Simu za Mikopo Scheme Mpya za Utapeli

Simu za Mikopo Scheme Mpya za Utapeli

Mkuu ila hizi kampuni kwa sasa huwa zina bima yaani wamejiandaa kwa lolote jambo
Ambayo hiyo wanailipia, which is ni ongezeko la gharama kwenye biashara. Bado walipe wakopeshaji, wafanyakazi, ads, kodi na mambo mengine.
 
Katika miaka ya karibuni, mfumo wa kununua simu kwa mkopo maarufu kama “Lipa Mdogo Mdogo” umeenea sana Afrika Mashariki. Kampuni kama Watu Credit zimejijengea jina kwa kuahidi wananchi kupata simu haraka bila kuwa na fedha zote mkononi. Ndani ya saa chache unaweza kuondoka na simu mpya uipendayo kama Samsung Galaxy A06, huku malipo yakigawanywa kidogo kidogo kila siku au kila wiki.
View attachment 3554867

Nitoe angalizo, kwa namna yoyote sina nia wala dhumuni lolote la kuharibu biashara ya mtu/ watu wala kampuni yoyote ile.

Kwa mtazamo wa kwanza, mpango huu unaonekana kuwa suluhisho kwa watu wenye kipato kidogo. Lakini nyuma ya urahisi huo kuna simulizi nyingi za maumivu ya kifedha ambazo watu huzipitia.
View attachment 3554868
Katika soko la kawaida la nchi za Afrika Mashariki, simu aina ya Samsung Galaxy A06 siyo simu ya gharama kubwa sana. Nchini Tanzania, bei yake inapatikana kati ya takribani shilingi 245,000 hadi 350,000 mtanirekebisha wauza simu kama nimekosea tarakimu.
View attachment 3554869
Kwa nchini Kenya, bei yake huanzia takribani KSh 11,500 hadi 14,800, sawa na takribani shilingi 230,000 hadi 350,000 za Tanzania.

Lakini hadithi ni tofauti pale ambapo unapoinunua kwa mkopo, taratibu usipaniki utaelewa.
View attachment 3554870
Baadhi ya watumiaji hudai baada ya miezi kadhaa ya kulipa kila siku, jumla ya fedha walizolipa huzidi hata shilingi 500,000, huku bado wakibakiwa na deni kubwa la kurejesha. Mfumo wa malipo ya kila siku—kwa mfano karibu shilingi 2,900 kwa siku—unaweza kuonekana mdogo mwanzoni, lakini unapojumlishwa kwa miezi mingi hugeuka mzigo mkubwa.
View attachment 3554875
Ukisoma matangazo yao mara kadhaa utaona wakitoa mchanganuo wa gharama kwa siku, wiki pamoja na mwezi ila hawatoi hesabu kamili ya jumla ya pesa ambazo unatakiwa kulipa kukamilisha malipo. Kwa kwa mtu masikini au wenye kipato cha chini kusikia malipo ya 2500 kwa siku ataona ni kitu rahisi ila piga hesabu 2500 kila siku kwa mwaka ni shilingi ngapi?
View attachment 3554872
Wengine wanasema presha huongezeka zaidi kwa sababu simu inaweza kufungwa moja kwa moja endapo malipo hayatafanyika kwa wakati. Ndani ya mfumo, mteja anaweza kuonywa kuwa ana masaa chache tu kabla kifaa chake hakijazimwa.
View attachment 3554873
Ni kweli kabsa, kuwa mipango ya mkopo imewasaidia watu wengi kumiliki simu za kisasa maarufu kama Smartphones, hasa wale ambao wasingeweza kulipa pesa yote kwa mkupuo ama kwa pamoja. Simu leo siyo anasa tu; ni chombo cha kazi, biashara na mawasiliano na hitaji la lazma.
View attachment 3554874
Lakini kuna wakati kama watanzania tunapaswa kukubaliana kuwa baadhi yetu tunawaumiza sana watanzania wa kipato cha chini. Kwa watu wenye kipato kidogo, mpango huu unaweza kugeuka kuwa kama mtego wa madeni.
View attachment 3554871
Mtu anachukua simu akiamini kuwa analipa kidogo kidogo, lakini mwishowe wanajikuta wamelipa 2X au hata zaidi ya thamani halisi ya simu.

Ndipo swali la msingi linapoibuka: Je, hizi ni huduma za kifedha zinazowasaidia wananchi, au ni mfumo unaowalazimisha maskini kulipa gharama kubwa kuliko thamani ya bidhaa?
Sasa hiyo ni ujinga wa hao wanaokwenda kukopa kwa nini wasigome kwenda kukopa kwani wamelazimishwa?unakopa simu kwani usipokuwa na simu utakufa?
Hizo pesa za kila siku unazowapelekea kwa nini usizihifadhi ndani kwako kisha zikitimia ukanunue simu mwenyewe dukani.
 
Back
Top Bottom