bioto
JF-Expert Member
- Oct 1, 2017
- 1,261
- 2,095
RIWAYA:: MAISHA YANGU YA UVUVI
MTUNZI:: Author Mudhihili
SIMU:: 0652667153
LINDI-RUANGWA
SEHEMU YA KWANZA 01
ENDELEA..............
.................Niliweza kuishi Maisha ya tabu baada
ya kufukuzwa kazi ambayo niliamini kuwa ndio
kitegemea uchumi wangu. Maisha yangu kiukweli
nilishindwa kuendelea kwa kuwa Nilishindwa
kumudu familia niliyonayo. Nilibahatika kuwa na
watoto wawili nikiwa na mke wangu.
Baada ya kukaa kwa muda mrefu sana ndipo siku
moja mke wangu aliniita. Nilienda kumsikiliza pale
alikoniita.
"Mume wangu nina jambo nataka kukushauri".
Moyo wangu uliahtuka baada ya kuona jambo la
ajabu sana kwa mke wangu. Kwani sikubahatika
kupata neno kama hilo kutoka kwa mke wangu.
"Ehee! Nakusikiliza mke wangu nambie".
Nilimuelea huku nikikaa vyema ili nipate nipate
kunsikiliza vizuri.
"Unajua kuwa mpaka sasa tuna maisha magumu
sana pia, mtoto wetu hapa anahitaji ada ya
shule...unaonaje ukatafuta kazi".
Mke wangu aliniambia.
"Kiukweli, Mke wangu jambo ambalo unaliongea
limeniingia akilini kabisa, ila sasa nilikuwa nawaza
kazi gani ambayo itaniwezesha kupata Fedha kwa
muda mfupi ili nifanikiwe na kujikwamua na maisha
haya?"
Nilibaki nikiduwaa baada ya kumueleza jambo lile.
"Sawa ila kumbuka kuwa Mtafutaji hachoki na
akichoka basi kapata, sitaki nikuvunje moyo tafuta
kazi yeyote halali pia mafanikio hayaji kwa wepesi
kama unavyofikilia jitihada zako ndizo zitafanikisha
kupata yale uyatakayo, kikubwa sisi tutakuombea
mungu na utafanikiwa kabisa".
Maneno ya Mke wangu, yalinifanya nijione kuwa ni
mtu wa kipekee kabisa.
Nilijiona sasa mwenye nguvu na kuamini kama
kweli nina mke ambae anapenda sana mafanikio
yetu.
Nilimpa moyo kuwa nipo tayari kufanya kazi yeyote
halali ambayo inaweza kunipatia kipato cha halali.
"Mke wangu hakika nakushukuru, wewe ni mke
ambae unajua majukumu yako ndani ya familia hii
nakuahidi kuwa naelekea sasa hivi kwa bwana
Kibona nadhani nikirudia nitakuwa na akili mpya".
Nilimuacha Mke wangu akiwa anaendelea
kunisindikiza kwa macho yake yaliyojaa mapenzi na
huruma. Safari yangu ilifika hadi kwa bwana Kibona.
Nilimfika hadi kwa bwana Kibona, nilimkuta
akitengeneza Mtumbwi wake vizuri. Kwa maisha ya
Pangani ambayo niliyazoea kama huna elimu basi
utaishia kuvua samaki mtoni au baharini.
"Bwana kibona, habari yako ndugu naona hapo
mambo yamepamba moto".
Nilimsalimu.
"Eeeh! Ni kweli ndugu bwana karibu sana nilikuwa
namalizia hapa kutengeneza huu mtumbwi kisha
nifungefunge nyavu yangu hapa kisha baadae
nielekee kazini".
Nilitamani sana ile kazi japo nilikuwa na uwoga
nayo mwanzo. Kitu ambacho nilikuwa nina hofu
kubwa kutokana na maji ya bahari aikupenda kua
karibu nayo kwa kuwa sikujua hata kuogelea.
Bwana Kibona alinikaribisha kwa bashasha sana
ndipo nilipomsogelea na kuketi karibu na yeye.
"Ndugu yangu kama unavyofahamu kuwa tangu
niache kazi yangu kule nina muda sasa, na halo
yangu kama unavyoifahamu sina hili wala lile
nilikuwa naomba sasa unishauri au hata kunipa
kibarua katika kazi zako hizi ili niweze kupata
chochote kitu."
"Mh! Teh teh teh! Teh......bwana unanishangaza
sana.."
Alikuwa anacheka baada ya kauli yangu kumueleza
kuwa nipate hata kibarua kupitia kazi yake ya Uvuvi.
"Sasa unacheka jambo gani?" Nilimuuliza
"Unajua, bwana Mnali ukisema kuwa nikupe kibarua
unanishangaza sana kwa kazi gani hapa...sema
tuungane tuifanye kazi hii kwa pamoja na si eti
nikupe kibarua..."
Nilimshukuru sana maana niliona sasa matumaini
yangu ya kuendelea kuishi vyema mimi na familia
yangu ilionekana. Niliondoka pale na kunyoosha njia
ya nyumbani huku nikiwa na Imani kubwa sana ya
kupata kazi kupitia kwa bwana Kibona.
Nilipofika nyumbani nilimuita Mke wangu kisha
nikamueleza kwa kila kitu ambacho kiliendelea
mimi na Kibona.
"Mke wangu ndio kama hivyo nimeongea nae na
kazi yenyewe ni Uvuvi........"
Nilishangaa kumuona mke wangu akikasirika baada
ya kumueleza kuwa kazi ya uvuvi. Ilinibidi nitumie
nguvu ya ziada kuendelea kumuuliza na kumtuliza.
"Sasa...wewe umenishauri nitafute kazi lakini mbona
sasa umebadili na uso?"
"Ndio ile kazi mbaya bwana Mtu mwenyewe hujui
hata kuogelea kabisaaa ukidondoka humo ndani ya
maji nani atakuokoa...tafuta nyingine".
Maneno yake yalionyesha hali ya ukakasi kwangu
lakini sikuwa na jinsi ilibidi nilazimishe lakini bila
hata yeye kujua, niliamua kufanya kazi ile mpaka
pale nitakapohisi nina uhitaji wa kutafuta nyngine.
"Sawa mke wangu ila itakubidi uvumilie mpaka
niikpata........"
Majira ya jioni bwana Kibona aliniambia kuwa nifike
kule kwake. Nilielekea na nilimkuta akiwa
anamalizia kupanga shughuli zake. Baada ya
kumaliza alinijia na kunikamatisha vifaa kadhaa
ikiwemo Magunia yaliyowekwa kwenye ndoo.
Nilibeba zile ndoo huku akili yangu ikiwaza
nyumbani kwa mke wangu pindi atakapojua kuwa
nipo baharini.
Yote niliyaacha na nikafanya kile ambacho kipo
mbele yangu. Tulifuatana hadi baharini muda
ulikuwa jioni sana na kiza kilianza kuingia zaidi.
Tulipofika sehemu hiyo bahari ilikuwa shwari kabisa
mawimbi hayakuwa makubwa sana yalikuwa
madogomadogo. Tulikaa kusubiri muda ufike usiku
hapo ndipo aliponielekeza mambo kadhaa.
"Ndugu yangu umekubali kufanya kazi hii lakini
fahamu kuwa inahitaji uvumilivu sana,juhudi pamoja
na ushujaa......kuna kukosa na kupata".
Baada ya hayo maneno ndipo tukaelekea kwenye
mtumbwi.
Safari ilianza kufika kwenye kina kirefu cha bahari.
Niliwasha chemli ndipo tukatundika nyavu kisha
tukatulia. Kibona alikuwa mzoefu mimi nilikuwa
muoga sana hata kusimama pale kwenye mtumbwi.
"Ukijifanya muoga haki ya nani utaishia humuhumu
ndani ya Maji kuwa makini". Kibona hakuwa mzito
alinieleza ukweli kabisa uliotokana na uoga wangu.
Baada ya muda tukaanza kuvuta nyavu na hatimae
samaki wakubwa wakubwa tuliwakamata.
Tulifika ufukweni na kutupa nyavu iliyokawa nzito
sana.
"Eeeeeeh!, hakika leo ni maajabu sana sijawahi
kupata samaki wengi kama hawa tangu nianze kazi
hii tena wakubwa sana...."
Alinishangaza kiasi kwamba nikajihisi kuwa mimi ni
mtu mwenye bahati sana. Muda ulikuwa umekwenda
ndipo Kibona aliniruhusu nifike nyumbani kisha
adubuhi na mapema niweze kurudi kwa ajili ya
kuangalia Mapato.
Kwa kawaida baada ya kuwapata samaki basi
wanunuzi wengi sana wanajitokeza pamoja na zile
biashara za kuagiza ambazo ndio nyingi sana.
Niliondoka majira yale japo yalikuwa magumu sana
yani muda mbaya. Nilimuodikia Mke wangu. Kumbe
alikuwa hajalala alikuwa ananisubiria mimi.
Alifungua mlango, niliingia nilimsalimu lakini hata
hakuitikia. Nilichofanya nikaelekea chooni haraka
nilioga kisha nikarudi kitandani. Mke wangu alinijua
kuwa natoka baharini kutokana na harufu ya samaki.
Asubuhi na mapema bado alikuwa kanuna japo
nilijua kipi kimemfanya anune.
"Mke wangu nitarejea muda si mrefu"
Japo nilimuambia lakini hata hakujibu. Nililazimisha
kuondoka asubuhi hiyo kuelekea kwa bwana kibona.
Nilimkuta tayari kashafanya biashara na akanipatia
kiasi cha pesa na ndipo nikarejea nyumbani.