Simulizi: Bwana Harusi aliyejeruhiwa

ndo wanisema hivi babe?? hebu relax

Mine eyes umeridhika sasa??
Jamani hakuna Deborah kama wa faraji humu, maana moyo umeanza kuloana....tafadhari jamani, kama yupo anyooshe mkono juu tu.....

#Deborah akili mingi mingi...
 
Tuliongozana hadi chumbani mtoto tukimwacha mikononi kwa dada wa kazi. Doreen. “Mke wangu,” nilimwita tukiwa chumbani.

Nasra au Doreen mkuu? Hapa umeniacha
 
SEHEMU YA 78

Alionekana kuchoka kwa urefu wa safari. Nasra alibaki ameketi kitako, macho yake yalikuwa mekundu na yaliyovimba kwa kilio. “Namtaka mwanangu! Kama kufa na nife mwanangu simwachi!” alipayuka na kuangua kilio ndani ya kito cha polisi.

Askari wakabaki wakishangaa,Nasra akazidi kuchanganyikiwa kwa kelele za kilio. “Kama ni makosa niliyafanya mimi!. Kama niadhabu nastahili nipewe mimi! Lawama na mateso yote nastahili! Lakini sio kumyima mwanangu haki yake! Haki ya kulelewa na mama yake mzazi anastahili....“

“Kelele ebo!! Kama hayo yote unayajua kwa nini ulivunja ndoa yako?” nikabwatukia kwa ukali. Ikabidi polisi wafanye kazi ya kumtuliza. Na kilichofanyika ni kumuingiza mahabusu, mimi na Debora tukakabidhiwa mtoto, lakini tukatakiwa kufika siku inayofuatia wakati polisi wanakamilisha uchunguzi.

Tukaondoka kurudi nyumbani, Nasra tukamwacha selo. nikawajulisha ndugu zangu juu ya mafanikio niliyapata katika songombingo lile.

Siku iliyofuatia tulirudi kituo cha polisi, kwa ajili ya mahojiano, nilionana na mkuu wa kituo ambaye aliniuliza maswali mawili matatu juu ya wizi ule na mimi nikamweleza ukweli.

“Kama ni hivyo mimi nadhani jambo hili mlimalize kwa hekima tu.”mkuu wa kituo alishauri “Kivipi?”

“Nadhani muweke makubaliano ya amani, juu ya mwanenu, unajua mtoto ni wenu wote, siyo vizuri mkiendelea kugombana kwa jambo hili.”

Tuliupokea ushauri wa yule kamanda, Nasra akachiwa huru. Baada ya kuwa huru, kwa pamoja tukazungumza naye, na tukakubaliana awe anakuja nyumbani kwangu kumsalimia mtoto muda wowote anaojisikia bila kuathiri hukumu ya mahakama.

Kuanzia wakati huo Nasra akawa anakuja nyumbani kwangu mara kwa mara kumjulia hali mtoto wangu.

Katika nyakati hizo, nikaja kugundua mwanamke yule aliachana na hawara siku chache baada ya ndoa yao, kuvunjika kwa ndoa yao ni baada ya kubainika kwamba alifunga ndoa ilihali akiwa bado ni mke wa mtu.

Nikaendelea kubaini kwamba, kumbe baada ya ndoa ile kuvunjika, bwana yule hakutamani tena kumwoa Nasra, akawa na wanawake wengine katika maeneo mbalimbali, huku nasra akibakia ndani akililia ndoa.

Penzi langu na Debora lilizidi kunoga, kama nilivyosema awali wote tulikuwa kwenye hamu kubwa.
 
Sehemu ya 79 .

Hata hivyo, kama wasemavyo Waswahili:

Kisicho riziki, hakiliki. Pamoja na penzi moto moto lililokuwepo kati yetu, huku suala la ndoa likizidi kugonga vichwa vyetu, nikaja kubaini kwamba, suala kufunga pingu za mausha na mwanamke yule lingekuwa gumu kutokana na jambo moja tu. Tofauti ya dini zetu.
Kwa kweli jambo hilo lilitukosesha raha, na hii ilichangizwa na sote kutokuwa tayari kuziacha dini zetu na kumfuata mwenziye.
Kikwazo cha dini kikayeyusha ndoto zetu, tukaendelea kuishi pamoja bila kufunga ndoa.

Maisha yangu na Debora yalikuwa mazuri sana, pesa na mafanikio niliyokuwa nayo ikanifanya nifurahie maisha wakati wote. Mtoto wangu Mwanda, naye akazidi kukua kwa kimo na hekima.

Mke wangu wa zamani,Nasra. Alikuwa akija kumwona mwanaye kila mwisho wa wiki, yanii jumamosi na jumapili. Na mara nyingi kila alipokuwa akifika, nilihakikisha haendi popote na mwanangu, walikaa kwenye bustani asubuhi hadi jioni. Alipondoka mtoto alibaki kwangu.

Kitendo cha kutokuwa huru na mwanaye kilikuwa kikimuudhi mno Nasra, lakini mimi sikujali, nilichokuwa nakitaka kwa wakati huo ni kubaki na mwanangu, japokuwa nilitambua nilikuwa nikikosea lakini sikuomwonea huruma hata kidogo mwanamke yule. Nilimwona ni binadamu asiyestahili kuonewa huruma.

Kila alipokuwa akifika kumwona mtoto, nilikuwa nikihisi hasira kali dhidi yake, mambo aliyonifanyia kipindi cha nyuma yalikuwa yakijitengeneza akilini mwangu mara kwa mara.

Kuna kitu nilisahau kukisimulia. Wakati mtoto wangu namrejesha mikononi mwangu, baada ya kuwa ameibwa na Nasra, kule Nguruka. Nilitafuta dada wa kazi. Msichana mdogo tu wa miaka kumi na tano au kumi na saba, binti huyo aliitwa Tatu.

Wakati mimi na Debora tukiwa bize na kazi, Tatu ndiye mara nyiingi alikuwa akibaki na Mwanda, alimwangalia asubuhi hadi jioni, alimwogesha, akampa chakula na kila kitu anachostahili mtoto.

Nilimpa tatu maelekezo juu ya utaratibu wa Nasra kumwona mwanaye.
Nilimwambia kila Nasra alipokuwa akifika nyumbani kwangu kumwona mwanaye, kama sipo nyumbani, ilikuwa ni lazima Nasra amwombe Tatu ndipo amwone mtoto, kisha Tatu naye sharti awasiliane aidha na mimi au mpenzi wangu Debora
 
Naomba unijulishe kila ukiweka muendelezo wa hizi story mbili,, yaan na ile ya ulinisaliti juliet
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…