Simulizi la Bibi, maisha ya Da es Salaam ya Tanganyika

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
Dar es Salaam ya Tanganyika ilikuwa na fursa nyingi sana za kazi kwa vijana. Vijana wakitoka mikoani na walipata ajira na kuendesha maisha yao. Ajira nyingi zilikuwa Bandarini kazi ya ukuli, hii ilikuwa ni nguvu yako tu, wengi walikua ni vibarua wa siku. Kulikua na kazi za Reli, kung’oa majani relini hii nayo ni nguvu yako tu, kibarua cha siku.

Wale waliojua lugha ya mkoloni kidogo walifundishwa kupika na kuhudumia wateja. Hawa walipata kazi mahotelini. Ajira ya u house boy kwenye makazi ya wazungu ilipatikana. Hii ilihitaji sana reference, kama mjomba ndiye mpishi wa Bwana Smith, una chance kubwa ya kuwa gardener au yaya wa bwana Smith. Gardener, yaya, mpishi, dereva wote walipata mkataba wa kazi na waliweza kukopeshwa nyumba za National Housing kwani walikua na uhakika wa mshahara.

Makuli wengi walitokea Kigoma, Tabora, hasa ile njia iliyokuwa ya Watumwa kutoka Ujiji. Wengi walipata viwanja Kariakoo mpaka Magomeni na walijenga nyumba za udongo na makuti. Hawa ndiyo walikuwa kupangisha vyumba kwa wageni walioingia mjini.

Maisha kama mke wa kuli, inabidi uwe na mafuta ya karafuu, mume akitoka kazini wife, ale baada ya hapo umchue mgongo na miguu alake vizuri na kesho aende kibaruani.
Mazuri ya Dar ya Tanganyika yalikuwa mengi sana.
 
Kuna mzee wangu mmoja sasa ni marehemu Allah amsamehe makosa yake, alikuwa akihadithia jinsi alivyopata kazi ya uhouse boy, kuoa mpaka kupata nyumba. Anasema zamani waliishi vizuri sana!
 
Asante simulizi ina uhalisia Wamanyema( Asili yao Kigoma) ni miongoni wa wamiliki viwanja vingi Kariakoo na Magomeni.
Wengi wa wamiliki wa viwanja sehemu hizi hasa Kariakoo wamejikuta wakiogelea kwenye utajiri baada maeneo hayo kugeuka sehemu za biashara. Sijui ni namna gani wametumia fursa hii kwani kwa jinsi mambo yanavyobadilika huenda baada ya muda Kariakoo isivutie tena wafanyabiashara wengi hivyo kipato kupungua.
 
Miaka ya 90 enzi za Mzee Ruksa lilitoka tamko, wakazi wote wa Kariakoo wajenge maghorofa. Wengi waliuza na kusogea nje ya mji. Waliobaki wemeingia mikataba kwenye majengo ya kisasa (apartments).
 
Dar ilikua miaka ya 90
IMagomeni, tazara club, railway club, kwa machein, shentembar na kumalizia na BONGA BAR
 
Kiswahili kigumu sana kwa wale wanaolitumia kama lugha yao ya pili

Neno SIMULIZI halina wingi wala kidogo, singular au Plural

SIMULIZI zangu ..ikiwa SIMULIZI ni nyinyi
SIMULIZI yangu...ikiwa SIMULIZI moja

Grammar hiyo inatumika kwenye neno PIMGAMIZI vile vile..
 
Dar es Salaam ya Tanganyika ilikuwa na fursa nyingi sana za kazi kwa vijana. Vijana wakitoka mikoani na walipata ajira na kuendesha maisha yao. Ajira nyingi zilikuwa Bandarini kazi ya ukuli, hii ilikuwa ni nguvu yako tu, wengi walikua ni vibarua wa siku. Kulikua na kazi za Reli, kung’oa majani relini hii nayo ni nguvu yako tu, kibarua cha siku.

Wale waliojua lugha ya mkoloni kidogo walifundishwa kupika na kuhudumia wateja. Hawa walipata kazi mahotelini. Ajira ya u house boy kwenye makazi ya wazungu ilipatikana. Hii ilihitaji sana reference, kama mjomba ndiye mpishi wa Bwana Smith, una chance kubwa ya kuwa gardener au yaya wa bwana Smith. Gardener, yaya, mpishi, dereva wote walipata mkataba wa kazi na waliweza kukopeshwa nyumba za National Housing kwani walikua na uhakika wa mshahara.

Makuli wengi walitokea Kigoma, Tabora, hasa ile njia iliyokuwa ya Watumwa kutoka Ujiji. Wengi walipata viwanja Kariakoo mpaka Magomeni na walijenga nyumba za udongo na makuti. Hawa ndiyo walikuwa kupangisha vyumba kwa wageni walioingia mjini.

Maisha kama mke wa kuli, inabidi uwe na mafuta ya karafuu, mume akitoka kazini wife, ale baada ya hapo umchue mgongo na miguu alake vizuri na kesho aende kibaruani.
Mazuri ya Dar ya Tanganyika yalikuwa mengi sana.
Hivi kumbe Yaya Toure yawezekana kwao ni Dar Es Salaam‍🦯‍🦯
 
Back
Top Bottom