englibertm
JF-Expert Member
- May 1, 2009
- 9,252
- 6,209
[h=3][/h]
Siku hizi watu mna masmartphone
Nilianza na nokia ya tochi mwaka 2006 niliinunua 20000 kwa mtu tena hela yenyewe ilikua pocket money ya term ya kwanza form five
Kulikuwa na Nokia fulani hivi, ina antena ya kupandisha na kushusha kama redio mkulima halafu inameza ile SIM CARD yote kama ilivyo pasipo kubandua ile Micro Chip.
Kabla hujaanza kuongea inabidi ukifunue kifuniko fulani hivi ambacho kilikuwa kinafunika keypad...
Enzi hizo ili ujulikane una simu basi unaiweka kwenye mfuko wa ghorofani "mfuko wa shati", bonge la simu kama kilo 2 hivi yaani ni kuchana mifuko ya shati mwanzo mwisho.
Dah! Upo serious?Tritel wapi!???
Simu yangu ya kwanza ilikuwa aina ya Sony, 1992.