Simulizi: Chumba cha Misukule (Sehemu ya 01)

Simulizi: Chumba cha Misukule (Sehemu ya 01)

Sehemu ya 16.

“Mwanzoni nilikuwa nikiambiwa na watu nikahisi labda walikuwa wananidanganya lakini huwezi kuamini siku moja mama mwenye nyumba wangu yeye mwenyewe alikuja kunitamkia kwamba ni mchawi na anafuga misukule ndani kwangu,” nilimwambia, sikuishia hapo tu, nikaendelea kumwambia kila kitu kilichokuwa kikiendelea mpaka kufikia hatua nikawa napewa vitisho kwamba kama ningezitoa siri za ndani humo basi ningegeuzwa kuwa msukule.

“Mungu wangu! Stella kweli upo kwenye matatizo makubwa.”
“Ndiyo hivyo yaani sijui nini nifanye na kuhama siwezi, naogopa kufanywa msukule.”

“Stella mchawi ukimuogopa sana na akijua ndiyo unakuwa umempa nafasi ya kukudhuru hivyo usimuogope.”
“Nisimuogope?”
“Ndiyo halafu mbona dawa yake ni ndogo sana.”

“Dawa yake ni ipi?”
“Maombi tu, naamini tukienda kwa mchungaji Emmanuel atamaliza kila kitu,” aliniambia huku akinifungua akili.
Huyu mchangaji Emmanuel, alikuwa ni mchungaji aliyejizolewa umaarufu mkubwa sana, hasa kwa uhodari wake wa kusaidia watu wengi waliokuwa na matatizo mbalimbali kwa maombi pamoja na mafuta ya upako.

Niliupokea ushauri huo na siku iliyofuata ndiyo siku tuliyopanga twende kanisani kwake kwa ajili ya kufanyiwa maombi.
Ilikuwa hivyo lakini siku hiyo majira ya usiku nilipokuwa nyumbani, nilipokea taarifa mbaya ya kifo cha Glory ambaye alifariki dunia ghafla!

Nilishtuka sana, kwanza sikutaka kuamini hata kidogo. Nilipopokea taarifa hiyo ya msiba haikuchukua sekunde nyingi mara simu yangu ikaanza kuita. Nilipoangalia kwenye kioo mtu aliyekuwa akinipigia kwa wakati huo alikuwa ni mfanyakazi mwenzangu ambaye alikuwa akiitwa, Theresia. Haraka sana nilipokea kisha nikaanza kuzungumza naye.

“Stella una taarifa zozote kuhusu Glory?” aliniuliza.

“Hapana kwani amefanyaje?” nilimuuliza huku nikijitoa ufahamu kwamba sikufahamu lolote lile kwa wakati huo.

“Glory amefariki dunia.”
“Amefariki dunia?”
“Ndiyo, amefariki usiku huu.”
“Sitaki kuamini Theresia kwani uko wapi?”
“Nipo njiani naelekea msibani,” alinijibu.
*
*

Je, nini kiliendelea?
Usikose sehemu ijayo..
 
Sehemu ya 17.

Mpaka kufikia hapo ndipo nilianza kuamini kwamba kweli Glory alifariki dunia. Nilijiuliza maswali mengi sana, nini kilimkuta mpaka kikamtoa uhai wake? Mbona mchana nilishinda naye vizuri na hakuniambia kama alikuwa anaumwa?

Kiukweli nilichanganyikiwa, kila swali ambalo nilijiuliza kwa wakati huo sikuweza kupata majibu.

Wakati nilikiendelea kuwa katika hali hiyo ya sintofahamu mara mlango wa chumba changu nikausikia ukigongwa. Sikutaka kupoteza muda, nikaamka kitandani nilipokuwa nimekaa kisha nikaenda kuufungua mlango. Ile naufungua tu mlango wangu ghafla! macho yangu yakagongana na macho ya mama mwenye nyumba. Nilishtuka!

“Unashtuka nini?” aliniuliza huku akinikazia macho yake yaliyozidi kunitisha. Nilishindwa kumjibu, kutokana na hofu iliyoniingia nikajikuta namsalimia.

“Sina shida na salamu yako,” alinijibu kisha akaendelea kuniambia;
“Kwa nini umekiukia makubaliano yetu?” aliniuliza.

“Makubaliano yapi?”
“Anha! Unajifanya umesahau siyo?”
“Ha…pa…” nilijibu kwa kusita lakini kabla sijamaliza kusema sentensi yangu akanitaka kauli kisha akanikumbusha makubaliano hayo.

“Nilikwambiaje kuhusu siri za humu ndani?”
“Uliniambia kwamba nisizitoe nje wala kumwambia mtu yeyote.”
“Sasa kwa nini umekiuka makubaliano yetu.”
“Nisamehe mama nili...”

“Nikusamehe nini? Hivi uliona Glory ndiyo atakuwa msaada wako, si ndiyo? Haya sasa yuko wapi? Niambie yuko wapi sasa?” aliniuliza kisha akaendelea;
“Nilikwambia hakuna kitu utakachokifanya nisikione, kila kitu unachokifanya nakijua na huwezi kunidanganya, umeona sasa umemponza mwenzako,” aliniambia.
“Nimemponza?”

“Ndiyo, nimemchukua msukule.”
“Mama!” nilimuita kwa mshangao.
“Shiiii! Nyamaza tena nikikusikia unawaambia watu nitakugeuza chakula changu cha usiku halafu nyama yako inaonekana ni tamu sana,” aliniambia huku akinipiga mkwara huo.

Je nini kitaendelea?
 
Sehemu ya 18.

Niliogopa sana, japokuwa aliniambia ukweli kwamba yeye ndiye aliyemuua Glory na kumgeuza msukule sikutaka kuamini hata kidogo, nilihisi labda nipo ndotoni lakini huo ndiyo ulikuwa ukweli wenyewe niliotakiwa kukubaliana nao.

Hapa ningependa niwaambie kitu kimoja, jamani hizi nyumba za kupanga zioneni tu hivi hivi kwa macho ya nje lakini usiombe siku moja upange kwenye nyumba kama niliyopanga mimi, utatamani ardhi ipasuke uingie.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa upande wangu, kuna wakati nilitamani kukimbia nyumba, yaani niache kila kitu changu ndani huku nikiamini kwa kufanya hivyo ningeweza kuyaepuka matatizo lakini ilikuwa ni sawa na bure. Kila mpango niliyoupanga mama mwenye nyumba wangu aliufahamu.
Kiukweli nilishindwa kuhama katika nyumba hiyo kutokana na vitisho nilivyokuwa nikipewa kila siku.

Mwanzoni nilichukulia kama ni mikwara ambayo asingeweza kuifanyia kazi lakini kadri siku zilivyokuwa zikisonga mbele na jinsi alivyokuwa akiwachukua watu misukule ndivyo nilivyozidi kumuogopa mno.
***

Kifo cha Glory kilimgusa kila mtu, katika kipindi hicho hakukuwa kuna mtu aliyetaka kuamini kama msichana huyo alikuwa amefariki dunia. Watu mbalimbali walikusanyika nyumbani kwao kuomboleza msiba huo.
Japokuwa nami nilikuwa mmoja wao lakini nilijua kila kitu kilichokuwa kikiendelea kwa wakati huo.

Nilijua fika kuwa Glory hakufa kama watu walivyokuwa wakiamini isipokuwa alichukuliwa kichawi na mama mwenye nyumba wangu ambaye alimfanya msukule.
Hata hivyo sikuweza kuwaambia ukweli huo, nilibaki na siri hiyo nzito moyoni mwangu huku kila siku ikiwa inanitesa katika maisha yangu.

Baada ya kupita siku kadhaa hatimaye Glory aliweza kuzikwa kwa heshima zote kama sisi wakristo tunavyofanya.

Je nini kitaendelea?
 
Sehemu ya 19.

Hapa ningependa nikwambie kitu ambacho nahisi hukifahamu, watu waliamini kwamba walimzika Glory lakini ukweli ni kwamba hawakumzika yeye na badala yake walizika kipande cha mgomba bila hilo kujua.
Hivyo ndivyo wachawi wanavyofanya, sijui ni mbinu gani huwa wanaitumia lakini huwa ni ngumu mno kuweza kufahamu hilo wala kuona kwa macho ya kawaida labda uwe na uwezo wa ziada.

Katika kipindi hicho niliona kila kitu kilichokuwa kikiendelea na yote hayo mama mwenye nyumba wangu ndiye aliyeamua kunionyesha kama kuendelea kunitisha ili nisiseme ukweli.

Baada ya mazishi kumalizika maisha yaliendelea kama kawaida. Nakumbuka zilipita siku kama tatu hivi, siku iliyofuata majira ya jioni niliporudi nyumbani kutoka kazini, ile nafungua mlango tu wa chumba changu ghafla! nikapokelewa na sauti ya mtu aliyeniita kutokea ndani humo, sauti hiyo niliifahamu, ilikuwa ni sauti ya Glory.
Kiukweli niliogopa sana, nilishindwa hata kuingia ndani. Nilichokifanya nikakimbilia kwa mama mwenye nyumba wangu huku hofu ikiwa imenijaa.
*
*

Je, nini kitaendelea?
 
Sehemu ya 20.

“Kuna nini?” aliniuliza huku akinishangaa.
“Nimesikia sauti kama ya Glory ikiniita kule ndani kwangu,” nilimjibu.

“Sasa hicho ndicho kilichokufanya ukimbie kiasi hicho, mimi nilifikiri labda kuna tatizo kubwa kumbe ni hilo. Ina maana umesahau kwamba unaishi na misukule yangu kule ndani kwako?” aliniambia kisha akaniuliza swali hilo.

“Najua mama laki…”
“Lakini nini?”
“Mama mimi siwezi kuishi na misukule ndani, naogopa.”

“Unafikiri ukiogopa kuishi na misukule yangu utaenda kuishi wapi kwingine?”
“Niruhusu nihame.”

“Hilo ni jambo lisilowezekana, yaani ni sawa sawa na kuuza nguruwe msikitini lazima utapata hasara tu,” aliniambia kisha akaendelea;

“Halafu mimi nakushangaa sana, unaogopa kuishi na misukule ndani kwani inang’ata au umesikia labda ukiishi nayo itakunyonya damu na kukubakisha mifupa mitupu?”
Kwa jinsi alivyokuwa akiniambia na kuniuliza maswali kwa wakati huo ni kama vile kitendo hicho cha kuishi na misukule ndani kilikuwa ni cha kawaida kabisa, yaani mfano wake ni kama vile kila mtu alikuwa akiishi nayo nyumbani kwake na hivyo sikutakiwa kuogopa hata kidogo.

Hilo kwangu lilikuwa ni jambo gumu mno, japokuwa alinitoa wasiwasi lakini moyoni mwangu bado sikuwa tayari kuendelea kuishi katika nyumba hiyo na misukule. Nilitamani nihame japokuwa hilo lilikuwa ni jambo lisilowezekana kutokana na kauli za vitisho alivyokuwa akinipa.

Je nini kitaendelea?
 
Sehemu ya 21.

“Kule ndani hayupo Glory peke yake, wapo watu wengi sana akiwemo mume wangu pamoja na mwanangu, Siwema nao pia niliwageuza misukule.”

Aliponiambia hivyo nikazidi kupigwa na butwaa! Maneno hayo yalinitisha vibaya mno, hofu isiyokuwa na kifani ikanitawala. Wakati mwingine sikutaka kuamini.

“Hapa bado wewe tu ndiye unayenichelewesha, kama umechoka kuendelea kuishi humu ndani niambie mapema usinipotezee muda wangu nina ratiba ya watu wengi sana ambao nataka kuwachukua na kuwafanya misukule ili wakanisaidie kazi zangu huko mashambani,” aliniambia.

Kiukweli hakukuwa kuna kitu ambacho nilikiogopa sana katika maisha yangu kama kurogwa.

Nilipoulizwa kwamba kama nilichoka kuishi katika nyumba hiyo niseme haraka ili nigeuzwe msukule, nilishindwa kuchukua maamuzi.

Ilibidi nikubali kuendelea kuishi ilihali niliogopa mno. Asikwambie mtu kuishi chumba kimoja na misukule inataka moyo sana.

Katika kipindi hicho sikuwa na jinsi ya kufanya, hata kama niliogopa kuishi na misukule lakini ilinilazimu nikubali kuishi nayo hivyo hivyo ilimradi niendelee kuulinda usalama wa maisha yangu.
Hivyo ndivyo ilivyokuwa, niliendelea kuishi huku kila siku nikitokewa na mauzauza.

Nakumbuka kuna siku nilipokuwa ndani ya chumba changu nilihisi kama kuna mtu amenishika mkono na kuanza kunivuta.
Nilipiga kelele ya kuomba msaada ndipo hapo mama mwenye nyumba wangu haraka sana akaja.

Mtu huyo niliyehisi amenishika mkono kwa wakati huo akaniachia, nikadondoka chini kama mzigo.

“Wewe Stella una nini lakini?” aliniuliza.
“Kuna mtu alikuwa ananivuta mkono,” nilimjibu kisha nikaamka hapo chini.
“Una uhakika?”

“Ndiyo.”
“Hebu subiri,” aliniambia kisha akatoka nje, sikujua alifuata nini mpaka pale aliporudi. Nikamwona mkononi akiwa ameshika kibakuli kilichokuwa ndani na kitu kama vile unga.

Je nini kitaendelea?
 
Sehemu ya 22.

Hakunisemesha kitu muda huo, alichokifanya akaanza kuunyunyiza ule unga uliokuwepo kwenye bakuli mule ndani kila kona.

Nilibaki kimya huku nikimtazama kwa hofu kubwa mno moyoni mwangu, kitendo hicho kilimchukua dakika kama tano hivi mpaka kumaliza.

Alipomaliza ndipo hapo akaniambia kwamba nisiogope, mtu huyo aliyenishika mkono na kuanza kunivuta alikuwa ni msukule wake na hivyo asingeweza kurudia tena kufanya kitendo hicho kwa sababu alikwishamdhibiti na ile dawa ambayo aliinyunyiza mule ndani.
Niliogopa sana lakini kama unavyojua sikuwa na jinsi ya kufanya, ilibidi nivumilie kila kitu kilichokuwa kikinitokea. Nilichokuwa nikikiogopa zaidi ni kugeuzwa msukule.

Siku hiyo ilipita na mauzauza yake, siku iliyofuata wakati nilipokuwa nikielekea kazini majira ya asubuhi ndipo hapo barabarani nilikutana tena na yule mama ambaye mwanzoni niliwahi kukutana naye na ndiye alikuwa mtu wa kwanza kuniambia habari za mama mwenye nyumba wangu kwamba alikuwa ni mchawi mpaka akafikia hatua ya kuniambia nilitakiwa nihame katika nyumba hiyo haraka sana na kama nisingehama basi nilichokuwa nikikitafuta ningekipata.

“Mrembo wangu unanikumbuka?” aliniuliza huku akitabasamu.
“Ndiyo nakukumbuka, shikamoo,” nilimjibu kisha nikamsalimia.

“Marahaba, unaendeleaje lakini?” aliniuliza.
“Naendelea vizuri, namshukuru Mungu, sijui wewe?” nilimwambia.

“Namshukuru Mungu pia ila unaonekana haupo sawa?” aliniuliza huku akinitazama kwa umakini.

“Kwa nini? Mbona nipo sawa.”
“Sura yako inaonyesha.”
“Hapana nipo sawa.”
“Sio kweli, halafu kwa nini hutaka kunisikiliza siku ile?”
“Kivipi?”

“Nilikwambia uhame mapema katika ile nyumba lakini nashangaa kuona mpaka sasa bado unaendelea kuishi.”
“Hapana sio kama siku…” nilimwambia lakini kabla sijamaliza kusema sentensi yangu akanikata kauli.
*
*

Je nini kitaendelea?
 
Sehemu ya 23.

“Usijali najua kila kitu kinachoendelea ila umefanya makosa makubwa sana ya kutonisikiliza laiti kama ungefuata ule ushauri wangu niliokupa sidhani kama leo hii ungeishi maisha haya,” aliniambia huku akinilaumu kutokana na uzembe huo nilioufanya.

Kitu kilichonishangaza zaidi ni kwa jinsi mama huyo alivyokuwa akifahamu kila kitu kilichokuwa kikiendelea katika maisha yangu.

Ukumbuke mpaka kufikia hapo nilikuwa bado simfahamu. Ilibidi nimuulize na ndipo hapo akajitambulisha kwa jina, akaniambia kwamba alikuwa anaitwa Mama Nyamisi ama kama ningependa basi nimuite mama wawili kwa sababu hilo ndiyo jina maarufu ambalo wengi walizoea kumuita.

“Mimi naitwa Stella,” nilijitambulisha.
“Nashukuru kukufahamu Stella ila jua upo katika vita vikubwa mno na kawaida ya vita siku zote kuna kushindwa na kushinda hapa lazima ukubaliane na moja wapo,” aliniambia maneno ambayo yalikuwa na fumbo zito, nilishindwa kulifumbua.

Sijui alikuwa na maana gani hata hivyo hakutaka kunichelewesha, akaniambia niwahi kazini lakini nikae nikielewa kwamba nilikuwa katika vita vikubwa na katika vita hivyo nilitakiwa kuchagua jambo moja, yaani nichague kati ya kushinda ama kushindwa.
***

Kiukweli maneno ya mama Nyamisi yalizidi kunichanganya vibaya mno, kila nilipokuwa nikifikiria namna ambavyo nilitakiwa kupigana vita hivyo alivyoniambia sikujua ni njia gani ambayo nilitakiwa kuitumia.

Labda nikwambie tu, katika kipindi hicho nilipanga kwenda kwa mchungaji kimya kimya ili aniombee niweze kuondokana na matatizo niliokuwa nayo, ikiwezekana anitoe katika kifungo cha maisha niliokuwa nikiishi.

Je nini kitaendelea?
 
Sehemu ya 24.

Katika hilo sikutaka kumshirikisha mtu yeyote kwa kuhofia yale ambayo yalimtokea Glory.
Siku zilikatika, siku ya jumapili ilipowadia nikaondoka zangu vizuri kuelekea katika kanisa la Praise na Worship lililokuwepo maeneo ya Mwenge.

Siku hiyo nakumbuka nilipanda daladala vizuri mpaka kufika Mwenge, kitu cha kushangaza baada ya kufika na kutaka kwenda katika kanisa hilo sikuliona.

Nilishangaa sana, nikahisi labda nimesahau mahali lilipokuwepo kwa sababu sikuja muda mrefu, ni hapa ambapo nilimsimamisha jamaa mmoja ambaye baada ya kumsalimia nilimuuliza;
“Samahani kaka nilikuwa naulizia kanisa la Praise and Worship nimesahau sijui lipo maeneo gani kwa hapa?”
“Kanisa la Praise and Worship?” aliniuliza huku akinishangaa.

“Ndiyo, lipo wapi?” nilimjibu kisha nikamuuliza.
“Mbona hapa Mwenge hakuna kanisa kabisa,” alinijibu.

“Hakuna kanisa?”
“Ndiyo hakuna kanisa hata moja sasa nashangaa unaponiuliza hilo kanisa la Praise and Worship sijui umelionea wapi?”
“Kivipi?”
“Kwani dada wewe umeulizia nini?”
“Kanisa.”

“Nimekwambia halipo,” aliniambia jamaa huyo kisha akaamua kuondoka zake.
Sikutaka kuamini, nilihisi labda jamaa huyo alikuwa ni mgeni na eneo hilo, nilichokifanya nikatafuta mtu mwingine wa kumuuliza, huyu alikuwa ni mwanamke mtu mzima kidogo.
“Shikamoo,” nilimsalimia.

“Marahaba hujambo,” aliiitika.
“Sijambo, samahani.”
“Bila samahani.”
“Nilikuwa naulizia kanisa la Praise and Worship sijui lipo maeneo gani kwa hapa Mwenge maana nimesahau.”

“Umesema kanisa gani?”
“La Praise and Worship.”
“Mbona hilo kanisa sijawahi kuliona.”
“Hujawahi kuliona?”
“Ndiyo.”

“Je, hakuna kanisa lingine unielekeze?”
“Kwa kweli kwa hapa Dar hakuna kanisa lolote nitakudanganya, kote utakapoenda utasumbuka bure,” alinijibu mwanamke huyo, nikazidi kupigwa na butwaa.

Je nini kitaendelea?
 
Sehemu ya 25.

Mpaka kufikia hapo nafikiri unaweza ukaona ni kwa jinsi gani nilipagawa. Yaani kwa jinsi Dar es salaam ilivyo eti uambiwe kwamba hakukuwa kuna kanisa hata moja, nadhani hata wewe ungestaajabu kama mimi nilivyostaajabu muda huo.

Hapa ningependa niseme kitu kimoja, pengine kwa hiki ninachokisimulia kwa wakati huu kuna baadhi ya watu watahisi labda hii ni simulizi ya kufikirika kama walizozoea kuzisoma lakini niseme kuwa hii sio simulizi ya kufikirika bali ni simulizi ya kweli ya maisha yangu iliyowahi kunitokea.

Nimeamua kusimulia kila kitu ili kila mtu ajue kuwa uchawi upo na kuna vitu vingi sana vya ajabu vinavyoendelea katika huu ulimwengu ambavyo kama ukisimuliwa huwezi kuamini.

Muda huo sikutaka kuamini hata kidogo, japokuwa niliambiwa kwamba hakukuwa kuna kanisa lingine mahali hapo, nilichokifanya niliondoka nikaelekea Magomeni, Kanisani.

Nilipofika sikutaka kuamini kile nilichokiona. Kama ilivyokuwa Mwenge huko napo sikuona kanisa jambo ambalo lilizidi kunishangaza vibaya mno.
*

Je, nini kitaendelea?
Tukutane kesho kwenye muendelezo...
 
Shunie
Wana jamii forum indirectly wanapenda wakusumbue sumbue ukiwa na simulizi au kisa, in case ukitaka popularity kwenye Thread fanya hivyo tuma vipande vipande pale utakapojiskia na sio kwa mpigo hivi ikibidi after every single day ndio utume

Vile vile kwa upande mwingine kuleta ndefu hivyo inapunguza ule uraibu wa usomaji
@moneytalk njoo unijibie hapa maana nimekosa cha kujibu kila nikitaka kujibu naandika nafuta
 
Mkuu sio story zangu za kwanza hizi kuleta jf nahisi we umefatilia hizi ukitaka soma ukitaka acha waache wanaofatilia waendelee kusoma halafu usiniquote ujinga ujinga
am sorry mimi sikujua hilo.
 
Natamani haya mauza uza yangemkumba marehemu màgufool kipindi cha mwisho mwisho cha uhai wake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom