Hapa nawaona ndugu zangu bado mnaile kasumba ya kununua vitu kwa kuzingatia majina na sio specification.
Hio oppo ina tumia chip ya mediatek na mnayafahamu madhaifu ya mediatek, developer wengi hawadil nazo hivo, kuchelewa kupata update au kutokupata kabisa.
Nm12, ndio iliotumika hivyo huwezi ishindanisha na note 8 , Nm11imetumika.
Izingatiwe kadri namba ya Nm inavyozid ku ndogo ndipo ukaaji wa chaji na ufanisi wa kubrowse unavyoongezeka.
Oppo inatumia fast chaja ya ten watt ilhali note 8 inatumia 18watt.
Camera ya oppo ni dhaifu sana kwa hio ya note 8 japo zote ni 48mp.
Bei ya simu pia note 8 ni kuanzia laki tatu na hamsini elfu za Kitanzania na hio sijajua bei ila nahisi ni zaidi ya hapo.
Ir blaster ni kitu muhimu pia.
Hakuna cha ziada kinachoishinda note 8 sema mnanunua bidhaa kwa kufuata mkumbo .