Jina la Mtunzi: Emmanuel Venance Hatari
Jina la Simulizi: Ni Yeye Pekee.
Sehemu ya: 1.
WhatsApp: +255768753437.
“Kila siku huwa na bahati yake” ni maneno aliyojisemea kijana Paul Gabriel pamoja na kutoswa mara kwa mara na msichana murembo aliyempenda kwa dhati kutoka moyoni lakini kila akijaribu kuurusha mtego kwa siku nyingi sasa alizojaribu msichana huyu amekuwa akimkataa. Paul anaifunga safari pasipo kujali akiamini kuwa huenda siku ya leo ikawa ni bahati kwake amechoka kuyavumilia maumivu yakulikosa penzi la murembo Johari, Msichana wa ndoto zake, fahari ya maisha yake na aliamini hakuna mwanamke anaweza kuja katika maisha yake na akailete furaha ambayo aliitarajia kuipata iwapo atafanikiwa kulipata penzi la malkia Johari. Safari hii ilikamilika nje ya geti la nyumba ya kina Johari ni nyumba ya mzee Mosses Kaseke baba mzazi wa Johari. Paul alijiandaa vyema kwa nidhamu iliyokuu alilisogelea geti hilo lenye hadhi ya juu sana eneo hilo la Nyakato national housing kisha huku akiwa na hofu moyoni geti lile taratibu ilichukua dakika mbili mpaka wahusika kuja kulifungua geti hivyo pamoja na kuisikia sauti ikimkaribisha lakini alipaswa kusubiri kwa muda.
Dakika mbili baadae mlango ulifunguliwa na zikakutana nyuso zenye furaha, Paul anakutana na tabasamu zito kutoka kwa Johari Mosses. Paul alihisi kama amepigwa shoti ya umeme lakini haraka haraka aliona huenda ni maigizo maana kulingana na majibu ya awali aliamini hiki kinachotokea saa hivi hakiwezekani na siyo rahisi. Kwani vijana hawa wamekuwa na historia mbaya mno katika mahusiano yao toka awali hivyo tabasamu la Johari lilimshishitua Paul akabaki kaduwaa maana alikuwa na hofu bado lakini baada ya kulichunguza aligundua hakuana ulaghai ndani yake bali lilitoka moyoni. Paul alijikuta akitanua mikono yake kuliandaa kumbatio kutoka kwa msichana wa ndoto zake na hapo ndipo mfuko uliokuwa mikononi mwa Johari uliporushwa na kutua vyema usoni kwa Paul. Kisha alisonya kwa dharau huku akitabasamu, ni maji yaliyooshewa samakini yalikuwa yamehifadhiwa kwenye mfuko wa plastiki ni samaki aina ya sangara nadhani kwa wakazi wa mwambao wa maziwa makuu mnaelewa ninachokimaanisha. Maji yaliyooshewa sangara yanashombo mbaya mno lakini yakilala hutoa harufu mbaya kuliko maelezo na sasa Paul alikuwa kaoshwa maji ya sangara tena yaliyolala. Paul anajaribu kujifuta na kuondoa baadhi ya takataka kama vile utumbo na magamba yaliyoganda kichani kwake baada ya kumwagiwa maji hayo machafu.
Pamoja na pigo hili Johari aliona kama haitoshi bali alimsakama kwa matusi na maneno yasiyofaa hata kusikilizwa.
“Paul umefuata ninia nyumbani kwetu?.... nilishakwambia je?” Paul alikuwa kimya kwani watu walijazana kumshangaa na walizidi kuongezeka kutokana na kuvutiwa na tukio hilo. Johari huku akipaza sauti aliongea bila uwoga wala hofu.
“Ukiambiwa sikutaki inamaanisha mtu hakutaki…. I hope sasa utakuwa na jibu kamili kuwa sikutaki… Huna hadhi yoyote katika maisha yangu…. Huna hadhi yakuingia ndani ya familia yangu pia hauna hadhi yakunipenda mimi …. Wewe ni masikini mpika vitumbua hebu watafute walio na hadhi kama yako.” Ni manno yaliyouchoma moyo wa Paul alijaribu kutembea akigeuka huku na kule huku aibu ikiwa imemtanda alinuka kama shimo la taka huku mongoni akiwa na lundo la nzi wakishangilia. Watu wengi waliokusanyika eneno lile walimsikitikia maana waliumizwa na kitendo alichofanyiwa na wengine wakimzomea. Paul alitegemea huenda leo Johari angekuwa amebadilisha msimamo wake na kumuonesha upendo kutoka moyoni lakini sasa imekuwa tofauti kabisa maana alichokutana nacho kinamuumiza maradufu. Paul anajaribu kutafuta njia ambazo hata kutana na watu kwa hali aliyokuwanayo kiukweli ilisikitisha mno alitia huruma kumuona na ilikuwa ni aibu kukutana na watu kutokana na harufu kali iliyokuwa ikimtoka alininuka kam\a gari la taka kwa waswahili hawakukosea waliposema gari la taka nalo taka. Ninaweza kusema alikuwa hajielewi maana moyo ulikufa ganzi ghafla baada ya tukio hilo na uvumilivu ukamiminwa ndani yake pamoja na kuwepo na wingi wa watu lakini ujasiri uliongezeka. Haikuwa kazi ndogo kwani iliuma saana lakini hakuwa na lakifanya maana yakitokea ni kukubaliana nayo.
Baada ya mwendo mfupi Paul anajikuta mitaa ya Gedeli anapita vichochoro mpaka anaufikia mto Kenge anatafuta sehemu iliyo jificha anavua nguo zake zote huku zikitoa harufu mbaya na ya ajabu. Paul alianza kufua hukua machozi yakimlengalenga maumivu ya moyo ni ngumu kuyaficha kadiri alivyodhidi kuwaza alijikuta ghafla anaangua kilio na kilikuwa ni kilio kwelikweli kwani aliwaza alivyodhalilishwa hakika ilimuuma sana maana ilimuuma sana kufanyiwa kitendo kile mbele za watu kumwagiwa maji yenye harafu mbaya na isitoshe watu wengi walimfahamu kuwa yeye ni kijana mpole na mtaratibu kabisa sasa kwa tukio hili ni wazi kuwa lilimdhalilisha. Baada ya kumaliza kufua Paul alianika nguo zake na kuketi kivulini akizingoja zikauke na hapo ndipo aliyakumbuka mambo mengi sana kuhusiana na huyo mpenziwe mtarajiwa Johari.
Anaikumbuka siku aliyopelekwa na mama yake shule kwa mara ya kwa mara ya kwanza akiwa kidato cha tano baada ya kuhamia shule ya sekondari ya Mweli shule mashuhuri sana jijini Mwanza. Akitokea shule ya sekondari Kalangalala huko Geita. Paul kwa mara ya kwanza anakutana na malkia huyu ambaye pasipo kutegemea alijikuta anampenda pamoja na kutokulijua hata jina lake lakini nafsi yake inazama na kuzipoteza uelekeo bila shaka alipenda. Moyo wa kijana paul ulikwama kwa msichana huyu murembo ambaye ngozi na nywele zake ziliasiliwa na asili ya mama yake namaanisha asili ya Kiarabu. Alionekana ni msicha murembo mwenye umbo zuri na mwenye mvuto wa ajabu kamwe ungemuona usinge choka kumtizama. Johari alipenda kutabasamu kila wakati kama humfahamu kila ukikutanisha naye macho hakika ungezani anakukonyeza au anakupenda tayari hata kama hujamsemesha na kama ulikuwa umeesha mtongoza basi ungejua tayari amekukubalia.
Siku moja Paul akiwa kaketi pembeni kidogo alijikuta anadata na kuumia roho yake. Anaitizama kuanzia miguu yake yenye ngozi raini na mieupe pee iliyokuwa imavalishwa siketi fupi ya shule iliyoishia juu ya magoti huku ikifuatiwa na soksi nyeupe ndefu kidogo, upande wa nyonga palipanuka na kumfanya aonekane kuwa na mvuto wa ajabu kiukweli msichana huyu aliumbika vilivyo hakuna mwanaume angemuangalia na asiache kumumezea mate. Nyele zake nyeusi tii na ndefu zilizoanguka mabegani na kuukoleza mvuto wake, uso wake mrefu ukipambwa na macho maangavu na makubwa kidogo yenye nyusi na kope nyeusi tii zilizo vutia hazikuhitaji hata kupakwa wanja. Rangi ya ngozi yake iliyoathiriwa vibaya na rangi ya mama yake namaanisha rangi ya kiarabu huku akichanganya na asili ya baba yake ambaye alikuwa ni mhangaza kutoka Ngala, Johari anaonekana mwenye mvuto sana na alimvutia Paul na kumfanya adate kwa kulitamani penzi lake. “Kuna wasichana warembo katika dunia hii kiukweli toka nimezaliwa na kukuwa sikuwahi kumuona kama huyu binti, ila leo ninakili wazi kuwa msichana huyu ni murembo kuliko kawaida.” Hayo ni maneno aliyokuwa akijisemea Paul.
Kutokana na kwamba alimpenda msichana huyu Paul alianza kujenga urafiki kwa Johari ingawa haikuwa rahisi kabisa.
“habari yako dada”
“oooh! Safi ….za kwako” Johari kama kawaida yake aliitikia kwa uchangamfu na kummaliza kabisa Paul”
“ niko Poa dadaaangu”
“Naitwa Paul sijui mwenzangu unaitwa nani?”
“wow! Naitwa Johari Mosse… vipi wewe ni mgeni hapa?”
“ndiyo leo ni siku ya tatu toka nihamie”
“sawa karibu sana” Johari alimkaribisha huku akiondoka .
Paul alijitahidi kujenga ukaribu ambao hata hivyo ulikwama kwani Johari hakuisha vikwazo maana alionekana kujali mambo yake kuliko kumsikiliza Paul, hakuonekana kushitushwa na jinsi Paul alivyoumia kwaajili yake maranyingi alimjibu tu atakavyo na kisha kuondoka zake. Johari aliwajua vizuri vijana na michezo yao michafu ya kuwalaghai wasichana hivyo alikuwa makini na hilo lakini pamoja na hayo bado Paul hakuwa moyoni kwake. Kama tujuavyo mapenzi yanaweza kumuendesha mtu na kumfanya aonekane zuzu hata kama anaakili zake timamu na hivyo ndivyo yalivyomgeuka Paul.
Pamoja na ujasiri wa kumfuata murembo huyu na kumueleza ukweli juu ya mapenzi yake kwake lakini hakukuwa na mabadiliko yoyote kwani hakuwa moyoni kwake. Kunawakati Johari alimjibu vibaya Paul lakini Paul alijikaza na akaiona kama ni hali ya kawaida kwani hakuna kilichomuumiza kwa Johari zaidi ya kulikosa Penzi laki nazani kulikosa penzi lake ndilo lilikuwa tatizo kuliko matatizo yote pia ndili lilikuwa tusi kuliko matusi yote hivi angetukanwa tusi gani ili alione tusi kutoka kwa Johari. Nadhani Paul hakuwa anayajali matusi yote bali aliujali upendo kuliko chochote . Waswahili husema upendo ni kama uyoga huota popote pasipo kuchagua waweza kuota jaani, shambani, juu ya mti na hata chooni.
Kijana huyu kutoka familia masikini anaishi na mama yake akiwa ni mtoto wa peke kwa mama huyua mpika vitumbua. Lakini anajikuta anaangukia kwenye penzi la msichana murembo kutoka familia bora lakini hadhi haikustahili hata kuzigusa nyayo za miguu ya Johari kweli upendo humsukuma mtu kufanya hata asichokitaraji na akijiona yuko sawa. Ni mungu tu ndiye husimama na kusema hapana au twaweza sema ni Mungu tu awezaye kuijua kesho yetu. Kitu kinachoitwa kukata tamaa kwa Paul ulikuwa ni muujiza ambao hauwezekani kutendeka kwani ni kijana anayejiamini sana kwa kila idara hana hofu wala uoga moyoni kwake. Kijana huyu alikuwa na uvumilivu na moyo wa ajabu kwani hakuwa mwepesi wakukata tamaa kabisa, kwa majibu mabaya aliyopewa na matusi aliyoyapokea kutoka kwa Jesca hakika angekuwa ameesha tafuta rafiki mwingine na kuachana na murembo huyu lakini ilikuwa tofauti sana kwa kijana huyu kwani alionekana kuwa na dhamira ya kweli daima aliusikiliza moyo wake unataka nini.
******************
Usiku wa siku hiyo usingizi haukupatikana kabisa kwa Paul anajaribu kulala lakini haikuwa rahisi kwani alijigeuza hukua na kule ni mawazo tu yaliyousulubu moyo wake. Aliwaza kuhusu Johari na chaajabu zaidi aliteseka mno na hata kushindwa kabisa kupata usingizi hakuhangaika na kilichomtokea mchana bali alisimama katika dhamira yake yakweli. Ni upendo aliamini sikumoja Johari atautambua ukweli ulioko ndania ya moyo wake, Siku moja atajua kuwa Paul anamaanisha nini katika maisha yake.
Paul anajaribu kujilaza lakini bado hali haikuwa poa kwake kwani alighubikwa na mawazo ambayo yalikichanganya kabisa kichwa chake. Alimpenda Johari, alimpenda sana na hili ni kovu lisilofutika akilini mwake. Anajaribu kuwaza ni nini kilichotokea mchana aliona ni kosa lake lakini hakupenda kabisa Johari amkasilikie na wala awe na kinyongo juu yake pia kilichomuuma zaidi Johari hajui kukasilika lakini ni yeye ndiye aliyeyasababisha mpaka Johari kuonesha hasra juu yake. Paul alijikuta ananyanyuka usiku huo na kufunga safari ilikuwa yapata saa tano na nusu usiku alianza kuikatisha mitaa bila hofu akijaribu kwenda kuisaka amani ya moyo wake nyumbani kwa akina Johari. Mara anafika nyumbani Kwa akina Johari kijana aligonga mlango mlinzi alifungua akiwa na bunduki yake aina ya AK 47 na wanakutana uso kwa uso na Paul. Je, ni nini kitafuata songa namimi?.
Nicheki kwa namba hii au whatsapp 0768753437