Simu za Mkopo: Unalipia karibu simu mbili

Wickama

Platinum Member
Joined
Mar 8, 2009
Posts
1,568
Reaction score
1,350
Wakuu,
Kiufupi ukifatilia wimbi la "simu za mkopo" hususan kutoka makampuni makubwa ya mawasiliano ya simu za mikononi utagundua mteja akimaliza mkopo basi kalipia karibu simu mbili za cash. Mteja anakopa Samsung Galaxy A15 (kwa cash ni Tshs 450K) tuseme kwa mwaka. Kila siku anakatwa Tshs 2200. Mwaka ukiisha kalipia Tshs 872 K. Sijui hii imekaaje na mamlaka zinazosimamia makampuni haya wala zile zinazolinda consumers. Sababu hata benki hazitozi riba za kiwango hiki kwenye mikopo yao.
 
Kwani umelazimishwa kukopa mzee kama huna uwezo baki na kiswaswadu kinachokisumbua ni umekimbia umande unataka upewe mkopo wa simu mwaka mzima halafu malipo ulipe hela ya cash that is bullshit......ujajiuliza ukiibiwa simu,ukifa,ukiharibu simu hizo hasara zinarudi vp ?

Kwa upande mwengine wanasaidia sana jamii watanzania wengi kutoa tsh 300k kwa pamoja anunue simu hawezi ila kutoa buku au buku jero kila siku anaweza.
 
Mikopo benki inakatiwa bima in case ukifa hujamaliza kulipa. Yet wanatoza almost 20%. Hii ya simu za mikopo ni 90%+
 
Siku hizi watu wanakopa halafu wanaenda kuziflash anatokomea mbali kampuni inakula hasara. Katika watu 10 waliokopa 4 tuu ndio wanamaliza kwa uaminifu.
Nchi imekosa watu waaminifu balaa, sasa mtu kwa shida zake anaenda kukopa, then anaishia kuiba maana huo ni wizi.

Tunakoelekea kwa lifestyle tunayoishi, kila mtu ataishia kukopa tu, iwe direct au indirect! Watu wajifunze kuwa waaminifu.
 
Nahisi kila mtu huwa anajua kuwa hapa nimedhulumiwa😅 una maana akiflash hawataijua iliko? Si huwa simu ina IMEI #
Siku hizi kuna mafundi wanafuta mpaka IMEI namba hizo simu inakuwa huwezi kuitrace kabisa ninachoshangaa kwanini bado wanaendelea kukopesha
 
Nchi imekosa watu waaminifu balaa, sasa mtu kwa shida zake anaenda kukopa, then anaishia kuiba maana huo ni wizi.

Tunakoelekea kwa lifestyle tunayoishi, kila mtu ataishia kukopa tu, iwe direct au indirect! Watu wajifunze kuwa waaminifu.
Hakuna watu tumekuwa wezi na matapeli kama watanzania. Mtu anakopa ila kwenye kulipa ndio inakuwa mtihani.

Kuna fundi nilienda kutengeneza simu ndio nikaona anafanya hizo kazi za kutoa software ya mkopo na anafuta IMEI namba kabisa. Vijana wanajaa kabisa. Ni wizi kila sehemu
 
Wakuu,
Kiufupi ukifatilia wimbi la "simu za mkopo" hususan kutoka makampuni makubwa ya mawasiliano ya simu za mikononi utagundua mteja akimaliza mkopo basi kalipia karibu simu mbili za cash. Mteja anakopa Samsung Galaxy A15 (kwa cash ni Tshs 450K) tuseme kwa mwaka. Kila siku anakatwa Tshs 2200. Mwaka ukiisha kalipia Tshs 872 K. Sijui hii imekaaje na mamlaka zinazosimamia makampuni haya wala zile zinazolinda consumers. Sababu hata benki hazitozi riba za kiwango hiki kwenye mikopo yao.
A15/A16 bei ya jumla ni chini ya 350K, wao wanachukua kwa Jumla sio reja Reja so sometime inafika hadi mara 3 ya bei halisi.

Simu za mkopo ni kutiana tu umasikini.
 
Mama Rais Mh. Samia Hassan Suluhu, msaidie mwanke huyo ( mama huyo apate haki yake ).
Benki ikitoa mkopo kwa riba ya 90% utasikia BOT au mamlaka nyingine wanailima😁
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom