Simulizi: Baradhuli mwenye mikono ya chuma

Simulizi: Baradhuli mwenye mikono ya chuma

SURA YA KUMI NA MOJA

Walifika eneo la ajali wakashuhudia gari la Filbert likiwa nyang'anyang'a damu zimetapakaa. Lori la mchanga halikujeruhiwa sana zaidi ya kubondeka kidogo kwa mbele. Watu kadhaa walikuwa wamezingira magari hayo wakiwa na nyuso za huruma mchanganyiko na mshangao.

"Samahani, wahanga wa ajali wapo wapi?" K square alimuuliza mmojawapo wa watu waliojikusanya pale wakati Mtemvu na Inspekta wakiwa wanarusharusha macho yao kana kwamba wanatafuta kitu.

"Wameshachukuliwa. Ambulance imewabeba muda si mrefu yani!"
"Wamewapeleka wapi?" K square akaongezea swali. Kabla hajajibiwa, sauti ya king'ora ilivuma. Gari la kubebelea magari yaliyoharibika liliingia eneo la ajali likakusanya gari la Filbert. Haikujulikana nani aliyetaarifu watoaji hao wa huduma, labda walipata taarifa juu ya aliyepata ajali ni mtu mzito na huenda ikawa ni fursa.

“Twendeni hospitali." Inspekta Vitalis aliwaambia Mtemvu na K square. "Kwa taarifa nilizopata ambulance iliyokuja kuwachukua wahanga ilikuwa imeandikwa MASSANA HOSPITAL ubavuni. Hivyo tuelekee huko."
"Sawa!"

Walipoingia kwenye gari ndipo wakagundua Pius hakuwepo pamoja nao. Walitizamana kabla hawajaulizana na kushuka kwenye gari wamtafute mwenzao. Kila mmoja alichukua njia yake kusaka akiita.

Kwa mbali ndani msitu, Inspekta aliona kitu chenye rangi ya njano kikiishilia. Hakujiuliza mara mbili akafungua miguu yake kukimbilia kule alipoona alichotilia shaka. Alitoa bunduki yake akaishikilia mkononi akiendelea kuzama msituni.

Macho yake yaliyokuwa yanapepesa huku na kule yalimuona mtu aliyevalia nguo ya njano akikimbia, mkononi kambebelea mtu kwa mbele. Alimtizama vizuri mtu aliyebebwa kwa haraka akagundua ni bwana Pius kwa mujibu wa nguoze.

Alifyatua risasi kumlenga mwanaume mwenye shati la njano lakini mwanaume huyo hakukoma kukimbia haraka kana kwamba hajaguswa na risasi! Mwishowe risasi za inspekta Vitalis ziliisha mwanaume yule hata asisimame.

Inspekta aliongeza kasi zaidi ya kukimbia hatimaye akamshika bega mwanaume mwenye shati la njano na kumvuta kwanguvu. Ghafula mwanaume huyo akapotea! Yeye pamoja na Pius!

Inspekta alisimama ameshika kiuno akitizama kila upande kama mtu anayefikiria jambo. Ghafula alisikia mtu amekatiza nyuma yake upesi, alipogeuka hakuona mtu yeyote isipokuwa miti tu.

Alihisi kabisa kuna mtu karibu yake japokuwa hamuoni. Aliinama akachota mchanga na mkono wake wa kuume kisha akatumikisha milango yake ya fahamu kutambua alipo mtu anayemtafuta, akagundua yupo nyuma yake.

Kugundua yu upande gani sasa huko nyuma aliumwaga mchanga kwa kuzungusha mkono, mahali mchanga ulipogota akaagiza teke kali lililomsulubu vema aliyekuwa haonekani na kumtupia chini. Alionekana kwa punde alafu akapotea tena.

Inspekta Vitalis alitumbua macho kutafuta. Hakuona wala kuhisi kitu kwa dakika tatu. Simu yake ilitetemeka mfukoni akaitoa na kuitizama – Mtemvu. Aliipokea haraka akaiweka sikioni.

“Ndio mkuu … Nipo msituni namtafuta bwana Pius … Upo nae? … Sawa, sawa basi ntakuwepo hapo muda si mrefu!”

Alikata simu na bumbuwazi la kupata taarifa Pius amepatikana ilhali anaenyeka kumtafuta. Ila zaidi ya hapo alipata hofu – huyo kweli waliye naye ni Pius, ama ni mtu mwenye shati la njano? Kama ndiye, je mtu mwenye shati la njano yu pande zipi huku hajamuona wala kumuhisi kwa dakika kadhaa? Atakuwa ameelekea huko? Inspekta alichanganyikiwa na maswali. Hakuwa na la kufanya zaidi ya kuanza kukimbia kwenda alipoitwa akifuatisha nyayo za viatu vyake asipotee msituni.

Alifika akamkuta Mtemvu na wenzake wawili ndani ya gari wakionekana wamechoka kwa kungoja.

“Pole sana inspekta kumbe alikuwa ametoka kwenda kukojoa. Tuondoke sasa, tunazidi chelewa.” Alisema Mtemvu.
“Sawa.” Inspekta Vitalis akaitikia kwa kumezea. Alimtizama Pius kwa macho ya mashaka. Na alifanya hivyo safari yote akitumia kioo cha gari kilichoketi juu ya kichwa chake lakini hakupata lililothibitisha walakini wake.

***

Muendelezo soma hapa
 
SURA YA KUMI NA MBILI

Muziki ulisikika kwenye simu kubwa nyeupe iliyokuwa imelala juu ya meza ya plastiki ya kampuni ya Serengeti. Bwana Raheem aliyekuwa amekaa peke yake kwenye kona ya bar maarufu jijini Dar aliitizama simu hiyo kiooni akaona jina la Mtemvu. Alisonya kisha akaendelea kunywa kinywaji chake kilichokuwa ndani ya glasi ndefu yenye kiuno chembamba.

Simu ilipiga muziki mwishowe ikakata. Ila baada ya muda kidogo, ikapiga tena muziki. Raheem aliitizama kwa jicho la hasira kabla hajaamua kuipokea ili kumuepushia usumbufu zaidi.

Alifoka:

“Nini!” Akiwa amekunja sura. Ila baada ya muda alinywea na kuwa mtulivu zaidi akiubinua mdomo wake.
“Muda gani? ... Kwahiyo mpo wapi kwa sasa? ... Ok, nitakuwa hapo muda si mrefu!”
Aliirudisha simu juu ya meza akakuna ndevu zake.
“Hiki kijamaa kina matatizo sana!” Aliongea mwenyewe. Alikunywa kinywaji chake mafundo kadhaa kisha akaendelea kuteta kama vile kuna mtu anamsikiliza.
“Kwanza kioga kama mwanamke! ... Sijui kilienda wapi huko kikabinuliwa na lori!”

Akanywa tena mafundo mengine na kumaliza kabisa knywaji chake.

“Najuta sana kufanya kazi na hawa watu waoga hivi. Kama ningelijua mapema lile dili nisingeliwashirikisha kabisa. Hivi inakuaje kumuua mtu mmoja tu inakuwa ishu kubwa hivi? Suush! Huu ni wakati wangu muafaka wa kujutia kumtupilia mbali na kumlaghai bwana Kim. Najua asingenisumbua katu! Uoga wangu waniponza vibaya sana.”

Alipiga kichwa chake kofi akiing’ata lips.

Ni miezi kadhaa tu huko nyuma alikuwa mtu wa kwanza kushirikishwa wazo adhimu la kuua tembo na kuwapokonya pembe ili wapate zisafirisha kwenda Asia kwa kupitia madalali wa ulaya. Wazo hilo lilikuja mezani kwake pale alipokuwa anaperuzi barua pepe akakuta ametumiwa kipande kidogo cha habari kutoka kwa bwana Kim, kikieleza faida kinaganaga za pembe za tembo huko mashariki ya mbali.

Kwa mara ya kwanza alipuuzia ujumbe huo ambao haukuambatana na maneno mengine yeyote, ila baada ya bwana Kim kumshawishi zaidi kwa kumtumia namba za madalali hao wa ulaya akiweka wazi pesa nono za biashara hiyo, Raheem akadakwa uchu.

Kwa siri, tena kubwa sana alisuka mpango huo na bwana Kim ya kwamba atumie dhamana ya cheo chake kizito bandarini kufanikisha hilo. Ila alikuja kugundua asingeweza kufanikisha kazi hiyo mwenyewe. Angekwapuaje pembe hizo za tembo huko mbugani kwa wepesi? Ilimlazimu amtafute na amshirikishe bwana Pius wa TANAPA.

Kuhusu usalama wake na wa bidhaa alimtafuta Mtemvu wa jeshi la polisi huku usafirishaji wa bidhaa hiyo mpaka ulaya akimshirikisha Filbert na K square kwa kutumia kampuni zao kubwa za usafirishaji wa bidhaa baharini.

Tamaa hulevya. Raheem aliona mgao wa bwana Kim wa asilimia sitini na tano ni mkubwa mno, angepata pesa ndogo. Alihamishia biashara yote kwa wenzake kwa makubaliano kwamba atachukua asilimia arobaini na tano na itakayobaki atawapa wagawane, makubaliano yakapita. Bado pesa ilikuwa ni nyingi mno.

Raheem alitikisa kichwa chake akijitahidi kufuta kumbukumbu hiyo akilini. Aliiona ni kama jinamizi linalomuandama na sasa lataka kumtoa roho. Alilipia kinywaji akanyanyuka kufuata gari lale la kisasa aina ya Jaguar. Alitokomea eneo hilo kwa mwendokasi mkubwa akifurahia mlio wa nguvu unaotoka kwenye gari lake uliofanya wapita njia na madereva wengine wamtizame.

Furaha hiyo ya majigambo ilikuja kukoma pale kwa kutumia kioo cha dereva alipomuona mtu kwenye viti vya nyuma. Haraka aligeuza shingo kutizama asione chochote, aliporudisha uso mbele akamkuta mtu yule kwenye kiti cha mbele alafu kufumba na kufumbua akapotea!

“Shit! What the ***!”

Raheem alitoa macho. Alipoteza umakini, gari likayumbayumba. Alijitahidi kulimudu na kulirudisha mstarini akafuta uso na kiganja chake kama mtu ambaye haamini alichokiona. Alishusha pumzi ndefu akakung’uta kichwa chake kofi.

“Na mimi naanza kuwa kama wale wapumbavu!”

Akasonya. Mapigo yake ya moyo na pumzi vilirejea katika hali ya kawaida lakini macho yake bado yalikuwa yanarandaranda yakitizama kila upande. Ndani ya dakika zisizopungua tatu, simu yake ikaita. Ilikuwa imejilaza kwenye kiti jirani. Alishituka. Kutizama ni nani akaona namba mpya. Alinyakua simu na mkono wake wa kushoto akaibandika sikioni.

“Haloo! … Ndio mimi, nani mwenzangu? ... Mgeni yupi? … Shenzi!” Alikata simu akasonya kwa hasira.
“Pumbavu kweli! Unadhani mimi wa kuchezewa chezewa enh? Kawatishe haohao!”

Alipomaliza tu, ujumbe ukaingia kunako simu. Mlio ulimjulisha hilo, akaiteka simu na kiganja cha mkono wake wa kushoto akaibia kuusoma ujumbe.

‘Tizama kushoto.’ Ujumbe uliagiza. Raheem pasipo kujiuliza mara mbili akageuza uso kutizama alipoelekezwa. Aliona Lori lililobeba mawe makubwa laja kwa kasi likitokea barabara ya kuchepukia iliyokuwepo hatua kadhaa kwa mbele. Haraka alisinya breki kwanguvu zote bila ya mafanikio – gari lilizidi kwenda. Nalo lori lilipiga honi kali likiendelea kutiririka kana kwamba breki zimefeli.

Gari la Raheem ghafula lilizima hatua kadhaa tu mbali na lori linalokuja kama faru aliyejeruhiwa. Moyo wa mwanaume huyo ulidunda kama ngoma ya mtaa. Milango haikufunguka wala gari halikusonga. Hakuwa na la kufanya zaidi ya kufunga macho yake angojee kifo.

Muda ulipita asihisi chochote. Alifungua jicho moja kwa uwoga akatizama, hakukuwa na lolote lile lililotukia. Sauti za honi na za watu zilisikika tokea nyuma ya gari lake.

"Wewee sogea bwana unatuchelewesha!"

Pipiiiii! Pipiiiiiii!

Foleni ya dharura ilikuwa tayari ishajiri. Raheem akiwa hajielewi, alikanyaga mafuta akaduwaa gari lasonga mbele. Kwa muda kidogo akili yake iliganda akabaki ameachama. Alikuja kushtushwa na muziki wa simu lakini hakuthubutu kupokea wala kuitizama mpaka pale aliposikia mlio wa ujumbe, akainyakua simu asome.

'Pole muheshimiwa, mengi yaja. Hautofaidi hizo pesa kamwe!'

Raheem akang'ata meno na kupiga ngumi usukani. Kwa pupa aliajiri vidole vyake juu ya vibonyezeo akaandika akibonyeza kwanguvu.

"Wewe ni nani?"

Ujumbe haukwenda. Raheem akalaani kwa tusi. Alifungua kidroo kilichopo pembeni ya usukani akatoa bunduki yake ndogo.

***

Muendelezo soma hapa
 
Nimekaa kiti cha Mbele kuisubiria..... Ngoja tusubirie Mkuu.

Angalia usifikie katikati ukaanza kuweka restrictions zingine.

Haya tunasubiri Kiongozi .........

Namie nipo tuu

Na Mimi nimo.

Naisubiri tu kwa shauku hiyo simulizi ya baradhuli hyo




So far so good.asante.ila usikae wee ukatuweka kwenye kusubiri

Nzuri sana

Ooo saaaaafi

story nzuri kesho uni tag mkuu

Safi twende sawa

Aisee kumbe mtu mwenyewe anageuka moshi duu. Haya tupo tunaendelea.

Nimewakuta sasa riwaya tamu sana ,,,unitagi pls muendelezo

Hebu nitumie kusoma hii

kajitahidi sana utunzi

Haya haya mkuu tuko pamoja
Haya karibuni wakuu tuendeleze mambo.
 
Jamaa wanapunguzwa mmoja mmoja. Hivi haiwezekani kumkodisha huyo jamaa mwenye SHATI LA NJANO aje kuwapunguza wapiga deal?
 
Kwa kiswahili cha zanzibar ukisema baradhuli manake mlawiti
IMG_20170202_055802.JPG
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom