bioto
JF-Expert Member
- Oct 1, 2017
- 1,261
- 2,099
- Thread starter
- #21
SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA 21
ENDELEA.......
.......Mlango unafunguliwa na kuingia Vijana kama
watatu ambao sikuwa nawafahamu kwa sura, bali
kwa idadi kutokana na wao walikuwa wakinimulika
tochi usoni na kufanya nikose nuru.
"Eheee! Kwa hiyo bwana Paul hakuona vijana wa
kufanya nao kazi hatari kama hii na wakakutumia
wewe?".
Mmoja wao aliongea aliyeonekana kuwa kama
mkubwa kati ya wale watatu. Lile swali halikunifanya
nijibu kwa haraka kama vile ambavyo wao walihitaji
nijibu bali nilibaki kuwa kimya. Hii yote kutokana na
kichwa changu kupokea maumivu makali ambayo
yalisababishwa na purukushani za kutwa nzima hadi
nyakati zile.
"Kijana! Sisi hatuna shida na wewe kabisa,
tunachohitaji ni kujua unaeje huyu bwana Paul?"
"Mimi sijui chochote".
Nilimjibu.
Lakini ilionyesha wazi kuwa jibu langu hakulizika
nalo maana alisimama kisha akainama tena na
kuniangalia
"Unasemaje?"
Aliniuliza swali lilelile
"Mimi sijui chochote"
Alinizaba kibao cha maana, kilichonipeperusha
kama mzoga hadi ukutani na kujikuta napata
maumivu ya zaidi.
"Aiseee! Muite mzee mara moja nitamuua huyu".
Ndipo yule kijana mwingine kati ya wale wawili
waliobakia alitoka na kuelekea nje ya chumba
tofauti na pale.
"Kijana, nakuambia hivi huyu anaekuja ni mkatili
sana sasa mjibu upuuzi wako alafu utajua nini
atakufanya nyang'ao nyoooooooh!".
Dawa ya mjuaji au baunsa ni kukaa kimya tu wala
usijibujibu ovyo.
Punde tu wanaingia wawili. Taa iliwashwa na kunipa
mimi nafasi ya kuwaona wote wa mule ndani. Huyu
aliyeongezeka nadhani ndie alikuwa mkuu au mzee
wao ambao walikuwa wanamzungumzia.
Yule jamaa aliwaomba wale waondoke kwanza,
baada ya kuondoka ndipo akachuchumaa na
kunitazama kwa makini.
"Kijana unaitwa nani?"
"Naitwa Mnali"
Nilimjibu
"Ooooh! Wewe kijana sio mgeni kwa hilo jina lako,
bwana Paul ni mtu mdogo sana kwenye biashara,
sasa alinipa taarifa zako juu ya wewe kuwa
ukimsumbua sana".
"Lakini sio kesi, nahitaji unifanyie kazi yangu tofauti
na hapo nakuua"
Nilishtuka sana kiukweli,
"Kazi gani hiyo".
Alikuwa anacheka.
"Hahaaaah! Hahaaaa! Aaaaah"
Nilibaki kumtazama tu huku nikitafakari ile kauli
yake.
"Wewe ni mvuvi hodari si ndioo!"
"Ndio ndio kazi yangu hiyoo"
"Sawa! Kuanzia sasa acha kufanya kazi na Paul.
Mimi nina kazi yangu ya kuuza madawa ya kulevya,
sasa nitakutumia wewe kuuza".
"Hapana kiukweli siwezi kufanya hiyo kazi mimi, na
pia naomba uniachie tu maana mimi ni mtu duni
sana sina cha kukulipa au kukupa zaidi utanionea
bure".
"Hapana wewe ni muhimu kwetu na kama
utasumbua tunakuua".
Tulichukua kama dakika kama kumi tukizozana
ndipo mzee akapandwa na hasira akamuita kijana
mmoja aliyepo nje.
"Nataka huyu usiku huu.."
Akiwa anaangalia saa
"Saa! Saba...mpatieni Adhabu si hapa! Pelekeni
kokote kule piga mpaka afe! Pumbavu hatutaki
ushahidi..akiachwa huyu polisi watatusumbua
uaaaaa!".
Hilo ndilo lilikuwa tamko la huyu jamaa kuwa
niuliwe lakini si pale kwake.
Nikiwa nasubiri kinachoendelea, ghafla kwa nje
nilisikia gari likinguruma. Ndipo nikajua maandalizi
ya mimi kwenda kuuliwayalikuwa tayari.
Mlango ulifunguliwa na mimi nikachukuliwa
mkukumkuku hadi kwenye gari.
Vijana wapatao sita sasa walinizoa moja kwa moja
njia kuu kuelekea huko ambako walitaka kuelekea
kutimiza azma yao.
Njiani nikiwa naomba mungu anisaidie kikombe kile
kisinikute, nilijikuta nakumbuka mambo mengi ya
nyuma ambayo yalinipandisha hasira sana.
Nilishindwa kufanya chochote.
Walizidi kusonga mbele zaidi majira ya usiku, mimi
nikiwa nawasikiliza sina uwezo kwani hata nikipiga
kelele hakuna ambae anaweza sikia.
Kwa mbali sauti ya maji yakinguruma kutokana na
mawimbi ya bahari, ndipo nikajua kuwa napelekwa
baharini, baharini wakiniua kwao ni rahisi kunitupa
humo.
Nikakumbuka kifo cha Kibona alivyokufa, alifia mule
baharini tena kwa hila za hawa watu hasa za bwana
Paul. Bwana Paul anafanya kazi, anamiliki hotel
nyingi, lakini pia anafanya kazi za uuzaji wa madawa
ya kulevya, akishirikiana na huyu jamaa ambae
simfahamu kabisa.
Safari ilifika mwisho hadi kwenye ufukwe wa bahari
ambako kulikuwa kimya kabisa, kwa kuwa ni usiku
mnene. Walinitoa mkuku mkuku na kunitupa kwenye
mchanga.
"Moris!..."
"Naaam!"
"Tunafanya lipi, kupiga kwanza na kumtupa au
tunamtupa moja kwa moja".
Nilimsikia mmoja akiwa anaongea hivyo.
"Hapana! Hawezi kutupwa hivihivi, huyu ni mvuvi pia
anajua kuogelea! Tupige tuvunje nguvu kisha
tunamaliza kilain".
Nikiwa pale chini, nilihisi kama wale viumbe ambao
nilikutana nao kule kisiwani, wananiangalia kwa
huruma sana, pia niliona kama yule rafiki
niliyekutana nae kule kama namuona kwenye macho
yangu yenye kutoa chozi la hasira.
Kama unafahamu kuwa baharini kuna hali ambayo
inaonyesha harufu ya samaki. Ile harufu yake
nilipata kuivuta kwenye pua zangu na kuanza kuhisi
msisimko.
Wakati najikongoja kuondokana na ile hali ndipo
nashindiliwa teke, nikaanguka tena chini, akaja
mwingine akanipiga nondo ya mguuni
nikashtuka na mguu nikahisi umevunjika kwa
maumivu wakati wanavuta bangi zao na wengine
wakivuta kupitia viganja na pua zao, walianza
kunicheka kwa dharau..
"Haaaaa! Haaaaa! Lazima ukasalimie kuzimu
mbaaaaafu!"
Nilijaribu kuomba msamaha kwao ili wasiendelee
kunidhuru lakini majibu yao yalinikata maini.
"Jamanii mimi masikini, nisietaka shari na mtu,
nimetoka kwenye matatizo na mpaka leo hii
nahangaika nipate kumsomesha mwanangu naomba
mnisameheee"
"Haaaa! Una mtoto wewe! Ina maana una
mwanamke! Huyo mwanamke unampa
nini...anaitwa nani huyo demu maana wewe unakufa
yeye tunaenda kumhudumia sisi.."
"Jamani kuweni na huruma! Familia yangu inaishi
kwa mwingine..mwanangu anaitwa Asantee.."
"Oooh!!! Haijarishi kwetu hilo kukuua wewe sisi
tunapata pesa ndefu...."
Wakaanza kunivutavuta pale kama mpira wa kona.
Hapo sasa mwili unachachamaa kubadilika baada
ya kupata harufu ya nyama ile ya samaki. Nilijikuta
nikipiga keleleee.
"Kimbieniiiiiiii....msije karibu yanguuuu".
Walinicheka na hapo wakiwa na nia ya kuja
kunimaliza kabisa waondoke.
Aiseee! Nguvu na shauku ya kila kiungo cha mwili
wangu kufanya kazi ilikuja, sielewi hata ilikuwaje
maana nilikuja kujitambua Karibu alfajiri hivi kidogo
gari kwa mbali nilizisikia.
Niliamka na kuangalia pale chini yote mizoga na
wengine hawana viungo kama mkono pamoja na
uso hautamaniki.
Ghaaa! Nilistaajabu baada ya kuona lile tukio la
ghafla na hatari kwangu.
Gari naliona wale watu walikuwa sita. Pale chini
wako tano hata sikuwa naelewa kwa lile tukio kwa
kuwa sifahamu. Niliona vyema nijifiche kwanza,
niliiba mtumbwi wa karibu yangu kisha nikaingia
ndani ya maji na kukaa kwa mbali hivi nione nani
ambae alifanya lile tukio au ilikuwaje...