Simu yako ya kwanza ilikuwa ipi?

Simu yako ya kwanza ilikuwa ipi?

Mimi nilianzia hiyo ya kwanza (NOKIA).

Dunia yaenda kasi kiteknolojia miaka kadhaa ijayo huenda zikawepo simu za audio tu yaani unaongea inatype yenyewe meseji(NI IDEA TU).
Kuna aap inafanya hio kazi kwenye android. Tatizo lake haijui Kibondei chetu, inaweza ikaandika tusi wakati wewe umetakia siku njema mtu!
 
Panasonic kadogo kama kiberit.ila nikaja tapeliwa na mahuni ya buguruni.
Mie niliwahi tapeliwa na kajamaa flan veta sim yangu nokia 8310, natumai kalishapigwa kibiriti kwa wizi kale!
 
Kuna nyingine hujaziweka mi simu yangu ya kwanza mwaka 1998 niliinunua Uganda
 
Usingeweka Siemens bichwa la Kambare nisingekuelewa. Lakini ukweli ni kuwa simu ulizoweka hapo nimetumia zote( namba mbili sina ukakika sana). Ungeweka na ile Siemens yenye mlio wa nyau A 55 nilikuwa naipenda sana niliita Siemens nyau
 
Jeneza linanikumbusha mbali sana. Niko ktk kipanya tiptop manzese mwizi anataka kuiba nikamkamata nmpiga ngumi kumbe mule walikuwa wawili wakataka kunichangia, abiria na konda wote kimya dah...simu niliitetea lakini nilijawa na hofu sana kuona sipati msaada
 
Mada yako imekosa head line ya kueleweka,,,
Simu yako ya kwanza kutumia ,,,
Alafu watoto wa juzi kaeni kando,,

Ungesema wahenga wenzangu weka hapa sim yako ya kwanza kutumia na ilikuwa mwaka gani?
Wahenga tungefunguka
Tumeanza na Erickson analog mwaka 1993 mobitel kabla ya ujio wa vodacom na celtel

Wanaosema wameanza na siemens c 25,; c 35,, A 36 motorola TID
Ni watoto wa juzi
Baada ya ujio wa vodacom na celtel..
 
SIEMENS 'Dore' nilikuwa naivaa shingoni basi mademu wanashoboka hatari enzi hizo,kweli kila kitu na zama zake
 
Back
Top Bottom