SEHEMU YA 83
Nafsi yangu ilikiri mwanamke si mtu wa kumwamini, hata kama atakueleza anakupenda huku anatokwa machozi ya damu. Viumbe hao hawaaminiki.
Nikaendelea kujifunza, katika maisha haijalishi uwe mtanashati kiasi gani, au una nguvu nyingi, aidha ni tajiri mkubwa, hayo hayawezi kuwa kinga ya kutosalitiwa.
Niliamini wanawake ni watu wenye kufanya usaliti wakati wowote wakiamua. Mwanamke kama Debora, aliyejitoa kwangu kwa nguvu na akili zake zote, aliyenipenda kwa muda mrefu, eti naye alikuwa amenisaliti!!!. Sasa nawaamini vipi tena.
Moyo wangu ulivunjika! Nikiwa chumbani nikapanga akitoka tu kuoga nampa vidonge vyake kisha penzi letu linamalizika. Niliwaza hayo japokuwa niliamini lazima atanibembeleza .
Dakika chache badaye, Debora alitoka bafuni, alikuwa kwenye kanga moja, nguo ile ilikuwa imenata kwenye manyama nyama yake, embe dodo zake zilikuwa wima, zimenona. Kiuno chake kilichoshikiria makalio na mapaja mazuri yalivutia kiasi ambacho kama isingekuwa makandokando yale, ningemrukia na kumfyekelea mbali.
“Vipi?”aliniuliza.
“Umebarikiwa. Mashallah”
“Mh,” akaguna.
Nikaendelea. “Bahati mbaya, urembo huo siufaidi peke yangu! Ni hasara kubwa tu.”
Niliposema hayo, macho akayapepesa kama Kinyonga.
“Sijakuelewa.”
“Unanisaliti.”
“Mimi?” “Unanisaliti ndani ya chumba hiki!” nikaendelea kumpasulia.
“Wewe unaongea nini?” “Usijitie uhayawani Debora, ile mipira ya kiume iliyokuwa kwenye droo iko wapi?”
“Mipira gani?” akazidi kujifanya hakuna ajuacho.
Nikamwangalia kwa chati, hasira kali ikiwa inachemka kifuani, naye bila woga akawa ananiangalia usoni, macho yakiwa makavu.
“Mipira gani nakukuliza?” akaniuliza tena. Alionekana kujiamini.
Hapa ngoja niseme jambo moja. Wanawake wengi ambao ni viongozi wa kisiasa au wenye nyadhifa kubwa katika taasisi fulani au serikalini huwa ni viumbe wanaojiamini kupitiliza.
Siyo makazini kwao hata majumbani mwao, ni viumbe wasiogopa lolote, sio watu wa kujishusha hata kama wao ndio wakosaji, wakati wote hujiona wako sahihi. Wanawake viongozi huathiriwa sana na mazingira.
Pamoja na kwamba ni watu wanaojua kupenda wakiwa wamezama penzini, lakini ni viumbe wajanja na hatari wanapokuwa wamekinaiwa na wapenzi wao!