Simulizi: Chumba cha Misukule (Sehemu ya 01)

Sehemu ya 29.

Nilishtuka kutoka usingizi, jasho lilinitiririka mno, mapigo ya moyo wangu yalikuwa yakidunda kupita kawaida huku mwili wangu ukisisimka sana.

Niliangalia saa ya ukutani, ilionyesha muda huo ilikuwa ni saa nane usiku, nilipochungulia nje, giza totoro lilikuwa limetawala kwa wakati huo.
Nilikaa kitandani huku picha kamili ya ndoto hiyo nilioiota ikianza kunijia kichwani mwangu.

Nilikumbuka kila kitu kilichokuwa kimetokea kuanzia nilipokufa mpaka pale nilipokuwa nikipelekwa makaburini kuzikwa.
Huku nikiwa sifahamu kitu kilichokuwa kimetokea, mara macho yangu yakaanza kuwa mazito, muda huo sikuweza kufahamu ni nini kilitokea mpaka kusababisha hali hiyo lakini ghafla! nikajikuta nipo ndani ya chumba kimoja.

Huku nikiwa najiuliza maswali kwamba mahali hapo nilifikaje, mbele yangu alisimama mama mwenye nyumba wangu.

“Stella nilikwambia ninakudai kiumbe changu ukajifanya mjanja ukanikimbia, ona sasa mbio zako zimeishia ukingoni,” aliniambia huku akinicheka, sauti ya kicheko chake kilikuwa kikijirudia masikioni mwangu kama vile sauti ya mwang’wi.
“Naomba unisamehe,” nilimwambia huku nikiogopa sana.

“Siwezi kukusamehe.”
Aliponiambia hivyo katika hali ya kushangaza nikashikwa na uchungu. Nilipiga kelele nyingi za kuomba msaada lakini mama mwenye nyumba wangu alibaki akiniangalia huku akicheka mpaka pale ambapo nilikumbwa na usingizi mzito. Sikujua ni kitu gani kiliendelea.

***
Nilipata fahamu nikajikuta nikiwa ndani ya chumba changu kile nilichopanga Sinza. Ndani humo sikuwa peke yangu, tulikuwa wengi sana.

Ile kutazama huku na kule ndipo hapo nilishangaa kumwona Glory. Nilimuita lakini hakusikia wala kuonyesha ishara yoyote kwamba alinisikia kwa wakati huo.
Wakati niking’ang’ana kumuita mara mama mwenye nyumba wangu aliingia.
“Usijisumbue kumuita, huyo ni msukule hawezi kukusikia,” aliniambia kisha akaendelea.

“Nasubiria muda wako ufike na wewe nikufanye msukule kama wenzako.”
“Muda wangu ufike?”
“Ndiyo.”
“Kivipi?”

“Nasubiria uzikwe kwanza,” aliniambia huku akimaanisha kwamba kwa wakati huo nilikuwa nimekufa. Sikutaka kuamini.
Huo ndiyo ulikuwa ukweli kwamba nilikuwa nimekufa kwa wakati huo lakini katika hali ya kustaajabisha kumbe kulikuwa kuna nguvu mbili zilizokuwa zinashindana.
Sikufahamu lolote lile mpaka pale ambapo nilizinduka na kujikuta nipo kanisani, muda huo mchungaji alikuwa akiniombea.

Kiukweli nilishangaa sana, nilijiuliza maswali mengi ilikuwaje mpaka nikafika kanisani hapo na wakati mara ya mwisho nakumbuka nilikuwa katika kile chumba cha misukule?
“Pole sana binti, Mungu ametenda muujiza mkubwa sana katika maisha yako,” aliniambia mchungaji kisha akanyamaza kwa muda kiasi cha kumeza fundo moja la mate halafu akaendelea kuniambia.

“Ulikuwa umelala usingizi wa kifo na kama sio huyu rafiki yako kukuleta kwenye maombi sidhani kama ungekuwa hai.”
Aliponiambia hivyo ndipo hapo kumbukumbu zikaanza kurejea kichwani mwangu na nikawakumbuka wazazi wangu pamoja na ndugu zangu.

Kwa uwezo wa Mungu mama mwenye nyumba wangu alikuja kanisani hapo, akatubu dhambi zake. Lilikuwa ni jambo la kushangaza sana ambalo lilimuacha kila muumini wa kanisa hilo mdomo wazi. Hakukuwa kuna mtu ambaye alitaka kuamini hilo hata kidogo.

Huo ndiyo mkasa ulionisibu kipindi nilipopanga chumba cha misukule bila kujua. Hapa nilichokuwa najaribu kukwambia muda wote huo ni kwamba uchawi upo, unachotakiwa kukifanya ni kumtanguliza Mungu mahali popote pale.

Laiti kama ningemtanguliza Mungu sidhani kama yote haya yangenitokea. Japokuwa kwa sasa imebakia kuwa simulizi tu! ambayo ningependa isimuliwe kizazi hadi kizazi, naomba ujifunze kitu kupitia mkasa huu.

MWISHO.
stori nzuri,,ubarikiwe sana

hakika Mungu wetu ni mwema.
 
Hatari sana...
Chapter Closed...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom