Habari hii inawezekana kuwa ya kweli,kuna rafiki yangu alinisimulia kisa cha bibi mmoja ambaye ana wajukuu wanaweza kuolewa na kuzaa kama wasingekuwa wanasoma.Siku moja yule bibi alitoka maeneo ya nyumbani kwake akajisogeza karibu na chumba cha huyo rafiki yangu ila kwa nje nadhani hakujua kama ndani kuna mtu hajalala maana ilikuwa ucku,basi akawa anaongea na simu anasema ''njoo bwana mimi siwezi kulala,njoo...'' eeh yule rafiki yangu baada ya muda akaona anatokea kijana wakaongozana kuingia kwa yule bibi alishangaa maana yule bibi alikuwa anaheshimika.
Kwa hiyo mi naona tabia ya mtu haizeeki au huenda na wazee wanapandisha mizuka ila wanajizuia,
Huyu mpenzi wako alikosea kuendekeza kuitwa baba watoto na mtu ambaye hazijui tabia zake tangu mwanzo,ila nampongeza kwa kumpotezea huyo bibi vinginevyo mngeanza kushare.