Simu yako ya kwanza iko wapi katika hizi??

Simu yako ya kwanza iko wapi katika hizi??

yangu ilikuwa simens c25 ,mwaka 2000, sh 99,000 nilicheza na line usikumzima ikablock, niambiwa nilazima kununua line nyingine,
 
Yangu ilikuwa nokia 3310 niliinunua mwaka 2003 kwa sh 100000. Na nilianza na line ya mobitel iliyoandikwa buzz line ambayo ndiyo nitumiayo mpaka sasa
 
Yangu ilikuwa SonyEricson ya screen nyembamba - msg ukiandika neno refu kama "HUNGUMALWA", inabidi maneno mengine yakatike, unascrow mbele/nyuma, ukubwa ka mche wa sabuni hivi, nakumbuka nilinunua kwenye promotion za Celtel elfu80...
:focus:
 
Kulikuwa na Nokia fulani hivi, ina antena ya kupandisha na kushusha kama redio mkulima halafu inameza ile SIM CARD yote kama ilivyo pasipo kubandua ile Micro Chip.
Kabla hujaanza kuongea inabidi ukifunue kifuniko fulani hivi ambacho kilikuwa kinafunika keypad...
Enzi hizo ili ujulikane una simu basi unaiweka kwenye mfuko wa ghorofani "mfuko wa shati", bonge la simu kama kilo 2 hivi yaani ni kuchana mifuko ya shati mwanzo mwisho.

dohhh...
 
nilianza na SIEMENS S 10-active ,nilikuwa TRITEL .tatizo naishi nje ya city centre nikifika Buguruni mtandao unapotea.ilikuwa 1997 July.
 
simu yangu ya kwanza ilikuwa motorola ya kufunua na aria ya kuchomoa,hivyo ilikuwa 1998 mwanzoni,niliinunua kwa mtu kwa sh 50.000,ilikuwa na battery nene kama jiwe

Simu hizo ziliitwa Motorola Micro Tac Pro na Micro Tac Duo. Zilitofautiana kidogo Micro Tac Duo ilikuwa ikihifadhi namba bila majina na Pro ilihifadhi namba na jina pia ila ikiita ilionesha neno call tu. Zilikuwa bni analogue.
 
Simu yangu ya kwanza ilikuwa Sony Erickson mwanzoni wa mwaka 2000, ilikuwa na taa fulani upande wa juu kulia ikiblink kuonesha chaji ipo full. Ngoma ilinipatia taabu sana hiyo maana mademu walikuwa wanaishobokea balaaa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom