KERO Responded Usagara A, Kata ya Usagara, Wilaya ya Misungwi tumewekewa dampo kwenye makazi ya watu

KERO Responded Usagara A, Kata ya Usagara, Wilaya ya Misungwi tumewekewa dampo kwenye makazi ya watu

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni Mwanakijiji cha Usagara A, Kata ya Usagara, Wilaya ya Misungwi Mkoa wa Mwanza, katika kitongoji changu tumewekewa dampo kwenye makazi ya watu, pia wanachoma taka na kuleta moshi unaosababisha tuvute hewa chafu usiku kucha, huku wananchi tunatozwa pesa kwa ajili ya uzoaji taka, tunaomba serikali ya Kijiji itafute eneo rafiki na si katika makazi ya watu.

Kwa sasa ni kama wiki tatu, lakini hapo kabla waliwahi kuweka ila wanakijiji tukafanikiwa kuliondoa, sasa naona baada ya kuzunguka kote wameona warudishe taka eneo hilo tena, yaani kwa kifupi Kijiji cha Usagara hakuna mahala pa kumwaga taka wakikataliwa huku wanahamia kwingine.
photo_2026-07-06_10-03-55.jpg

Pia soma:
~
RC Mtanda: Suala la dampo katika makazi ya watu Kata ya Usagara, litashughulikiwa na DC na Halmashauri ya Misungwi
~ DC Johari Samizi: Dampo lililokuwa katika makazi ya watu Usagara A, Kata ya Usagara, Wilaya ya Misungwi limeondolewa
 
Back
Top Bottom