EvilSpirit
JF-Expert Member
- Jun 15, 2017
- 13,278
- 20,900
Mzee jumaa yu wapi
Je, hiki ni kisa halisi au fiction?Yaani ndio mimi usiku ndio siwezi kupost kabisa naisoma huku naogopa
Ahsante mkuu japo mzee Juma hajaonekana tenaPole mkuu
Asante kwa hii burudaniSubiri basi nilipie mpenzi nitaleta nyingi
Sehemu ya 103.
Nilipofika nyumbani Manzese na kumuelezea yule kaka yangu kuhusu matatizo yaliyonipata kwa jinsi alivyoyapokea, nilianza kuhisi kuwa, huenda aliniona muongo. Huenda nilifukuzwa tu kwenye nyumba kwa matatizo ya kutolipa kodi, sasa nilikuwa nahitaji msaada wa makazi ndiyo maana nimeamua kusingizia matatizo ya kutisha.
"Kwa hiyo sasa kuhusu kutengeneza hayo majeneza umeamuaje, utaachana nayo au kwa sababu umehama kule kwa mtu uliyekuwa unamdhani ndiye mbaya wako, utaendelea?" aliniuliza tena.
"Akili zangu zinaniambia niachane kabisa na kazi ya kuchonga majeneza," nilimjibu.
"Unaweza kunipa sababu tatu za kuacha kutengeneza majeneza?" aliniuliza akinikazia macho.
Nilikaa kimya kwa muda kisha nikamwangalia na kumjibu.
"Kwanza kabisa, imenifanya niishi bila amani kwa muda mrefu sasa," nilimwambia akatingisha kichwa kuonesha kuwa anakubaliana na mimi.
"Pili, kwa sababu mambo yenyewe yana nguvu ya ushirikina, naweza kusema niendelee nikajikuta napoteza maisha hivi hivi hata kama nitakuwa nimehama kule!"
Alitingisha kichwa tena kuonesha kunielewa.
"Tatu inabidi nitulize akili kwanza kuhusu mambo ya majeneza kwani naamini ndiyo yaliyoniletea matatizo yote haya."
Yule kaka aliniangalia na kuniambia kuwa, hata yeye aliponiuliza alitaka kusikia mtazamo wangu lakini ukweli ni kwamba hakubaliani na mimi kuendelea kutengeneza majeneza.
Basi usiku huo huo tulikodisha gari na kwenda kuchukua vyombo vyangu nyumbani kwa yule bibi. Lakini mwenyewe hatukumkuta. Tuliambiwa ametoka, lakini hakuna aliyejua alikwenda wapi!
Nilimwaga yule jirani yangu niliyekuwa nikiangalia Tv kwake, naye akanitakia kila la kheri akisema kuwa, kila lililotokea ni mpango wa Mungu wa Israel.
Kwa hiyo nikawa nimehama rasmi nyumbani kwa yule bibi na kukaa kwa yule kaka yangu.
Pesa za kutafutia chumba kingine cha kuishi nilikuwa nazo, lakini niliamua kuwa, nitakuwa hapo kwa kaka yangu kwa siku kadhaa nikipumzisha akili na mwili pia.
Kesho yake asubuhi nilikwenda kazini kama kawaida. Nilifanya kazi zangu kama kawaida ingawa nilikuwa naogopa kama angetokea mtu na kusema anataka kuchongewa jeneza ingekuwaje?
Kwenye saa tisa hivi, nilimuona yule mama jirani akitokea kwa mbali huku ameshika begi kubwa mkono wa kulia na kimkoba kidogo mkono wa kushoto.
Alionekana kutabasamu huku akiniangalia kwa hamu kubwa.
Alipifika, nilimpokea begi kubwa mpaka nyumbani kwake. Aliniuliza za siku nyingi nikamjibu salama.
Lakini kwamba alisafiri mimi sijui.
Nilipomuuliza akasema aliondoka wiki mbili zilizopita kwenda Moshi.
Alipata safari ya ghafla na alishindwa kuniaga kwa sababu aliondoka asubuhi sana na mabasi ya Moshi yanayoondoka saa kumi na mbili asubuhi.
Alinichangamkia sana na kunionyesha upendo wote. Moyoni niliamini jirani huyu ndiye mwenyewe, lakini yule aliyekuwa akinifanyia visa siye, ni wa kugeza tu ili niamini ni huyu.
"Kumbe jirani yangu ulisafiri bwana," nilimwambia nikiwa siamini.
"Ee mwanangu, kakini kazi vipi, zinaendelea vizuri?" aliniuliza.
"Vizuri tu."
"Sawa," alinijibu.
Nikarudi kazini kwangu na kuendelea na kazi zangu kama kawaida.
Mpaka jioni inaingia sikuona mtu kutaka kutengenezewa jeneza wala kusema amefiwa. Wala yule mama sikumuona akija na vituko vyake. Na watu walikuwa wakiingia na kutoka kwake kama zamani.
Wengine niliokuwa nawafahamu waliingia huku wakimuuliza huju nasikia, "Kumbe umerudi?"
Jioni nilipofunga kazi, nilikwenda kumwaga mama nikamkuta yupo na wanawake watano wakisali. Walisema wanasali jumuiya, nikaaga na kuondoka zangu.
Mpaka nafika kwa kaka sikuona kituko wala maajabu.
Usiku nililala kwa amani na sharehe mpaka asubuhi iliyofuata nikaamka na kwenda kazini. Nikajua mambo yaliisha siku ile ile nilipoangalia yale mahubiri kwenye Tv.
Ndipo nilipobaini kuwa, yule bibi mwenye nyumba ndiye aliyekuwa mbaya wangu, ila alivaa sura ya watu mbali mbali akiwemo yule mama jirani ili kujificha nisimjue kama ni yeye.
Mpaka ninapoongea kwa kaka nilihama, sasa hivi naishi Mwembechai, kazi yangu ni hii hii ya useremala, lakini sichongi majeneza wala kuyahifadhi kazini kwangu.
Naogopa sana! Tena sana! Baadhi ya watu kwenye nyumba tunazoishi ni wabaya sana. Mtu unapanga kwake halafu anakufanya mbuzi wake!
Anakufunga akilini huku akikuchezea anavyotaka. Ni dhambi kubwa kwa Mungu.
MWISHO.
Asante mpenzi kwa kushukuru ila inatisha
Asante mpenzi kwa kushukuru ila inatisha