Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,529
Kama kuna ujinga uliokubuhu na kupata PHD, ni kutoka kwa Serikali yetu na Wanasiasa wetu.
Ni vipi leo tudai Blackberry simu yenye uwezo wa kupata mtandao wa intaneti ndio iwe kichocheo cha kuboresha maisha ya Mtanzania?
Nilifikiri Elimu, Afya, Chakula, Ajira, Bei nzuri za Mazao,Maji, Umeme Kilimo bora, Uvuvi na Ufugaji wa kisasa ndio vyanzo vya kuboresha maisha.
Zaidi ongezea Siasa Safi na Uongozi katika vitu muhimu kuongeza ubora wa Maisha na kuleta maendeleo katika Taifa.
Sasa kule kijijini Simu ya intaneti itamsaidia nini mwanancho ambaye hana umeme wa kuchaji hiyo simu na ni lazima atembee maili 3 kwenda kwenye umeme wa kuaminika?
Je hizo gharama za mawasiliano tunazolalamika kila siku za kutaka miundombinu ya mawasiliano ibadilishwe, itasaidia vipi ufanisi na kuboresha maisha ikiwa bado tunatumia mitambo na utandawazi wa zama za kale?
Kinachosikitisha ni hili tamko lenye mamlakakuwa kijisimu cha Blackberry kitaboresha maisha ya Mtanzania!
Ama kweli Mtanzania unaendelea kudanganywa na Serikali yako na kufanywa mjinga kila siku!
Maisha Bora kwa kila Mtanzania kupitia Blackberry!

Serikali yaipongeza Vodacom kuzindua Blackberry
na Amana Nyembo
SERIKALI imeipongeza Vodacom Tanzania kwa kuzindua simu za kisasa za Blackberry kwani zitaboresha maisha ya Watanzania.
Akizindua simu hizo mwishoni mwa wiki, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Balozi Khamis Kagasheki, alisema simu hizo zenye kasi kubwa ya intaneti zitasaidia kuboresha maisha ya Watanzania.
Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na mtandao wa Vodafone imezindua simu mpya na ya kisasa ya Blackberry nchini yenye mvuto wa aina yake na uwezo mkubwa wa kuzuru internet pamoja na huduma ya kutuma na kupokea barua pepe popote nchini.
Awali, Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania, Ephahim Mafuru alisema simu kwa kuanzia na Vodacom kupitia mtandao wa Vodafone wamezindua simu za Blackberry za aina mbili ambazo ni Curve 8310 na Pearl 8110 mahsusi kwa wateja wa malipo kabla na baada.
Alisema lengo la kuzindua huduma za simu hiyo ni kuboresha mawasiliano na maisha ya Watanzania, kwani mawasiliano ya uhakika ni jambo muhimu la maendeleo.
Baadhi ya faida ya simu hiyo ni kuwa wateja binafsi na wafanyabiashara wenye anuani za mitandao, wanaweza kupata huduma za mitandao kama vile ya Yahoo, Hotmail, Gmail na mingineyo bila wasiwasi wowote na kwa muda wote.
"Kutokana na ubora wa huduma ya simu hiyo Watanzania kwa mara nyingine wanapata bidhaa bora kutoka Vodacom ambayo itawasaidia kuboresha maisha yao," alisema. Kwa wateja wa malipo kabla, wanaweza kujiunga na huduma za Blackberry kwa kutuma ujumbe mfupi wa maandishi yenye alama sahihi kwenda namba 123 na kuunganishwa na huduma ya kuzuru ya internet pamoja na huduma ya kutuma na kupokea barua pepe kwa muda wa siku kadhaa kabla ya kujiunga tena.
Mteja anaweza kuandika Blackberry1 kama anataka kutumia huduma ya internet kwa siku 30 kwa sh 36,000 au Blackberry3 kama anataka kutumia huduma ya internet kwa siku 90 kwa sh 99,000 na Blackberry6 kama anataka kutumia huduma hiyo kwa siku 180 kwa sh 180,000 na kisha kutuma namba 123.