa amekasirika sana! akamnyooshea kidole mganga huku akimwambia...

ENDELEA NAYO......

Nakusihi acha mara moja kufatilia maisha ya watu, ukiendelea nitakupoteza nitainywa damu yako kabla haijapoa, mimi ndie Janeth Malkia wa Kuzimu." Binti uyo alitoweka ghafla.

"Aanh! Anhaa! sasa saa" Mganga alishikwa na kigugumizi cha ghafla. "Naomba mrudi kesho kutwa, leo mizimu imegoma." ilikuwa ni sauti ya mganga akizungumza, aliogopa vitisho alivyopewa na kiumbe kile cha ajabu kilichotokea pembezoni mwa kile kijumba chake anachotibia wagonjwa.

"Sawa mzee nimekuelewa" alijibu Desmund uku akiwa anasimama kutoka kwenye ile ngozi ya fisi. Hakujua kilichoendelea pale ndani mpaka mganga kusitisha huduma.

"Umesikia rafiki yangu uyu ni mganga bingwa siunaona alivyo na madawa mengi? sasa kesho kutwa nitakuleta pia" alitamka Manumbu wakati wakiwa wanaingia ndani ya gari na kuianza safari yao kurejea katikati ya Jiji la Dar - es - salaam. Desmund alimshusha rafiki yake kisha yeye akaelekea nyumbani kwake Masaki.

"Habari ya hapa nyumbani mama? "

"Nzuri mwanangu za miangaiko? " alijibu mamake Deamund.

"Ni nzuri vipi hali yako? "

"Kwa kweli leo na kila sababu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu niko vizuri kabisa Mungu ni mwema kila wakati mwanangu!"

"Amina" aliitikia Desmund uku akimpa koti mkewe ampokee.

"Waoooh! karibu mume wangu! " ilikuwa ni sauti ya Janeth.

"Pole na majukumu! nakupenda sana kipenzi changu, kutokuwa nawe kwa masaa yote hayo uwa nahisi kuchanganyikiwa kabisa, najihisi mwenye furaha sana wakati nikiwa nawe, ni wewe pekee uliyenitoa katika dhoruba ya mapenzi," baada ya Janeth kuzungumza maneno hayo alimkumbatia Desmund kwa nguvu akambusu shavuni, akamshika mkono na kumsindikiza mpaka chumbani. Mamake Desmund alipoona mahaba hayo alisimama kwa aibu na kuelekea chumbani uku akijisemea mwenyewe kwa sauti ya chini, "Mmh! wazungu hawa wametuletea balaaa!, sisi enzi zetu hatukuwa na mambo kama hayo."

"Lakini leo mume wangu umechelewa ulikuwa wapi? " Janeth aliuliza.
"Mmh! Mmh! leo! " alisita kidogo Deamund akajikohoza kuweka koo sawa kisha akaendelea kuzungumza, "Nilikuwa kwa rafiki yangu tukipanga mipango ya biashara!." "Eti eeeh! sawa endelea kupanga hiyo mipango ya biashara!" Janeth alijibu kwa dharau, akaelekea sebuleni kwenda kuandaa chakula. Baada ya dakika kama thelathini walikuwa wamemaliza kula chakula wakaelekea chumbani kupumzika, Desmund na mkewe wakamtakia mama usiku mwema kama ilivyo utamaduni wetu watanzania, na hata nchi za Afrika kwa ujumla.

Ilikuwa ni Ijumaa siku ambayo Desmund aliamini ilishiba matumaini na inao upya wa maisha yake. Akaamini ni siku ambayo anakwenda kufunguliwa minyororo ya mateso, ndoto mbaya za usiku. Hakika moyo wake ulijawa na imani ya ushindi dhidi ya siku hiyo ya Ijumaa ambayo alitakiwa arudi kwa mganga.

Jua lilikuwa ndio kwanza linajitahidi kutokeza nyuma ya yale mawingu mazito yaliyotanda angani. Mvua nyepesi iliyonyesha jana usiku ilifanikiwa kuacha vidimbwi vya maji machafu hapa na pale kando ya barabara za jiji la Dar - es - salaam.

Desmund alijiandaa haraka, alivaa ile suti yake maridhawa ya hudhurungi, akaweka na tai nyeusi yenye madoa meupe, akazama ndani ya kabati akatoa manukato na kujipulizia, kisha akaenda kumjulia hali Mamake, akamkumbatia mkewe tayari kwa kuondoka.

"Mmh! mume wangu mbona leo mapema sana? " Janeth aliuliza.
"Kuna mzigo naenda kufata!"
"Subiri basi nikuandalia hata chai"
"Nitachelewa ngoja niwahi sawa mke wangu? "
"Sawa Baba nenda ufike salama,"
Wakati Desmund akipiga hatua kuelekea ndani ya gari, Janeth alijisemea mwenyewe kwa sauti ya chini, "Hivi uyu anadhani sijui kinachoendelea sasa ngoja." Janeth alielekea nyuma ya nyumba akafukua chini na kutoa kibuyu chenye damu ya moto ya binadamu ilikuwa ikichemka kana kwamba inatoka jikoni, akanywa kisha nyingine akajimwagia usoni na kuutoa ulimi nje uku akisema..

"Nani anataka kunijaribu mimi! nitamaliza wote," akaanza kuunguruma. "Ngruuuuuh! Ngruuuuuuh! mimi ndie malkia wa kuzimu nataka damu mbichi saa hii!! Ngruuuuuuh!" Janeth akazidi kuunguruma.

"Njoo! Njoo! Njoo! aje mmoja hapa" Baada ya Janeth kutamka neno njoo mara tatu, ghafla alitokea binti mrembo aliyefanana kama Janeth kuanzia unyayo mpaka utosi, usingeweza kuwatofautisha. Janeth akamuacha yule binti pale nyumbani kisha yeye akatoweka ulionekana moshi ukipaa juu angani kwenda kumfatilia Desmund.

"Mama karibu chai tayari!"
" Asante mwanangu nakuja!" alijibu Mama Desmund.
"Mmh! chai ya leo tamu, naona chapati laini zinatafunika kwa raha utanifundisha na mimi kupika mwanangu. Maana hata sisi wazee tunatakiwa tule vitu vizuri," alizungumza Mama Desmund uku akiachia tabasamu.

"Usijari Mama nitakufundisha,"
" Sawa mwanangu,"
Mama Desmund yeye alijua anazungumza na Janeth mkamwana wake, la ashaa!!... Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza. Yule hakuwa Janeth bali ni mzimu uliovikwa sura ya Janeth, na hata kile chakula alichokula hakikuwa cha kawaida kabisa.
"Ooh! rafiki yangu karibu sana naona umewahi, unakwenda na muda kweli wewe msomi," alipaza sauti Manumbu akiwa anamkaribisha Desmund nyumbani kwake.

"Asante sana lazima nizingatie muda sababu nina shida ndugu yangu," alijibu Desmund kwa sauti ya upole kabisa. Safari ilianza kuelekea kwa mzee Matiku ambaye ndie mganga, kutokana na kujitenga kwake na makazi ya watu aliishi pembezoni sana, walitumia takribani masaa sita kufika sababu ya msongamano wa foleni za magari ya watu waliokuwa wakienda makazini kwao.

Umati wa watu ulikuwa umekusanyika vilio na simanzi vilitawala. Nyuso za huzuni ambazo machozi yalimelemeta machoni kwao zilidhihilisha wazi kuna msiba umetokea.
"Kuna nini tena hapa!?" aliduwaa Matiku.
"Mbona kama watu wanalia!" alidakia Desmund. "Ebu ngoja tuulize kwanza," alizungumza Matiku kwa sauti ya chini sana.

"Binti habari za kwako! Kuna nini hapa?" Manumbu aliuliza. "Nzuri tu shikamoo!" "Marahaba binti ebu nieleze kwa marefu na mapana sasa!"
" Mimi ni mjukuu wa Mzee Matiku ambaye alikuwa ni mganga hapa. Dakika kumi zilizopita historia ya mji huu ilibadirika ghafla! ikawa ni historia mbaya na chungu kuisimulia,"

"Babu alilalamika kwamba kichwa kinamuuma sana! tukampa dawa aliyoitengeneza mwenyewe, tukasahau kwamba mganga hajigangi, baada ya kunywa dawa hiyo Babu alilala usingizi, usingizi wa milele, aliipa Dunia kisogo, alisafiri njia ya wote yaani alikuwa tayari amefariki Dunia."
Binti uyo aliangua kilio cha kwikwi, akakumbuka ucheshi aliokuwa nao Babu yake, akakumbuka zawadi na hata pesa alizovuna, hakika kumbukumbu hiyo ilizidi kuuponda moyo wake.

Desmund na rafiki yake walibaki vinywa wazi kana kwamba walitaka kupiga chafya lakini chafya ikagoma kutoka, taharuki kubwa iliwazonga ndani ya mioyo yao.
FB_IMG_1594922887276.jpg
 
MALKIA WA KUZIMU..... 07
MTUNZI: LOVI PIUS KIJOGOO
WHATSAP: 0757 238 304.
0622 738 310.

................................................................
SEHEMU YA SABA. .
( 07 )

"Unaona hiki nini sasa! nilikwambia kumtegemea mwanadamu ukafanikiwa ni asilimia sifuri, ona sasa mganga mwenyewe kafariki" alipaza sauti Desmund.

"Tulia, tulia rafiki yangu kila mwanzo ni mzito, mwanzo mateso mwisho furaha. Usikate tamaa hakuna kitu kigumu kwa mtu mwenye bidii" ilikuwa ni sauti ya Manumbu akijaribu kumtuliza Desmund kisha akaichukua sigara katika mfuko wake akaiwasha akapiga funda moja na kuupuliza ule moshi kuelekea juu.

"Unauona moshi huu wa sigara?"

"Ndio nauona," alijibu Desmund.

"Sasa hata ujana ni kama huo moshi ukenda hauji, sasa ndio maana nakusihi tutafute mganga mwingine akuwekee kinga ukiwa bado kijana mwenye nguvu."

"Tazama mpaka sasa hauna mtoto hata mmoja sasa hiyo ni ndoa au mchezo wa kuigiza kama ile tulioiona miaka ya themanini uko. Mimi mwenyewe sijakata tamaa sembuse wewe uliye na shida!"

"Siku zote uwa najua kwamba anayechomwa na mwiba ndiye anasikia maumivu. Sasa rafiki yangu kama umezoea mauzauza hayo ya kuitwa na marehemu mdogo wako usiku wa manane sawa. Ila mimi niko tayari tupange siku nikupeleke kwa mtaalamu mwingine sumba wanga yule ni bingwa anaweza kugeuza mchana ikawa usiku, na usiku jua likawaka, ule ni moto wa kuotea mbali kabisa."

Desmund alikiuma kidomo chake cha juu huku machozi yakimdondoka, akainua macho yake na kutazama juu angani, alionekana kusononeka sana moyoni mwake, akafungua kinywa na kumwambia rafiki yake kwamba...

"Nimekuelewa vizuri kabisa rafiki yangu, hii vita sio ya kawaida yanipasa kupambana zaidi, maana leo nimeamka nakuta nimechanjwa chale sita ubavuni kwangu. Yaani sijui ni nani anayenitesa hivi! nasema mbele yako nikimjua namkata vipande vipande bila huruma ngoja uone." Desmund alizungumza kwa sauti ya ukali kisha akaelekea ndani ya gari kwaajili ya kuondoka, hawakutaka kusubiri mazishi ya yule mganga.

Desmund alikuwa mtoto wa tano kati ya watoto sita wa familia ya marehemu mzee Theodori, waliofariki ni watoto wanne, walio hai ni wawili ambao ni Deus pamoja na mdogo wake ambaye ni Desmund. Deus anaishi jijini Mwanza na familia yake ya watoto wawili mapacha ambao ni Caren na Collin.

Ndege wa asubuhi walikuwa wameanza kuimba nyimbo zao zisizoeleweka, nyimbo za kulibembeleza jua liweze kuchomoza. Hatimaye jua lilifanikiwa kutokeza nyuma ya mawingu yaliyotanda angani. Ilikuwa ni asubuhi nyingine na ya kupendeza yenye tumaini jipya kwa wale wanaoamini usiku utakapokwisha wataweza kutimiza ndoto zao au kufanikiwa kimaisha kutoka hatua moja kwenda nyingine.

"Yaani mke wangu tangia siku nimetoka Dar - es - salaam kumsalimia mama pale nyumbani kwa yule mdogo wangu Desmund, mwili wangu umekuwa tofauti sana, kichwa kinanigonga!" alizungumza Deus akiwa bado kitandani, alishindwa hata kuamka kutokana na maumivu ya kichwa.

"Eeh! pole sana mume wangu, mbona hukuwahi kuniambia!" alijibu kwa hofu sana Sophia ambaye ndie mke wa Deus.
"Yaliyonikuta uko ni makubwa mke wangu, usiku nilikuwa silali kabisa! Kuna siku nikiwa nimelala niliona mwanamke aliyevalia mavazi meupe ila sura yake sikuweza kuitambua, kucha zake zilitisha kwa urefu! Alisogea mpaka nilipokuwa nimelala akanikalia kifuani na kuanza kunikaba shingoni. Nilishindwa kupumua nikahisi roho inataka kutoka, nikajaribu kupiga kelele nikashindwa mpaka alipoondoka. Mwili mzima uliloa jasho nikahisi moyo unakwenda mapigo mia tano kwa dakika."

Deus alishindwa kuendelea kuzungumza machozi yakazidi kumeremeta machoni kwake.

"Mke wangu mimi sitapona!" Deus alinena.
"Kwanini unasema hivyo? aliuliza Sophia.
"Kila mwanadamu lazima afe....!!.. Hii ni zamu yangu mke wangu, Lakini nakuombea Mungu akujalie afya njema uweze kuwatunza wanangu nakupenda sana mama watoto wangu."

Baada ya maneno hayo Deus alinyamaza hakuongea tena. Sophia alimshika na kumtikisa akitaka kumueleza kuwa atafanya alivyosema lakini hakujibu. Akapaza sauti yake na kumwambia kuwa atafanya lakini hakujibu alinyamaza tu, kumbe alikuwa amefariki tayari.

Huzuni kubwa ilimgubika Sophia, akaanza kupiga yowe la uchungu, majirani wakajitokeza kwa wingi wanakuta Deus ametulia tuli juu ya kitanda, amezima ghafla kama mshumaa pindi upepo mkali uvumapo.

Sophia hakuamini macho yake akazidi kumtikisa mumewe, "Baba Caren!... Baba Caren.. amka, ni ukweli umeondoka! umeniacha na nani sasa! Kipi nilichokukosea Baba Caren mpaka uondoke ghafla kiasi hicho!.Watoto wanakulilia amka, umeniacha katika kipindi kigumu sana! Niambie kilichokusibu jamani eeeh! ni mwezi tu tangia tumeamia kwenye nyumba yetu mpya umeliacha jasho lako, umeacha juhudi zako na kujituma kwako masikini ya Mungu! Dunia imenielemea mwenzenu, hiki ndicho kilio changu cha mwisho nisaidie Mwokozi wangu, iangalie roho iliyopondeka inayolia na kuhuzunika mbele ya mwili wa mume wangu. Mungu wangu njoo hima unisaidie watoto ndio kwanza wana miezi tisa!."

Sophia uvumilivu ulitoweka, moyo ukachoka kuvumilia akawa amepoteza fahamu. Watoto nao walizidi kulia, majirani wakajua labda ni njaa lakini nani angewanyonyesha sababu mama yao alikuwa bado amepoteza fahamu.
 
MALKIA WA KUZIMU..... 08
MTUNZI: LOVI PIUS KIJOGOO
WHATSAP: 0757 238 304.
0622 738 310.

................................................................
SEHEMU YA NANE. .
( 08 )

ILIPOISHIA.....

Sophia uvumilivu ulitoweka, moyo ukachoka kuvumilia akawa amepoteza fahamu. Watoto nao walizidi kulia, majirani wakajua labda ni njaa lakini nani angewanyonyesha sababu mama yao alikuwa bado amepoteza fahamu.

ENDELEA NAYO.....

Ebu chukueni yale maziwa juu ya meza tuwanyweshe," alizungumza jirani wa kwanza.
"Na ndio maziwa ambayo uwa anawapa kila siku," alidakia jirani wa pili. Watoto waligoma kunywa maziwa kana kwamba wamegundua kwamba Baba yao amefariki na hawatamuona tena katika maisha yao yote ya hapa Duniani. Kitendo hicho cha watoto hao kugoma kunywa maziwa kiliwashangaza sana majirani.

Ilikuwa yapata saa tano kamili za asubuhi, Mamake Desmund mkewe pamoja na Desmund walikuwa wanawasili nyumbani kwa marehemu, vilio vya kwikwi vilitawala.

"Mwanangu! Mwanangu! ni mimi mama yako nimekuja amka" alipaza sauti ya uchungu Mama Desmund.

"uzito wa mateso umenielemea, nani atanizika mimi jamani! watoto wangu nazidi kuwafukia ardhini kila siku, hivi wewe kifo ni kiumbe wa aina gani? ni nani wewe usiye na huruma!? uko wapi nikufate unirudishie mwanangu? Nilimzika mume wangu nikavumilia, nikazika watoto wangu wanne nikasema ni kazi ya mola, sasa nimebaki na mtoto mmoja tu! Eeh Dunia moyo wangu unavuja damu, moyo wangu unasononeka kwa uchungu, jamani ni lini! na wapi? nitaonana tena na mwanangu, Deus hivi ni kweli umelala usingizi wa milele!"

Mama Desmund hakuweza kuzungumza uchungu ulimzidi, machozi yakazidi kumchuruzika wakinamama wakamzunguka na kujaribu kumtuliza. Taratibu za mazishi zilikamilika waliamua wamzike hapo hapo Jijini Mwanza kwenye nyumba yake aliyojenga, mwili wa marehemu uliwekwa nje kwaajili ya kutoa heshima za mwisho.

Desmund huzuni kubwa ilimgubika akashusha pumzi isiyokuwa na tumaini lolote jipya, kiza kilimteka pale alipomuona kaka yake akiwa ametulia tuli ndani ya jeneza hakuweza kutikisika wala kuyafumbua macho yake alikuwa amelala usingizi wa wote! usingizi mzito.

"hivi ni kweli umeondoka kaka yangu!" alipaza sauti Desmund baada ya kumuona ndugu yake akiwa amewekwa ndani ya jeneza na ile suti yake nadhifu ya hudhurungi tayari kwa mazishi.

"Sina kaka! sina Dada! nitakuwa mgeni wa nani mimi, mbona Dunia imenipa adhabu kali moyo na hata mwili vimeshindwa kuipokea. Tazama leo mshauri wangu, rafiki yangu, ndugu yangu sitamuona tena katika maisha yangu yote yaliyosalia hapa Duniani. Busara, ucheshi na hekima zake zote amepumzika nazo ndani ya jeneza masikini ya Mungu." Desmund hakuweza kuzungumza tena huzuni ilizidi kumuunguza ndani ya moyo, machozi njia mbili mbili aliyaachia yamwagike yakalowanisha mashavu yake na kudondoka kwenye suti nadhifu ya rangi nyeusi.

Hatimaye mazishi yalikuwa yamekamilika, mwili wa Deus tayari ulikuwa umehifadhiwa ndani ya udongo mziiiiiito! udongo usiovumilika! udongo usiokwepeka na pia ni mwanzo wa safari yetu ya kuufikia uzima wa milele kama tuliishi vyema hapa Duniani.

Mke wa marehemu alipiga magoti mbele ya kaburi la mumewe uku akiwa ameikusanya mikono yake miwili kwa pamoja, " Kwa heri Baba Caren! Kwa heri kipenzi changu! Majonzi uliyoniachia katu sitoyasahau, sina tena tabasamu, roho yangu imevamiwa na uchungu usiokoma. Naiona njia ya maisha yangu ya mbeleni imejaa manyanyaso yanayoumiza, mwili wangu umepoa! Roho mtakatifu wewe ni mfariji wangu pigana vita hivi kwaajili yangu na unifariji katika jina la Yesu Kristo Amina.

Baada ya majuma mawili kupita msiba ulikuwa umemalizika, Desmund akajitolea kuhudumia familia ya marehemu. Desmund, Mamake pamoja na Janeth walirejea Jijini Dar - es - salaam, hali ya Mama Desmund ilidhoofu sana. Tangia mwanaye afariki chakula kilikuwa kichungu kinywani mwake, hivyo Desmund akamzuia mamake asirudi pwani ili awe karibu na kijana wake mpaka atakapopata nafuu.

Janeth alikuwa jikoni akiandaa samaki wa kukaanga pamoja na ndizi bukoba akatia nazi ndani yake. Hakika kilikuwa ni chakula kitamu na cha kuvutia, ilipofika saa mbili kamili za usiku chakula kilikuwa tayari wakajongea mezani na kuanza kula.
"Mama kula chakula mbona umepoa sana? " alihoji Desmund.

"Nakula mwanangu tena chakula kitamu sana!" alijibu Mama Desmund akaliachia tabasamu hafifu lisilokuwa na tumaini lolote lile lakuonana na mwanaye tena.
"Na nimeunga nazi kwaajili yako Mama, maana ninyi kule pwani hata dagaa mnaweka nazi kwasababu zinapatikana kwa wingi uko" alidakia Janeth, akacheka kidogo na kurembua lile jicho lake la hudhurungi.

"Kwenye kupika nakuaminia sana mwanangu!" alisisitiza Mama Desmund.
Hali ya hewa nje haikuwa nzuri, kulikuwa na mvua ya manyunyu, kulianza kuvuma upepo mkali kidogo, upepo wenye baridi kiasi, upepo ulizidisha kasi Mama Desmund akaelekea chumbani kwake kupumzika, vivyo hivyo kwa Desmund na mkewe.

Saa kumi kamili za usiku Janeth aliamka akamtazama mumewe usoni, akagundua kalala fofofo akampuliza machoni kumuongezea usingizi mzito mithili ya kifo. Janeth alikuwa mtupu kabisa! akasogea pembezoni mwa ukuta akapotelea ukutani.

Janeth alitokezea ufukweni mwa bahari, akiwa bado amesimama walitokea fisi wawili wakiwa wameshikilia vazi jeupe wakamvisha kisha fisi hao wakatoweka. Janeth alizipiga hatua akaingia ndani ya bahari mpaka katikati kisha akazama na kuelekea chini kabisa.

Huko chini ya bahari kulikuwa na mji mkubwa kama jiji la Dar - es - salaam au Newyork Nchini Marekani pengine tupafananishe na Paris ya Nchini Ufaransa. Kulikuwa na barabara za lami pamoja na taa ambazo ziliwekwa ndani ya mafuvu ya binadamu zilimulika kwa mwanga mkali sana! Kulikuwa pia na kumbi za starehe ambazo zilipiga muziki wa kila aina, lakini gita zao zilitengenezwa kwa utumbo wa mtoto mchanga! Kinanda ni mbavu za binadamu. Walikuwa wakiuza vinywaji ambavyo ni damu ya binadamu, maji na hata supu yao ilikuwa ni damu pia, walikuwa na viwanda vya kuhifadhi damu na wale binadamu waliowaua sababu ya kupata kitoweo.

Siku hiyo mji huo ulioko chini ya bahari ulikuwa umechangamka, ilikuwa ni siku ya kumpaka mafuta malkia wa kuzimu. Lakini viumbe wa mji huo walikuwa na nywele ndefu zinagusa mpaka chini, miguu yao ilikuwa ni kwato za ng'ombe, macho makubwa yenye kutoa matone matone ya damu.

Kengere iligongwa kuashiria malkia anaingia, Janeth akiwa ndani ya vazi lake jeupe la kimalkia, alipandishwa juu ya fisi mweusi maalumu kwaajili yake. Alipofika sehemu aliyoandaliwa aliketi juu ya moyo wa binadamu uliotapakaa damu.

"Malkia wa kuzimuuuuuuuu!" alipaza sauti Janeth. Upepo ukavuma, miti ikakatika ovyo! makaburi yakapasuka, mifupa ya miili ya watu waliofariki ikatoka ndani ya makaburi na kuelekea pale alipo malkia kwaajili ya kumsikiliza.

ITAENDELEA
 
MALKIA WA KUZIMU..... 09
MTUNZI: LOVI PIUS KIJOGOO
WHATSAP: 0757 238 304.
0622 738 304.

................................................................
SEHEMU YA TISA. .
( 09 )

ILIPOISHIA.....

Malkia wa kuzimuuuuuuuu!" alipaza sauti Janeth. Upepo ukavuma, miti ikakatika ovyo! makaburi yakapasuka, mifupa ya miili ya watu waliofariki ikatoka ndani ya makaburi na kuelekea pale alipo malkia kwaajili ya kumsikiliza.

ENDELEA NAYO....
Kiwiliwili cha mtu kilisimama na kuanza kuzungumza... "Malkia wa kuzimu karibu katika himaya yako hii," ilikuwa ni sauti nzito sana yenye mikwaruzo, alikuwa ni msaidizi wa malkia huko kuzimu.

"Tunashukuru kwa kutuletea damu kwa wingi, tuko hapa kukupaka mafuta ya heshima" kilizidi kusisitiza kiwiliwili hicho. Fisi watano wakiwa wameng'ata kitoto kimoja kimoja katika midomo yao walielekea pale alipoketi malkia, watoto hao wazazi wao wanajua wamefariki walilia kwa uchungu wakilalamika...

"Baba njoo hima utusaidie, yaani tumebeba ujauzito miezi tisa na kujifungua kwa uchungu alafu wanetu wanafariki wakiwa hawana hata siku mbili, tuonee huruma Baba wa mbinguni" hivyo vilikuwa vilio vya wanawake waliopoteza watoto wao japo waliamini kwamba wamefariki. Ila Janeth alikuwa akifanya mchezo mchafu katika wodi za wazazi, alikuwa anajibadilisha sura na kufanana na muuguzi anayekuwa zamu, kisha anaingia na kwenda kuchukua watoto huku akiweka fisi mzee kitandani! binadamu wa kawaida wao waliona ni mtoto tu.

Fisi wale walipofika karibu na malkia wakawaweka watoto wale katika chungu kikubwa cheusi, kisha wakakikaliza katika moto mkali, watoto wale waliyeyuka na kubaki mafuta tupu.

Mabinti warembo watatu, warefu sana, wakiwa na manyoya mwili mzima kama kondoo, na mkia mrefu kama ng'ombe, walichukua mafuta yale na kuanza kuzipiga hatua kusogea kwa malkia.

"Desmuuuuuuuuuuuuuuuuuund! " alipaza sauti Janeth akiita jina la mumewe, baada ya sauti hiyo kumalizika lilitokea jeneza chakavu, mbao zake zikiwa zimeoza limetapakaa udongo mzito, lilikuwa wazi ndipo Desmund akasimama kutoka ndani ya jeneza, binti mmoja miongoni mwa wale waliobeba mafuta alimshika Desmund mkono akamsogeza karibu na malkia.

Hatimaye malkia alianza kupakwa mafuta kama ishara ya heshima katika ulimwengu wao wa kuzimu. Ndelemo na vifijo vilitawala, nyimbo zisizoeleweka zikawa zinaimbwa! paka waliendelea kulialia! Bundi nao walitoa sauti za kustajabisha. Makaburi yakawa yanapasuka katikati majoka makubwa yenye vichwa viwili yakawa yanamzunguka malkia kama ishara ya heshima.

Baada ya malkia kupakwa mafuta Desmund alimwagiwa damu ya binadamu mwili mzima kisha akarudishwa tena ndani ya jeneza.

Jua lilikuwa ndio kwanza linajitahidi kutokeza nyuma ya mawingu yaliyotanda angani, ndege wa angani walikuwa wameanza kuimba nyimbo zao za kichawi kuliondoa jua baharini! Kulikuwa kumekucha.

Desmund akakurupuka kutoka usingizini, "Mmh! kumbe jua limeshachomoza! " aliduwaa akiwa anagusa ubavuni kwake, kukagua kama kuna kidonda cha aina yeyote ile.

"Mke wangu kichwa kinagonga! mbavu zinauma yaani mwili wote umejawa na maumivu, sijui ni ugonjwa gani huu!" alizungumza Desmund katika hali ya unyonge sana.

"Pole sana mume wangu itakuwa ni malaria hiyo, ngoja nikupe panado utulize maumivu ya kichwa" Janeth alijibu kisha akaelekea kabatini akachukua vidonge viwili na glasi ya maji akampelekea mumewe akanywa kisha akajiandaa na kuelekea kazini.

Desmund akiwa kazini aliamua ajiegeshe kidogo kwenye kiti, basi usingizi nao ukamchukua bila yeye kujua.
"vipi mbona unalala saizi?" ilikuwa ni sauti ya Manumbu rafiki yake na Desmund.
"We acha tu rafiki yangu" alijibu Desmund akiwa anatikisa kichwa chake kwa masikitiko.

"Kwani bado unateseka usiku?" alihoji Manumbu. "Yaani saizi ndio usiseme" alidakia Desmund, akachukua chupa yake ya maji ya kunywa akapiga funda moja kisha akaweka chupa chini akiwa anatikisa kichwa chake katika hali ya kukata tamaa.

"Sasa sikia nimeishaongea na yule mganga wa sumba wanga, kasema twende kesho kutwa tunaweza kukaa huko kati ya wiki moja au mbili"

"Mmh! wiki mbili!" Desmund alishangaa.
"Sasa mke wangu nimuache mwenyewe! wataniibia aisee, kwa urembo ule alionao"
"Kwa hiyo umeridhika uendelee kuteseka si ndio?" Manumbu aliuliza.
"Hapana sipendi kuteseka ila mke wangu nampenda sana!"
"Kwani ulimpata vipi mpaka huwezi kumuacha peke yake hata kwa wiki moja?"
"Ni historia ndefu kidogo rafiki yangu" alinyamaza kidogo Desmund kisha akaendelea kuzungumza,

"Ilikuwa ni siku ya Jumapili majira ya saa nne asubuhi, kazini sikwenda Mungu anisamehe hata kanisani sikuweza kwenda. Ilikuwa ni siku ambayo nilitaka nitulie peke yangu nikaamua kwenda ufukweni mwa bahari ya hindi. Kulikuwa hamna mtu yeyote yule! upepo mzuri ukawa unapuliza, mawimbi ya hapa na pale yakawa yanapiga na kurusha maji mpaka nilipokuwa nimeketi, ndege nao wakawa wanazunguka huku na kule wakivizia samaki, "

"Nikiwa bado nimekaa hapo ufukweni niligeuka nyuma ghafla nikamuona msichana mrembo akiwa amesimama kwa nyuma, sikuyaamini macho yangu yalipogongana na macho yake, alikuwa ni mwanamke wa kuvutia mwenye urefu wa sentimita 160, macho mazuri ya hudhurungi. Nilijikaza nikasimama na kumfata nikaongea nae mengi akanipa namba zake za simu tukaanza kuwasiliana mpaka leo ndie mke wangu."

"Hivyo ndivyo ilivyokuwa" alimaliza kuelezea Desmund.

"Hahahahahah..!!!" alicheka kwa sauti Manumbu kisha akasema, "Kumbe ulipata zali la mentali kama yule msanii alivyoimba"

"Naweza sema hivyo, ndio maana sitaki kumuacha" alijibu Desmund huku akiachia tabasamu.

"Sasa rafiki yangu nimekubali twende Sumba wanga, leo nitafunga mapema Duka kwaajili ya kwenda kujiandaa ili kesho asubuhi safari ianze" Desmund alisema.

"Sawa kafanye hivyo mimi naondoka niwahi kupeleka mboga nyumbani" aliaga Manumbu na kuondoka zake. Desmund nae hakutaka kupoteza muda alifunga duka mapema na kuianza safari ya kuelekea nyumbani, baada ya dakika kama thelathini alikuwa amefika, siku hiyo foleni haikuwa ndefu sana.

"Karibu sana mume wangu naona leo umewahi kurudi nyumbani hadi raha" alitamka Janeth.

"Asante mke wangu, nimewahi kesho nasafiri, niandalie nguo chache kwenye kile kibegi changu kidogo cheusi" alizungumza Desmund.

"Haaaa.! kila siku safari" alipaza sauti Janeth.
"Sio hivyo mke wangu, ni kwaajili ya biashara usiwe na hofu natafuta kwaajili yako sawa?"

"Sawa mume wangu nimekuelewa, kaoge mimi niende kukuandalia hizo nguo za kuondoka nazo kesho"

Desmund alitumia muda huo kumuaga mamake, akapokea baraka zote hakueleza ukweli kwamba anaenda sumbawanga kwa mganga, bali alisema anasafiri kwa shughuli za kibiashara.

Kiubaridi kikali kilikuwa kinapuliza, miti ikawa inayumba kulia na kushoto yaani shwiiiiiiii shwaaaaa shwiiiiiii shwaaaaa. Ilikuwa ni saa kumi na moja kamili za alfajiri, Desmund pamoja na rafiki yake walikuwa ndani ya basi wakielekea Sumba wanga.

"Unajua rafiki yangu huyo mganga anaitwa Mangazini" Manumbu alimnong'oneza Desmund ili abiria wengine wasisikie.
"Ok! kumbe ndio jina lake basi atakuwa ni mtaalamu sana huyo" alijibu Desmund.
Hatimaye walikuwa wamefika Sumbawanga mjini, wakachukua usafiri wa piki piki kwasababu mganga huyo alikuwa anaishi mbali na makazi ya watu, ulikuwa ni mwendo wa dakika takribani hamsini ili kufika anapoishi.

"Karibuni sana!" Mzee Mangazini alinena ambaye ndie mganga. "Asante sana tumeishakaribia" alijibu Manumbu kwa niaba.

Mzee Mangazini aliwaelekeza mahali pakuelekea, ilikuwa ni pembezoni kidogo na nyumba yake ya kuishi iliyoezekwa kwa paa zuri na la kisasa. Manumbu aliambiwa asiingie katika kajumba kale ka udongo kalikoezekwa kwa nyasi ni maalumu kwaajili ya kutibia wagonjwa wake, basi Desmund aliingia akaamuliwa aketi katika mkeka mkuu kuu uliochanika haswaa, awamu hii Desmund hakuogopa hata kidogo. Maana ilikuwa ni mara ya pili sasa anaenda kwa waganga wa kienyeji alianza kuyazoea mazingira hayo.

Mzee Mangazini alitoa vibuyu vitatu na vyungu vikubwa viwili akaviweka juu ya ngozi, akatoa hirizi kubwa tatu, moja ina rangi nyeusi ya pili nyekundu na ya tatu ilikuwa mchanganyiko wa rangi mbalimbali. Akachukua tena pembe mbili za ng'ombe, kuku weupe watatu waliokufa na kichwa cha fisi.
Desmund alipewa ashike mkono mmoja kibuyu na mwingine pembe la ng'ombe, Mzee Mangazini akaanza jukumu la kumuagua Desmund.
Alianza kumzunguka Desmund kutoka kushoto kwenda kulia na kutoka kulia kwenda kushoto akiwa anazungumza maneno yasioeleweka na yanayoeleweka pia.

"Oooh! mzimu wa Tunkamanyinyi!, mzimu wa kyamalukenye!, njoeni, njoeni mnisaidie mniambie anaemtesa huyu bwana, moto wa kabuduchwilooo mulika nione."
Mzee Mangazini alianza kuunguruma kama simba akiwa anazungumza kwa sauti nzito na ya kuogofya sana.

"Asante mizimu ya Nyarukolu kwa kunisaidia, sasa sikiliza kijana anayekutesa ni mtu wako wa karibu, mdogo wako hajafa! na kaka yako pia hajafa!"

Ghafla mganga alipigwa na kitu kama kombora usoni, akashindwa kuendelea kuzungumza. Akawa anatetemeka, jasho zikimdondonka. Janeth alikuwa amesimama pembezoni mwa kajumba ako ka mganga na ndie aliyetuma kombora ilo. Desmund hakuweza kuona kinachoendelea hakuwa na uwezo huo wa nguvu za giza.

Janeth alisogea mpaka pale alipoketi mganga, akaanza kuyeyuka na kuwa kama moshi, kisha moshi huo ukamuingia mganga, kwa hiyo Janeth ndio akawa kama mganga akaendelea kumtibu Desmund.

"Oooh! samahani kijana, nilikuwa naongea na mizimu ya mbali ndio maana nikawa kimya kidogo" mganga akasimama tena na kuanza kumzunguka Desmund akamvisha hirizi kubwa nyekundu katika shingo yake.

"Sasa sikiliza kijana" mganga alinena.

"Mdogo wako hajafa na hata kaka yako kama nilivyosema awali, na pia sio kwamba hamuwezi kupata watoto hapana, uwezo mnao vizuri wewe pamoja na mkeo, ila anayefanya yote hayo ni mama yako mzazi, na saizi unaishi nae nyumbani kwako"*

"Sio kwamba anaumwa, hapana. Ila anataka akuuwe wewe na mkeo pia, anaona mnapendana sana. Sasa anataka awatoe kafara kama alivyowatoa ndugu zako wengine. Kuokoa maisha yako ni kumfukuza nyumbani kwako haraka sana." alimaliza kuzungumza mganga akakusanya vifaa vyake na kuvirudisha anapovihifadhi.

"ITAENDELEA"
 
janeth mbwa wewe
 
MALKIA WA KUZIMU..... 10
MTUNZI: LOVI PIUS KIJOGOO
WHATSAP: 0757 238 304.
0622 738 310.

................................................................
SEHEMU YA KUMI. .
( 10 )

ILIPOISHIA.....

Janeth alisogea mpaka pale alipoketi mganga, akaanza kusambalatika na kuwa kama moshi kisha moshi huo ukamuingia mganga, kwa hiyo Janeth ndio akawa kama mganga akaendelea kumtibu Desmund.
"Oooh! samahani kijana nilikuwa naongea na mizimu ya mbali ndio maana nikawa kimya kidogo" mganga akasimama tena na kuanza kumzunguka Desmund akamvisha hirizi kubwa nyekundu katika shingo yake.
"Sasa sikiliza kijana" mganga alinena.
"Mdogo wako hajafa na hata kaka yako kama nilivyosema awali, na pia sio kwamba hamuwezi kupata watoto hapana, uwezo mnao vizuri wewe pamoja na mkeo, ila anayefanya yote hayo ni mama yako mzazi, na saizi unaishi nae nyumbani kwako"
"Sio kwamba anaumwa hapana ila anataka akuuwe wewe na mkeo pia anaona mnapendana sana sasa anataka awatoe kafara kama alivyowatoa ndugu zako wengine, kuokoa maisha yako ni kumfukuza nyumbani kwako haraka sana." alimaliza kuzungumza mganga akakusanya vifaa vyake na kuvirudisha anapovihifadhi.

ENDELEA NAYO......
Desmund aliduwaa, moyo ulimpapa na kumtweta, alikiuma kidomo chake cha juu huku machozi yakidondoka, alihisi moyo unakwenda mapigo mia mbili kwa dakika, akashusha pumzi iliyojawa na chuki, akasimama na kutoka nje ya kale kajumba chakavu anakotibia mganga.

"Vipi mambo yameenda vizuri?" alihoji Manumbu, kwasababu yeye alibaki nje ya kajumba ako ka mganga. Desmund hakujibu kitu alikuwa kama kachanganyikiwa.

"Aisee! Desmund sinaongea na wewe lakini!" Manumbu alisisitiza kwa mara ya pili.

"Rafiki yangu wewe acha tu!" Alizungumza Desmund akiwa anayafuta machozi yake.

"Yaani mganga kanieleza kila kitu kama tulikuwa nae nyumbani, kuna vingine sikumwambia ila kajua kifo cha mdogo wangu na kaka pia! hakuishia hapo kazungumzia kuhusu mimi na mke wangu kutopata mtoto. Kumbe yote hayo yanafanywa na mama yangu mzazi! Na yuko mbioni kuniua, mganga kasema nimfukuze haraka sana"

"Jamani mbona hatari hii!" alidakia kwa sauti ya juu Manumbu.

"Sitaki tena kumuona mama yangu katika maisha yangu yote yaliyosalia hapa Duniani, na nitamuua kabla ya yeye kufanya hivyo mchawi mkubwa huyo, kumbe anasali unafiki tu" alizungumza Desmund akiwa ameikunja sura yake kwa hasira, akamshika rafiki yake mkono wakaondoka kwenda kutafuta usafiri wa kurejea Jijini Dar - es - Salaam.

Janeth Akiwa chumbani kwake alicheka kwa sauti ya juu, aliushangilia ushindi wake akaamua aende akaoge kwenye bafu la nje lakini hakufunga mlango, kama dakika 50 zilipita lakini bafuni palikuwa kimya kabisa. Mamake Desmund alikuwa ameketi mbali kidogo akiota jua, alivyoona ni takribani dakika hamsini zimepita mtu hatoki bafuni ikabidi asimame akajaribu kufungua mlango, ile anavuta alikumbana na joka kubwa likiwa bafuni, alipiga kelele akakimbia, ndipo Janeth akatoka bafuni.
"Umekuaje Mama?" Janeth aliuliza.
"Nimeona joka kubwa bafuni!" alijibu Mama Desmund akiwa anahema juu juu.

"Mmh! Wala itakuwa hujaona vizuri ni mimi nilikuwa nakoga" Janeth alijibu.
Basi Mamake Desmund alisimama taratibu maana alikuwa amedondoka chini sababu ya uwoga uliokithiri, akaelekea chumbani kwake kwenda kupumzika, hakutaka kutumia tena bafu ilo la nje.

"Nakuja jamani!" alipaza sauti Janeth, baada ya kusikia kuna mtu anagonga geti kwa nguvu sana kana kwamba anataka kulivunja, alipofungua anakuta ni mumewe akiwa ameikunja sura yake kwa hasira, alivimba kama puto.

"Kulikoni tena?" Janeth aliuliza, lakini Desmund hakujibu.
"Mama yuko wapi?" alihoji Desmund kisha akalibamiza geti kwa nguvu.

"Yuko ndani!" Janeth alinena kisha akatabasamu maana alikuwa anajua kinachoenda kutokea.

"Mamaaaa..! Mamaaa..!!" alipaza sauti Desmund, Mamake akaitika na kuja sebuleni.

"Mama uchawi unakusaidia nini? umemuua Baraka, kaka Deus nahisi na ndugu zangu wote wa tumbo moja, umefaidika na nini mama?, na bado unataka kuniua na mimi! Wanao wa kuwazaa unawatendea hivyo! leo na mimi nakumaliza ondoka kwangu mchawi mkubwa wewe" alifoka kwa sauti ya juu Desmund, akaenda jikoni akachukua kisu.

"Mwanangu nimeanza uchawi lini mimi! kwanini unanitendea hivyi? uchungu nilioupata leba leo niue wanangu kweli jamani!?. Umetonesha donda langu ambalo bado bichi kabisa, umenikumbusha wanangu waliofariki, unanishikia kisu mimi mama yako! basi njoo unichinje mwanangu ili nife wewe ubaki na amani hapa Duniani. Sitaki nikukwaze. Nakupenda sana mwanangu" Mama Desmund hakuweza kuendelea kuzungumza akakiuma kidomo chake cha chini huku machozi yakidondoka.
Yule mpangaji wa chumba cha uwani alisikia kelele akaingia ndani anakuta Desmund ameshika kisu anapiga hatua kwenda kumchoma Mamake.

"Hapana usifanye hivyo!" alikemea kwa sauti ya hofu mpangaji huyo.
"Acha nimmalize kwanini aue ndugu zangu" alijibu Desmund.
"Sikiliza ndugu yangu, Abraham Lincoln alisema, "Vile nilivyo au vile ninavyotarajia kuwa ni kwasababu ya mama yangu" sasa kwanini unamfanyia hivyo mama yako?" alisisitiza mpangaji huyo.

"Kwenda huko na wewe, nitakufukuza hapa nyumbani uende kuishi kwa huyo Lincoln wako" alijibu Desmund kwa hasira sana.
Desmund aliingia chumbani kwa mamake akakusanya nguo na kumtupia miguuni kwake. Mama Desmund alikuwa analia tu kama mtoto mdogo.

"Mwanangu niliyekuzaa leo unanitupia nguo zangu! Unanitusi mwanangu, naumia sana nani atanizika mimi? wewe ndie mwanangu wa pekee uliyebakia" alizungumza kwa huzuni sana Mama Desmund.

"Utazikwa na wachawi wenzako" alidakia Desmund akasogea alipo mamake na kuanza kumvuta kumpeleka nje ya nyumba yake.

"Mwanangu unanivuta kama mwizi, mwili wangu umekufa ganzi, Eeh Baba wa mbinguni unauona moyo wangu ulivyopondwa pondwa na magumu ya Dunia. Hiki ndicho kilio changu cha mwisho, niokoe Baba moyo wangu unavuja damu! Iangalie roho iliyopondeka inayolia na kuhuzunika mbele yako."

"ITAENDELEA"
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom