Simulizi: Chumba cha Misukule (Sehemu ya 01)

Sehemu ya 26.

“Jamani hapa si kulikuwa kuna kanisa mbona sasa silioni?” nilijiuliza peke yangu huku nisiamini kama kweli mahali hapo hakukuwa kuna kanisa. Nilichokuwa nikikiona kwa wakati huo ulikuwa ni uwanja mkubwa uliotawaliwa na nyasi nyingi.

Nilihisi kupagawa zaidi, hebu fikiria tu kwa akili ya kawaida unapanda daladala vizuri halafu unamwambia konda akushushe Magomeni kanisani, anafanya hivyo lakini unaposhuka kituoni hapo huoni kanisa. Ungefanyaje?

Kama ni kuchanganyikiwa basi siku hiyo nilichanganyikiwa haswa, kuna wakati sikutaka kuamini mauzauza hayo yaliokuwa yakinitokea.

“Habari yako anko,” nilimsalimia kijana mmoja niliyekutana naye kituoni hapo.
“Poa tu sister sijui wewe?” aliitikia salamu yangu kisha akanijulia hali.
“Nzuri samahani eti hapa ni Magomeni kanisani?” nilimuuliza ili nihakikishe kwamba sikupotea ama la.

“Ndiyo,” alinijibu.
“Hivi hilo kanisa lenyewe liko wapi?” nilimuuliza.
“Aah! Sister acha kunichora basi ina maana unataka kuniambia kanisa hulioni au?”
“Sasa anko kama ningeliona ningekuuliza kweli?”

“Kanisa si lile pale,” aliniambia huku akinionyesha kwa kidole cha shahada.
Japokuwa alinionyesha mahali lilipokuwepo kanisa hilo lakini sikuweza kuona kitu. Nilichokiona ulikuwa ni ule uwanja uliojaa nyasi.

Hapa ngoja nikwambie kitu, mimi sikuwa mgeni na jiji la Dar es salaam, hapo ambapo alikuwa akinionyesha kweli ndipo mahali ambapo hata mimi mwenyewe nilikuwa nafahamu kwamba kanisa hilo lipo hapo lakini kitu cha kushangaza muda huo sikuweza kuliona. Unaweza kufikiri labda ni utani lakini huo ndiyo ulikuwa ukweli.
“Umeliona?” aliniuliza.

“Ndiyo ahsante sana anko,” nilimjibu huku nikimshukuru kwa kumridhisha japokuwa ukweli ni kwamba sikuliona kanisa.
Kiukweli nilishindwa kuvumilia mauzauza hayo yaliyokuwa yakiendelea kunitokea.

Baada ya kuona mauzauza yamezidi kushamiri ndipo hapo niliamua kuvuka upande wa pili wa barabara, nikapanda daladala za kuelekea Sinza ambapo nilirudi nyumbani huku kichwani mwangu nikiwa nimetawaliwa na maswali mengi ambayo yalikosa mtu wa kunijibu kwa wakati huo.

Ile nafika tu nyumbani kwanza nilipokelewa na mama mwenye nyumba ambaye nilimkuta akiwa amekasirika mno. Naweza kusema siku hiyo ilikuwa ni tofauti na siku nyingine nilizowahi kumwona akiwa amekasirika.

“Stella naona sasa unataka kunijaribu, unanipima imani yangu,” aliniambia huku akiwa amekasirika. Sura yake ilimkakamaa na macho yake pia aliyakaza.

“Kwa nini mama?” nilimuuliza.
“Kule kanisani ulitaka kwenda kufanya nini?”
“Lakini mama kwani kuna ubaya gani mimi kwenda kanisani?”
“Unajifanya hujui? Unataka kuniangamiza?”
“Hapana mimi si…”

“Sasa nisikilize kwa umakini, kuanzia leo sitaki kukuona ukienda tena kanisani. Nilijua lengo lako na ndiyo sababu nikakufanyia vile ulivyoviona kule,” aliniambia kisha akaendelea.
“Kama umechoka kuishi humu ndani niambie.”

Siku hiyo alinipa vitisho vile vile kama alivyozoea kunipa kila siku na kunitishia kunigeuza msukule, aliona kuniambia hivyo kama haitoshi, alichokifanya akaamua kufanya kwa vitendo.

Sijui alifanya nini muda huo lakini nilishangaa nikianza kuhisi kizunguzungu, haikuchukua sekunde nyingi mara ghafla! nikadondoka chini kama mzigo na kisha hapohapo nikakumbwa na usingizi mzito, sikujua ni kitu gani kilichoendelea tena mahali hapo.
***
Nilipata fahamu majira ya usiku, muda huo nilikuwa makaburini peke yangu huku nikiwa sina nguo hata moja.
Nilikuwa uchi wa mnyama na nilisimama mbele ya kaburi moja ambalo sikuweza kujua lilikuwa ni la nani.

Hofu kubwa mno ilinitawala moyoni mwangu na nilipokuwa nikiyakwepesha macho yangu yasiendelee kulitazama kaburi hilo ndipo hapo nyuma niliposhangaa kumuona mama mwenye nyumba wangu akiwa amevalia vazi la kaniki huku usoni akiwa amejichora michoro ya ajabu kwa kutumia kitu kama vile chokaa.

Nilishtuka sana kumuona mahali hapo, nikatamani kukimbia lakini kitu cha kushangaza miguu yangu ilikuwa mizito na kila nilipojaribu kukimbia, nilishindwa.
Hapo ndipo mama mwenye nyumba wangu akaanza kucheka kwa sauti kubwa. Sauti yake ilikuwa ikijirudia masikioni mwangu kama vile sauti ya mwang’wi.

“Stella unataka kukimbilia wapi?” aliniuliza huku akiendelea kucheka kwa sauti kubwa iliyokuwa ikijirudia mara mbilimbili masuikioni mwangu.
Niliogopa sana, kwa hofu kubwa niliokuwa nayo nilimjibu.

“Nyumbani.”
“Hahaha! Stella kwa sasa huwezi kurudi tena nyumbani.”
“Kwa nini?”
“Wewe tayari umeshakufa na hili kaburi unaloliona hapa ni lako, watu wanajua umeshakufa,” aliponiambia hivyo nilishangaa mno.

“Nimekufa?” nilimuuliza.
“Ndiyo umeshakufa,” alinijibu huku akicheka kama kawaida yake.
“Kivipi nimekufa?” nilimuuliza tena.
“Kwani watu wanaokufa wanakufaje?”
“Haiwezekani mimi sijafa.”

“Stella wewe umeshakufa na kuanzia sasa utakuwa msukule wangu,” aliponiambia hivyo akanishika mkono.
Sikutaka kuamini hata kidogo, ndipo hapo nikaanza kupiga kelele za kuomba msaada.
***

Nilikuja kupata fahamu nikajikuta nipo nje na mama mwenye nyumba wangu. Muda huo nilikuwa nimelala chini pale nilipoangukia. Nilishangaa sana.
“Nini kimetokea?” nilimuuliza kwa kukurupuka, badala ya kunijibu nikamuona akitabasamu.

“Stella nadhani umeona kila kitu?” aliniambia huku akiniuliza.
“Kitu gani?” nilimuuliza.
“Kule makaburini nilipokupeleka.”
Aliponijibu hivyo nilizidi kuogopa.
“Sasa nakupa onyo la mwisho, nikikuona unaenda tena kanisani ama unajaribu kutoroka humu ndani kile ulichokiona kule makaburini ndicho kitakachokutokea,” aliniambia kisha akaondoka kuelekea ndani kwake.

Kiukweli hapa duniani hakuna kitu kigumu sana kama kuishi na mchawi, kila kitu unachokifanya lazima akijue. Yaani hata upange kufanya siri kiasi gani lazima ajue tu na ugumu huo ndiyo nilikuwa nikiupitia mimi katika kipindi hicho.

Unaweza ukahisi labda nilikuwa sina wazo la kutoroka katika nyumba hiyo ama labda nilikuwa sifikirii kwenda kutafuta msaada mahali fulani lahasha vyote hivyo nilikuwa nikiviwaza kichwani mwangu lakini tatizo lilikuja pale ambapo kila kitu nilichokuwa nikikipanga kufanya mama mwenye nyumba wangu alijua na nilikuwa nikijihatarishia usalama wangu.

***
Niliendelea kuishi katika nyumba hiyo huku kila siku nikiendelea kumuogopa mama mwenye nyumba wangu kama mbogo.
Siku ziliendelea kukatika, baada ya kupita kipindi fulani ndipo hapo siku moja akaniuliza kama nilikuwa nina matatizo yoyote kiafya kwa sababu alikuwa hanielewi. Nilikuwa tofauti na wasichana wengine.
“Kwa nini umeniuliza hivyo?” nilimuuliza.

“Unajua tangu ulipohamia hapa sijawahi kukuona ukiingia na mwanaume yeyote humu ndani sasa ndiyo najiuliza labda una matatizo kwenye kizazi au pengine umeukwaa gonjwa hili hatari la Ukimwi?”
“Hapana mama, sina tatizo lolote.”

“Sasa kama huna tatizo lolote nini shida inayokufanya usiwe na mwanaume?”
“Nafikiri kila kitu ni maamuzi, kwa sasa sijafikiria kuingia katika mahusiano na mwanaume.”

“Kwa nini?”
“Nimeamua tu.”
“Ina maana unataka kuniambia huna hisia kabisa?”
“Ninazo.”
“Sasa kama unazo kwa nini hutaki kuwa na mwanaume?”
“Muda ukifika nitakuwa naye tu.”

“Mpaka lini?”
“Mpaka pale nitakapompata.”
“Sawa,” aliniambia huku akionyesha kukubaliana na jibu langu hilo. Siku hiyo ilipita.

Siku iliyofuata majira ya asubuhi nilipoamka tu nilishangaa kujiona sipo sawa mwilini mwangu.

Kwanza nilijikuta sina nguo hata moja wakati usiku wa kuamkia siku hiyo nakumbuka nililala na nguo, ukiachana na hilo, nilipojiangalia sehemu zangu za siri nilijiona kuwa tofauti, niliona kitu kama uteute hivi jambo lililozidi kunishangaza mno.
“Mungu wangu ina maana nimebakwa?” nilijiuliza huku nisijue ni nani ambaye aliamua kunifanyia ukatili huo.

Nilipouangalia mlango wa chumba changu kwa kuhofia labda ulikuwa umevunjwa kwa wakati huo niliukuta ukiwa vilevile kama nilivyoufunga.

“Sasa kama ni mtu amenivamia na kuamua kunibaka ameingilia wapi?” nilijiuliza swali ambalo nilikosa majibu kiukweli.
Nilichanganyikiwa vibaya mno, hofu yangu muda huo ilikuwa ni kwa misukule niliokuwa nikiishi nayo ndani humo.

“Ina maana nimebakwa na misukule?”
“Kweli?”
“Itawezekana vipi?”
“Mungu wangu!”
Kichwani mwangu niliendelea kujiuliza maswali lukuki ambayo yalikosa mtu wa kunijibu kwa wakati huo.

Sijui niseme nini ili ujue ni kwa jinsi gani nilichanganyikiwa. Naweza kusema hakuna siku niliyowahi kuchanganyikiwa katika maisha yangu kama siku hiyo.

Kitendo cha kuamka asubuhi na kukuta nimebakwa hakika kilinivuruga akili yangu kupita kawaida.

Je nini kiliendelea?
 
Sehemu ya 27.

Hapa sio mimi tu, naamini kwa asilimia zote mia moja hata kama ungekuwa ni wewe ndugu msomaji lazima ungechanganyikiwa.
Kwa vyovyote vile niliamini kama sio mama mwenye nyumba wangu alihusika katika hilo basi alifahamu kila kitu kilichokuwa
kimetokea kwa sababu katika mazingira ya kawaida ni jambo lisilowezekana hata kidogo.

Hebu fikiria umefunga mlango wa chumba chako vizuri halafu anakuja mtu kukubaka usiku, asivunje mlango wala kuonyesha dalili zozote kwamba alipitia dirishani. Ungewaza nini kama sio uchawi?

Nilichokifanya niliamka kitandani hapo nikavaa nguo zangu kisha nikatoka kuelekea kwa mama mwenye nyumba wangu, muda huo hasira zilikuwa zimenipanda kwa sababu kitendo nilichokuwa nimefanyiwa hakikuwa kizuri.

“Stella kulikoni mbona asubuhi asubuhi yote hii?” aliniuliza, nilimkuta akiwa anafagia.
“Mama unaweza kuniambia ni nani aliyenibaka?”

“Mwanangu hiyo ndiyo salamu kweli au ndivyo ulivyofundishwa huko nyumbani kwenu kutowasalimia wakubwa zako?” aliniuliza lakini kutokana na hasira nilizokuwa nazo sikutaka kumsalimia, nilichokifanya nikarudia kumuuliza tena kwa mara ya pili aniambie ukweli ni nani aliyenibaka.

Hapo ndipo nilipomkwaza zaidi.
“Stella hivi umechanganyikiwa? Ina maana unataka kuniambia kwamba mimi ndiye niliyekubaka? Mbona unanivunjia heshima wewe mtoto?”

“Sijasema kwamba wewe ndiye uliyenibaka ila utakuwa unafahamu kila kitu.”
“Mimi nafahamu kila kitu?”
“Ndiyo kwa sababu haiwezekani.”
“Kivipi?”

“Mama usijitoe ufahamu, najua unajua kila kitu kwa sababu mazingira niliobakwa ni ya ajabu na humu ndani tunaishi wawili tu.”
Nilipomwambia hivyo alinyamaza kwa muda kidogo, nikamwona kama vile kuna jambo fulani ambalo alikuwa akilitafari na baada ya kumaliza ndipo hapo aliniambia;

“Stella mwanangu mimi siwezi kukufanyia kitu kama hicho, kwanza nawezaje kukubaka wakati mimi ni mwanamke mwenzio?”

aliniuliza sauti ya upole swali hilo ambalo lilikuwa na mantiki kubwa sana lakini kwa sababu alikuwa mchawi niliamini yote hayo yanawezekana. Mchawi ni mchawi tu siku zote, anaweza kufanya kitu kisichowezekana kikawezekana.

“Mimi sijui kama ni wewe ama ni nani anayehusika, nataka kujua,” nilimwambia maneno yaliyozidi kumkwaza.

“Unataka kujua ukweli?” aliniuliza.
“Ndiyo,” nilimjibu.
“Sawa aliyekubaka ni msukule.”

“Msukule?”
“Ndiyo umefanya naye mapenzi usiku kucha bila wewe kujua,” aliniambia, nilipigwa na butwaa.

Sikutaka kuamini hata kidogo, japokuwa nilitaka kuujua ukweli kwa wakati huo lakini baada ya kuambiwa kwamba nilifanya mapenzi na msukule usiku kucha kiukweli hilo liliniogopesha sana na kunifanya niingiwe na simanzi nzito moyoni mwangu.
“Nimefanya mapenzi na msukule?”

“Ndiyo sasa unaogopa nini, si ulitaka kuujua ukweli?” aliniambia huku akiniuliza swali hilo kana kwamba lilikuwa ni jambo la kawaida kufanya mapenzi na msukule.

Moyo wangu ulilipuka kwa maumivu makali na kila nilipokuwa nikiifikiria kauli hiyo nilihisi kuchanganyikiwa.

Hapa najua kuna watu wanaweza wakajiuliza msukule uliweza vipi kufanya mapenzi na mimi? Swali hili ndilo ambalo hata mimi muda huo nilijiuliza bila kupata jibu.

Hakika lilikuwa ni jambo la kushangaza sana, wakati mwingine nilitamani iwe ni ndoto kama zilivyokuwa ndoto nyingine lakini huo ndiyo ulikuwa ukweli wenyewe. Nilifanyishwa mapenzi na msukule bila kujijua.

Labda nikwambie tu, huo haukuwa ni mwisho wangu wa kufanyishwa mapenzi na msukule bali ndiyo ulikuwa mwanzo.
Kila siku nilipokuwa nikiamka asubuhi na kujiangalia sehemu zangu za siri nilikuta tayari nimeshaingiliwa kimwili bila kujijua. Ukiachana na hilo pia nilihisi uchovu wa mwili usiokuwa wa kawaida.

Kiukweli niliumia sana, kuna wakati nilitamani kwenda polisi kushtaki kutokana na ukatili niliokuwa nafanyiwa na mama mwenye nyumba wangu lakini sikujua ningeanzia wapi?

Kwanza hivi kuna kesi gani ya ubakaji inaweza ikafunguliwa mahakamani kwa madai kwamba nimebakwa na msukule?
Hilo ni jambo lisilowezekana hata kidogo na hiyo ndiyo sababu ambayo naweza kusema ilinifanya nisifikirie kwenda polisi kwa wakati huo.
***
Siku ziliendelea kukatika, katika kipindi hicho sikujua kama nilibeba ujauzito mpaka pale ambapo nilianza kuhisi dalili, nilipoenda hospitalini kupima ndipo hapo majibu yalionyesha kwamba kweli nilikuwa nina ujauzito.

Mpaka kufikia hapo ilimaanisha kuwa nilibeba ujauzito wa msukule. Huo ndiyo ulikuwa ukweli ambao sikutaka kukubaliana nao kabisa.

“Hapana dokta haiwezekani,” nilimwambia daktari wakati akinipa majibu hayo.
“Haiwezekani kivipi na wakati vipimo vinaonyesha kwamba una ujauzito tena wa mwezi mmoja na nusu,” aliniambia daktari huku akiendelea kunisisitiza ukweli wa majibu ya vipimo.

“Ina maana nimebeba mimba ya msukule?” niliropoka.

“Mimba ya msukule? Kivipi? Una maanisha nini?” aliniuliza maswali matatu kwa mpigo, muda huo hata yeye mwenyewe alishangaa.
“Aa..ah..hakuna kitu,” nilimjibu kwa kigugumizi huku nikipotezea mada muda huo, sikutaka kumwambia kitu kilichokuwa kikiendelea lakini kwa kufanya hivyo moja kwa moja ilipelekea ahisi kuna kitu nilichokuwa nikimficha ambacho ndicho kilichokuwa kikiendelea nyuma ya pazia.

“Nimekusikia lakini ukisema kwamba umebeba mimba ya msukule?” aliniuliza huku akionekana kutoamini hicho alichokisikia.

“Ni kweli dokta huu ujauzito ni wa msukule,” nilimjibu, jibu hilo lilizidi kumchanganya sana.

“Kivipi? inawezekanaje binadamu akazaa na msukule?”

“Dokta najua huwezi kunielewa lakini wewe fahamu hivyo kuwa nimebeba ujauzito wa msukule,” nilimjibu.

Japokuwa nilimwambia ukweli daktari huyo lakini kile nilichomweleza kwa wakati huo alikiona kuwa kama maigizo.

Hakutaka kuamini hata kidogo, hata hivyo sikuwa na muda wa kumwelewesha zaidi na zaidi, nilichokifanya niliondoka zangu kuelekea nyumbani huku kichwa changu kikiwa kimetawaliwa na mawazo lukuki.
***

Kwa mambo yote hayo yaliyokuwa yakiendelea kunitokea katika maisha yangu najua unaweza ukahisi kwamba labda nilifukuzwa nyumbani kwetu ama sikuwa na ndugu yeyote hapa mjini na hiyo ndiyo sababu ambayo ilinifanya nishindwe kwenda kuomba msaada.

Haikuwa hivyo, ndugu nilikuwa nao na hata wazazi wangu pia walikuwepo ila sijui ni nini kilitokea, katika kipindi hicho sikukumbuka kama nilikuwa nina ndugu, hata wazo la kuwapigia simu kiukweli sikuwa nalo kichwani mwangu, ajabu sasa hata wao pia hawakunikumbuka jambo lililonifanya nizidi kusahau kama nilikuwa nina ndugu.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa, naweza kusema nilirogwa kwa sababu kwa akili ya haraka haraka ni jambo lisilowezekana mtu kusahau nyumbani kwao ama ndugu zake.

Je nini kiliendelea?
Tukutane kesho.....
 
Kesho sasa.....!

Asanteh Shunie
 
Bibiee shunie,
Poleeee sana kwa mfumo wa maisha ulioupitia.
Nashauku ya kutambua ukomo wa maisha ya jera huru
 
Mfyuu me unaniudhi na hizo kesho zako
 
Sehemu ya 28.

Siku hiyo ambayo nilienda hospitalini kupima na kukutwa nilikuwa nina ujauzito wa mwezi mmoja na nusu kiukweli nilikuwa mnyonge mithili ya yatima.

Niliporudi nyumbani tu, mama mwenye nyumba wangu alinifuata, akaanza kunipa hongera huku akiniambia kwamba alikuwa akinidai.

Kwa mawazo yangu ya haraka nilihisi labda hilo deni alilokuwa akinidai muda huo lilikuwa ni kodi ya nyumba yake kwa sababu niliendelea kuishi katika nyumba yake hiyo bila kulipa kodi wala kulipia kitu chochote kile.

“Lakini kama ni kodi yake mbona nilishamwambia na akaniruhusu niendelee kuishi bure ina maana mawazo yake ameyabadilisha?” nilijiuliza moyoni lakini sikuweza kupata jibu.

Ilibidi nimuulize na ndipo hapo akanijibu kwa kuniambia kuwa kiumbe nilichokuwa nacho tumboni ndiyo deni alilokuwa akinidai kwa wakati huo. Nilishangaa sana.

“Unashangaa nini?” aliniuliza huku akinikazia macho kwa ukali.
“Hakuna kitu,” nilimjibu kwa sauti ya chini iliyojaa uwoga.

“Sawa halafu usije ukathubutu kumwambia mtu yeyote kuhusu hili.”
“Sitomwambia.”
“Na ukithubutu nadhani unajua ni kitu gani nitakachokufanya.”

“Ndiyo najua mama.”
“Sawa unaweza kuendelea na mambo yako,” aliniambia kisha nikaingia ndani ya chumba changu.

Kiukweli maisha niliokuwa nikiishi katika nyumba hiyo hayakufanana kabisa na maisha ya binadamu wengine waliokuwa wakiishi maisha yao yenye furaha pamoja na amani tele.

Kuna usemi unaosema kuwa ni bora ukose pesa lakini sio furaha. Ukiwa na pesa halafu katika maisha yako ukakosa furaha hapa pesa huonekana si kitu.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa upande wangu, nilikuwa nikifanya kazi nzuri ambapo kila ilipofika mwisho wa mwezi nilikuwa nikilipwa mshahara mzuri lakini katika maisha yangu nilikosa furaha na yote hayo yalisababishwa na chumba nilichokipanga ambacho ndicho kilichonikutanisha na maswahibu makubwa ambayo sikuwahi kuwaza hata siku moja kwamba yangeweza kunitokea katika maisha yangu.

***
Siku ziliendelea kukatika, miezi nayo ikazidi kusonga mbele. Kitu cha kushangaza mimba niliokuwa nayo haikuwa ikikuwa kama ilivyokuwa kawaida ya mimba nyingine.
Japokuwa tumboni nilihisi kabisa nimebeba kiumbe lakini kwa taswira ya nje sikuonekana kama nilikuwa nina tumbo kubwa.

Kiukweli hayo yalikuwa ni mauzauza mengine, kwa wakati huo wazo lililonijia kichwani mwangu lilikuwa ni kwenda hospitalini lakini kabla sijaondoka kuelekea huko ghafla! mama mwenye nyumba wangu alinifuata na kunighairisha safari hiyo.
“Kwa nini?” nilimuuliza.

“Nimekwambia usiende hospitalini,” alinijibu kwa sauti ya ukali.
“Sawa nimekuelewa,” nilimjibu huku nikimuogopa kama kawaida yangu.
Mpaka kufikia hapo sikuwa na jinsi ya kufanya, ilibidi nikubali niendelee kuishi na mimba hiyo ya ajabu huku nisijue ni kitu gani ambacho kingekwenda kunitokea huko mbeleni.
***
Baada ya kupita mwezi mmoja ndipo hapo nilipochoka kuishi kama mtumwa katika nyumba hiyo.

Nilipanga kutoroka, sikuhofia kitu chochote kile ambacho kingeweza kunitokea, kama ni kufa ama kugeuzwa msukule nilikuwa nipo tayari katika kipindi hicho lakini sio kuona nikiendelea kuishi kama mtumwa na mwisho wa siku nizae msukule.

Nilipowaza kutoroka pia niliwaza na kwenda hospitalini kuitoa mimba hiyo kwa sababu sikuwa tayari kuzaa kiumbe cha ajabu.
Siku hiyo niliondoka nyumbani vizuri kuelekea kazini huku mpango wangu ukiwa kichwani mwangu.

Jioni ya siku hiyo sikurudi nyumbani kama ilivyokuwa kawaida yangu, isipokuwa nilienda nyumbani kwa Theresia yule mfanyakazi mwenzangu.

Nakumbuka nilimsimulia mkasa mzima ulionisibu mpaka nikaamua kumuomba hifadhi ya kukaa nyumbani kwake kwa muda.

“Pole sana Stella kwa changamoto ulizozipitia,” aliniambia.
“Nimeshapoa Theresia,” nilimwambia.
“Kwa hiyo usiniambie kuwa umepanga chumba cha misukule?”
“Ndiyo hivyo shoga yangu nilikuwa naishi nayo chumba kimoja.”
“Yesu wangu! Unajua nilikuwa naishia kusikiaga tu, kumbe haya mambo yapo kweli.”

“Yapo tena usiombe yakukute kama yalionikuta mimi.”
“Na sitamani yanikute kwa kweli maana nahisi ningekufa kabla ya siku zangu.”
“Ndiyo hivyo shoga yangu.”
“Kwa hiyo vipi kuhusu ndugu zako wanajua lakini?”

“Ndugu zangu?”
“Ndiyo ndugu zako.”
“Ndugu zangu wapi hao?”
“Yaani namaanisha wazazi wako.”
“Wazazi wangu?”
“Ndiyo.”
“Ndiyo akina nani?”
“Stella hebu acha masihara yako, ina maana unataka kuniambia huwajui wazazi wako.

Umewasahau?”
“Mbona siwajui?”
“Huna ndugu?”
“Sina,” nilimjibu.
Hapa unaweza ukahisi labda nilikuwa nikifanya utani muda huo lakini huo ndiyo ulikuwa ukweli wenyewe.

Nilikuwa nimewasahau ndugu zangu kwa wakati huo, kama wazazi wangu ndiyo kabisa nilikuwa siwajui wala sikuwa na kumbukumbu yoyote kichwani mwangu.
Japokuwa Theresia aliniuliza mara mbilimbili huku akitaka kuhakikisha lakini nilishindwa kukumbuka kama niliwahi kuwa na wazazi katika maisha yangu.
“Unajua Stella unanishangaza sana?”
“Kivipi?”

“Unavyoniambia kwamba huwajui ndugu wala wazazi wako.”
“Kweli siwajui, kama ningekuwa nawajua ningekuomba unipe hifadhi hapa nyumbani kwako?”
“Nitajuaje kama wapo mkoani je?”

“Mkoa gani sasa?”
“Ndiyo ninakuuliza.”
“Siwajui kwanza sina kumbukumbu kama nilikuwa nao katika maisha yangu.”
“Stella hivi unayoniambia unamaanisha kweli ama unanitania.”
“Thereasia tangu lini nimeanza utani na wewe?”
“Nashangaa.”

“Huo ndiyo ukweli,” nilimwambia.
Hilo lilikuwa ni jambo ambalo kwa mtu yeyote yule lisingeweza kumuingia akilini mwake hata kidogo, mfano wake ni sawa sawa na mtu uamke asubuhi halafu ulisahau jina lako, hilo ni jambo lisilowezekana.

Kwa muda huo ambao nilikuwa nikizungumza na Theresia naweza kusema alihisi labda nilikuwa nimechanganyikiwa kutokana na maswahibu yalionipata hivyo aliniacha kwa muda wa siku tatu ndipo hapo akaja kuniuliza tena kuhusu wazazi wangu.

Jibu langu lilikuwa ni lile lile kwamba sikukumbuka kama niliwahi kuwa nao katika maisha yangu. Hilo lilizidi kumshangaza mno.

“Theresia mbona kama huniamini hivi?” nilimuuliza.
“Sio sikuamini Stella, kwa mambo unayonieleza kiukweli hayaniingi akilini hata kidogo.”

“Tuachane na hayo shoga yangu halafu kuna kitu naomba unisaidie.”

“Kitu gani hicho?”
“Nataka kutoa mimba.”
“Unataka kutoa mimba?”
“Ndiyo mbona umeshtuka hivyo?”
“Una mimba?”

“Ndiyo tena ina miezi minne.”
“Stella.”
“Abee.”
“Una mimba ya miezi minne?”
“Ndiyo.”
“Mbona tumbo lako halionyeshi kama una mimba?”

“Sasa wewe unashangaa tumbo langu kutoonyesha kama nina mimba, mbona huulizi mhusika ni nani.”
“Haya ni ya nani?”
“Ni ya msukule?”
“Msukule?”
“Ndiyo.”
“Kivipi?”

“Kwani ukisikia msukule unaelewa nini?”
“Msukule huu huu ninaoujua kwamba mtu amekufa lakini kiuchwawi anakuwa amegeuzwa msukule?”
“Ndiyo huo huo, nilikuwa nafanyishwa nao mapenzi bila kujua.”

“Yesu wangu!” alisema.
Mambo niliokuwa nikimueleza Theresia kwa wakati huo yalikuwa ni ya kustaajabisha mno. Nilipomwambia kwamba nilibeba mimba ya msukule hiyo yote ilitosha kumwambia nilikuwa katika kifungo cha nguvu za giza na nilihitaji msaada ili niweze kufunguliwa katika kifungo hicho cha mateso.

“Stella hivi unajua kuwa haupo sawa,” aliniambia.
“Sipo sawa kivipi?” nilimuuliza.
“Wewe unajiona upo sawa lakini ukweli ni kwamba haupo sawa kabisa.”
“Nipoje sasa?”

“Unahitaji kufanyiwa maombi haraka sana,” aliniambia huku akinipa ushauri huo.
Hapa ngoja nikwambie kitu kimoja ambacho hukifahamu. Japokuwa nilitoroka katika ile nyumba na kuacha kila kitu huku nikikubali kuanza upya katika maisha yangu lakini bado mauzauza yaliendelea kuniandama kila kukicha.

Siku hiyo ambayo Theresia aliniambia nahitaji kufanyiwa maombi haraka sana, usiku wake niliota ndoto kwamba nilikuwa nimekufa na watu walikuwa wakinipeleka makaburini kunizika.

Je nini kitaendelea?
 
Sehemu ya 29.

Nilishtuka kutoka usingizi, jasho lilinitiririka mno, mapigo ya moyo wangu yalikuwa yakidunda kupita kawaida huku mwili wangu ukisisimka sana.

Niliangalia saa ya ukutani, ilionyesha muda huo ilikuwa ni saa nane usiku, nilipochungulia nje, giza totoro lilikuwa limetawala kwa wakati huo.
Nilikaa kitandani huku picha kamili ya ndoto hiyo nilioiota ikianza kunijia kichwani mwangu.

Nilikumbuka kila kitu kilichokuwa kimetokea kuanzia nilipokufa mpaka pale nilipokuwa nikipelekwa makaburini kuzikwa.
Huku nikiwa sifahamu kitu kilichokuwa kimetokea, mara macho yangu yakaanza kuwa mazito, muda huo sikuweza kufahamu ni nini kilitokea mpaka kusababisha hali hiyo lakini ghafla! nikajikuta nipo ndani ya chumba kimoja.

Huku nikiwa najiuliza maswali kwamba mahali hapo nilifikaje, mbele yangu alisimama mama mwenye nyumba wangu.

“Stella nilikwambia ninakudai kiumbe changu ukajifanya mjanja ukanikimbia, ona sasa mbio zako zimeishia ukingoni,” aliniambia huku akinicheka, sauti ya kicheko chake kilikuwa kikijirudia masikioni mwangu kama vile sauti ya mwang’wi.
“Naomba unisamehe,” nilimwambia huku nikiogopa sana.

“Siwezi kukusamehe.”
Aliponiambia hivyo katika hali ya kushangaza nikashikwa na uchungu. Nilipiga kelele nyingi za kuomba msaada lakini mama mwenye nyumba wangu alibaki akiniangalia huku akicheka mpaka pale ambapo nilikumbwa na usingizi mzito. Sikujua ni kitu gani kiliendelea.

***
Nilipata fahamu nikajikuta nikiwa ndani ya chumba changu kile nilichopanga Sinza. Ndani humo sikuwa peke yangu, tulikuwa wengi sana.

Ile kutazama huku na kule ndipo hapo nilishangaa kumwona Glory. Nilimuita lakini hakusikia wala kuonyesha ishara yoyote kwamba alinisikia kwa wakati huo.
Wakati niking’ang’ana kumuita mara mama mwenye nyumba wangu aliingia.
“Usijisumbue kumuita, huyo ni msukule hawezi kukusikia,” aliniambia kisha akaendelea.

“Nasubiria muda wako ufike na wewe nikufanye msukule kama wenzako.”
“Muda wangu ufike?”
“Ndiyo.”
“Kivipi?”

“Nasubiria uzikwe kwanza,” aliniambia huku akimaanisha kwamba kwa wakati huo nilikuwa nimekufa. Sikutaka kuamini.
Huo ndiyo ulikuwa ukweli kwamba nilikuwa nimekufa kwa wakati huo lakini katika hali ya kustaajabisha kumbe kulikuwa kuna nguvu mbili zilizokuwa zinashindana.
Sikufahamu lolote lile mpaka pale ambapo nilizinduka na kujikuta nipo kanisani, muda huo mchungaji alikuwa akiniombea.

Kiukweli nilishangaa sana, nilijiuliza maswali mengi ilikuwaje mpaka nikafika kanisani hapo na wakati mara ya mwisho nakumbuka nilikuwa katika kile chumba cha misukule?
“Pole sana binti, Mungu ametenda muujiza mkubwa sana katika maisha yako,” aliniambia mchungaji kisha akanyamaza kwa muda kiasi cha kumeza fundo moja la mate halafu akaendelea kuniambia.

“Ulikuwa umelala usingizi wa kifo na kama sio huyu rafiki yako kukuleta kwenye maombi sidhani kama ungekuwa hai.”
Aliponiambia hivyo ndipo hapo kumbukumbu zikaanza kurejea kichwani mwangu na nikawakumbuka wazazi wangu pamoja na ndugu zangu.

Kwa uwezo wa Mungu mama mwenye nyumba wangu alikuja kanisani hapo, akatubu dhambi zake. Lilikuwa ni jambo la kushangaza sana ambalo lilimuacha kila muumini wa kanisa hilo mdomo wazi. Hakukuwa kuna mtu ambaye alitaka kuamini hilo hata kidogo.

Huo ndiyo mkasa ulionisibu kipindi nilipopanga chumba cha misukule bila kujua. Hapa nilichokuwa najaribu kukwambia muda wote huo ni kwamba uchawi upo, unachotakiwa kukifanya ni kumtanguliza Mungu mahali popote pale.

Laiti kama ningemtanguliza Mungu sidhani kama yote haya yangenitokea. Japokuwa kwa sasa imebakia kuwa simulizi tu! ambayo ningependa isimuliwe kizazi hadi kizazi, naomba ujifunze kitu kupitia mkasa huu.

MWISHO.
 
Mwaaah mwaaah barikiwa kipenzi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom