bioto
JF-Expert Member
- Oct 1, 2017
- 1,261
- 2,099
- Thread starter
- #41
SEHEMU YA AROBAINI 40
ENDELEA.........
Nikiwa nipo kitandani mawazo yanaanza kunijia
lakini niliamua kulala ndoto ya ajabu ilinijia. Sura ya
bwana Kibona inakuja machoni mwangu
ikinikumbusha mambo mengi sana ambayo
yalifanya kurudisha kumbukumbu zangu ndipo
nikaamka. sasa nikakumbuka kule nyumbani
ambako nilikuwa ninaishi kwa mara ya kwanza
kabla ya haya matatizo. Nikakumbuka pia kuwa
nina familia yangu ambayo nilikuwa nayo miaka
kadhaa, pia nikakumbuka kuwa kuna familia ya
kibona ambayo nilijiahidi kuwa mimi pekee ndie
nitaitunza. Ndoto ilikuwa na maana tosha kwangu
kutimiza ile ahadi yangu lakini mawazo makuu
kuhusu ile alama niliyonayo kwa mkono wangu wa
kuume. Nilipata kuangalia sana ile alama kisha
nikaamua kulala. Lakini nilipanga nikiamka asubuhi
nianze kwenda kule nyumbani pamoja na familia
yangu ili nikazidi kurudisha kumbukumbu zangu
labda naweza kujua chochote.
Asubuhi na Mapema sana niliamka na kuvaa nguo
ambazo yule mama Penina alikuwa kaninunulia.
Mama Penina ni Mkuu katika moja ya ofisi za
serikali mtoto wake aliondoka na kwenda kusoma
nje za nje kabisa, hivyo sikupata kumfahamu
mapema. Baada ya kuvaa kwa kweli sikukumbuka
hata kusafisha mdomo na uso kwani kwangu
ilikuwa ni kawaida sana vitu kama hivyo kutofanya.
Nilitoka na kuikanyaga sebule kubwa nika angaza
huku na kule ili kuona kama kuna mtu ananiona
nilitoka na kushika kitasa cha mlango lakini nyuma
yangu ulisikika mlango ukifunguliwa na sauti ya
salamu ikitawala sebule. "Mnali umeamkaje?.."
niligeuka nyuma uso kwa uso na mama mwenye
nyumba. "Salama mama sijui za kwako". Nilimjibu
jambo ambalo lilimshangaza kidogo. "Ebu!..njoo
tukae hapa kwenye kochi kwanza..." niliuachia
mlango kisha nikafika pale kwenye kochi.
"Unaelekea wapi asubuhi yote hii saa kumi na mbili
kasoro haya na hii si kawaida yako..". Nilibaki
kuduwaa tu. "Nimbie kuna kipi ambacho unataka
kukifanya?". "Mama..kuna kitu nimekumbuka nataka
nirudi kwanza kule nyumbani kwangu kwa mara ya
kwanza". Yule mama alisimama kwanza
"Khaaa!..ina maana unaanza kurudisha
kumbukumbu zako?...basi ngoja nimueleze dereva
akuchukue hadi huko". Nilimkubalia na baada ya
hapo maandalizi yakaanza. Tuliianza safari mnamo
majir av y saa tatu asubuhi taratiibu tukielekea
nyumbani. Nilimuomba kwanza anipitishe kule
baharini ili kuna vitu nikapate kuona. Mwendo wa
dakika kadhaa nilifika ufukweni na yule dereva.
Baada ya kushuka nikamuomba aendelee na safari
yake na ikiwezekana arudi kabisa kwani mimi
nitarejea mwenyewe huko nyumbani. Nikiwa
nazunguka pale. ndipo nikagundua jambo ambalo
lilinifanya hata nighaili kuendelea na kazi
niliyoiendea. Nilirudi nyuma kisha na kuongoza njia
ambayo ilinifikisha kwenye nyumba ya mshana.
Kumbukumbu ilinifanya nijue kuwa rafiki yangu
nilimuacha kwenye wakati mgumu sana. Hapo
ndipo hasira zilinishika na laiti wangekuwa karibu
basi ningefanya hata mauaji dhidi yao. Niliamua
kurudi ufukweni. Kwa kweli hali ya ufukwe uko
kwenye hatari sana maana watu hawakai kutokana
na matatizo yanayoendelea kutokea. Ukimya
ulioendelea kutokea pale ndipo na mimi nikaanza
kutafuta ukweli hata nije kukumbuka kitu. Maji
yaliyokuwa yanapiga pale ufukweni nilijihisi mpweke
sana kutokana na ile hali. Mwendo wa dakika
kadhaa nilifika hadi maeneo ya nyumbani lakini
sikupata kupaelewa vyema kutokana na ile sehemu
kuvunjwa na kujengwa jumba la kifahari. Ajabu zaidi
nilifika hadi kwa mjumbe ambae anaishi karibu
yangu pale lakini hakuweza kunipa msaada thabiti
ambao ungeweza kunipa matumaini kwangu.
Alinifukuza kama mnyama na akitaka nisionekane
kabisa yale maeneo. Nilirudi kinyumenyume kisha
nikaelekea kwenye nyumba ya mke wa marehemu
Kibona ambako nilifanikiwa kumkuta akiwa na
watoto wake wawili. Hali yao kwa kweli hairidhishi
kwa muonekano wa kawaida maana umasikini ndio
sababu ya kuwa dhoofu. Alivyoniona hakuweza
kuamini kama ni mimi pia mimi sikuweza kuamini
kama nitamkuta huyu mama. Kwa sababu siku ya
mwisho kuonana basi yeye aliondoka kijijini kwenye
familia ya mumewe ili akapate hifadhi. "Shemeji
habari ya miaka mingi.." uchungu ukiwa umemshika
machozi ya huruma yakimtoka, mwili wake ukiwa
mwembamba kutokana na ukosefu wa chakula
bora. Pia akiwa na mtoto mdogo mchanga sana
aliyekuwa akimnyonyesha jambo ambalo lilinipa
shaka kidogo. Kibona tangu afariki miaka takribani
sita mpaka saba sasa huyu mtoto mchanga
imekuaje sikutaka kuuliza sana maana nilijua sasa
anaishi na mume mwingine. "Salama
shemeji..angu.." tukiwa tunaangaliana pale
tukajikuta wote tunadondosha chozi. "Mnali...kwa
nini huniulizi kuhusu huyu mtoto?." Kwa kweli
nilijisikia aibu sana na uchungu mkubwa hasa
nikiangalia ile familia. "..mnali uliniahidi kuwa
utanitunza lakini ona sasa nimebakwa na ndugu wa
kibona huko kijijini na wakanifukuza kwa kuniita
mimi kaaba..Mnaliii hali yangu mbaya
sana..njamaniiiii" nilipatwa na uchungu mkubwa
sana pale ndipo nikapata wazo la haraka haraka
sana. "Shemeji! Kweli ila ukweli ninao mimi pekee
kwa nini nilishindwa kuwa karibu na wewe labda
niseme mpaka kuwa hapa ni mapenzi ya mungu
maana niliyoyapitia yanadhihirisha uwepo wa mungu
kwangu...sasa nimekuja kukuchukua tukakae kule
ambako mimi naishi sawa hapo itakuwa na
usalama wa wewe kukupa huduma kwa urahisi
sana". Shemeji kwa kweli alikuwa mgumu kukubali
kuondoka pale nyumbani kwake lakini nilimforce
sana hadi alipokubaliana na mimi japo sikuwa na
uhakika wapi nampeleka huyu mtu pamoja na
familia yake. Lakini nilipata wazo kwenda kwenye
nyumba ile ya Mshana ambayo zamani tulikuwa
tunaishi. Muda ulipotimu wa saa tisa jioni ndipo
tunaingia hadi ndani mulikuwa shaghala baghala.
Ndani ya dakika kadhaa tayari tulishamaliza usafi.
***********************
Majira ya jioni nikiwa na shemeji pale kwenye ile
nyumba ndipo gari linaingia na hawakuwa wengine
bali ni yule dereva akiwa na yule mama kiongozi.
Walishuka na kutukuta mimi na shemeji yangu
tukikoka moto kutokana na baridi kali. Walishuka
ndipo wakajumuika na sisi pale. "Mnali naomba
kuongea na wewe tafadhali..." nilitoka pembeni
kisha tukaanza kuongea "..mnali unajua unajiweka
kwenye hatari kubwa sana...unafahamu wewe kwa
sasa ni mtu wa thamani sana kwenye hili
eneo?...shida ni nini na huyu mama ni nani.."
Nilivuta pumzi kidogo " huyu ni mke wa Marehemu
rafiki yangu anaitwa Kibona nakumbuka katika hali
halisi ambayo naikumbuka nikiwa kwenye kile
kisiwa nakumbuka nilikutana nae. Ila nilimuahidi
huyu mama kumuhudumia ndio maana safari yangu
ilifika kwake na kumchukua mama huyu." Ndipo
maamuzi ya mwisho yalikuwa ni kuwaacha pale ili
kesho t utajua tunawasaidia vipi. Tuliwafanyia
utaratibu wa chakula usiku huo kisha sisi
tukaondoka hadi kule kwa yule mama. Usiku nikiwa
nimelala ilinijia sauti ya ukumbusho kutoka kwa mtu
nisie mfahamu ikisema. # CHAKULA_CHA_MWE
NDAWAZIMU_HUPIKWA_NA_WENYE_KUS
AZA_CHAKULA . Hii kauli ilinitia mashaka sana
ilijirudia sana kichwani mwangu mara kwa mara.
Nikajaribu kupotezea ndipo ikaja kauli nyingine
ambayo kama roho fulani ikiniambia
# Tulilolifanya_ni_funzo_kwako . Naamka asubuhi
akili yangi hainipi kabisa kutokana na ile kauli mbili
za usiku. Niliwaomba wanipeleke kwa mke wa
marehemu kibona. Sikutaka hata kusubiria chai na
nini niliwataka mara moja kwenda kuwaangalia.
Kweli tulipanda gari mara moja hadi kule kwa
Mshana. Aaaaah! Sikuweza kuamini kabisa
nilichokuwa nakiona. Maiti tatu zikiwa kitandani
pale mke wa kibona na watoto wake wamefariki
iliniuma sana tena sana. Sikuendelea kuchunguza
chochote pale. Baada ya siku tatu kupita mazishi
yaliisha huku nikitafakari kwa yale yanayonikuta
mara kwa mara. Tulikutana nyumbani kwa yule
mama Penina pamoja na mwanangu Asante baada
ya kutoka masomoni kwake. Mama Penina
alinipasha habari pale. "Mnali! Kuna mambo hapa
nataka kukujuza" niligeuka na kumsikiliza. "Ile siku
ya msiba pale nilipata barua iliyoandikwa kwa damu
hii hapa.." alinipa ile barua kisha nikaanza kuisoma.
Ilisomeka hivi. """Sasa ahadi umeshindwa kuitimiza
sasa tuna siku chache kuja kuikamata dunia"""".
" haya niambie ahadi gani hiyo na akina nani
wamemuua yule mama wa watu kule kwenye
nyumba?". Nilishindwa kumjibu kwa ufasaha
kutokana na kichwa changu kuuma sana. Wakati
huo yule mke wangu ambae tayari kaolewa na
mwanaume mwengine alikuja juu kwa kunituhumu
mimi huku akizidi kumpandikiza chuki mwanangu.
"Mama Penina kwa kweli huyu mwanaume ni muuaji
kabisa hafai kukaribiwa na huyu mwanangu acha
akae na mimi hutokuja kumuona anakuja hapa
tena.." maneno makali ambayo nilikuwa
nashambuliwa pale huku nikizidi kubanwa zaidi kwa
maneno ya shombo. Japo mama penina aliniombea
msamaha lakini haukuweza kusaidia. Mwisho wa
muda waliondoka kabisa mule ndani na kutuacha
sisi. "Ebu nambie ukweli mnali kuhusiana na hii
barua..". Nilitulia kisha nikaanza kumueleza kila kitu
ambacho nilikuwa nakikumbuka. "Ukweli ni
kwamba....ndio hivo niliyafanya hayo nika ahidi
kuwafanyia hayo ili nipate kuwasaidia ndugu zangu
ambao walipotelea huko..". "Pole sana hapo naweza
kukusaidia kabisa inatakiwa tuelekee kwa mtaalamu
mmoja hivi ambae yeye anaweza kutusaidia
kurudisha mwili wako wa halali na tukaanza kazi
ambayo nilitaka unifanyie." Siku ya pili mimi, mama
penina pamoja na dereva tulielekea mkoa wa jirani
kwa mganga mmoja maarufu tulipofika tulimueleza
kila kitu ambacho kinanisibu. Alianza kwa kucheka
sana na kunisikitikia kwa majonzi sana huku
akiniambia "kijana wangu upo na wakati mgumu
sana..una alama ambayo inawafanya wao wakuone
na wakufuate mara kwa mara popote ulipo. Na
ahadi uliyoiweka ya kuwasaidia wao wapate wafuasi
ndio itakugharimu sana maishani mwako". Daah!
Kila mmoja wetu alisikitika sana. "Sasa
unatusaidiaje baba". Alisema yule mama Penina.
"Mimi sitowatoza hata senti ila niwaombe nyinyi
mtanisaidiaje mimi ili nipate njia ya kuwasaidia."
Tuliangaliana pale "sema babu tupo tayari". "Sawa
dawa yake ni ndogo sana nenda baharini wewe
mwenyewe usiku a saa sita, kisha chukua maji
kwenye chupa, ukifika nyumbani andaa udi 12 alafu
sita ichome alafu sita ivunjevunje alafu itie kwenye
maji ya bahari ukimaliza hapo paka kama mafuta
kwa siku tatu tu utaona mabadiliko. Mabadiliko
yake ni kuondoa hiyo alama na kukurudishia
kumbukumbu wewe". Tulielewana kuwa baada ya
kufanikiwa ndipo nitakuja kumuona pale kwake kwa
ajili ya kumshukuru....