Reuben Challe
JF-Expert Member
- Dec 10, 2021
- 2,761
- 5,039
Samsung S23 Ultra inatarajiwa kutoka Februari mwaka huu na pia tetesi ni kwamba simu hiyo itakuja na kioo flat kabisa tofauti na ilivyo kwa toleo lililopita (Galaxy S22 Ultra)
Samsung Galaxy S22 Ultra ilikuwa na curved screen yaani kioo chake kilikuwa curved na sio kila mtu atavutiwa na hii design.
Kumekuwa na malalamiko kuwa curved screen kwenye Samsung Galaxy S22 Ultra imepelekea ugumu katika kutumia S Pen kwenye display ya simu hiyo. Watumiaji wanasema kuwa wakati wa kutumia hiyo S Pen kwenye S22 Ultra basi peni ilitelezea kirahisi kuelekea kwenye edge za kioo cha simu.
Pia inasemekana kuwa vioo curved viko kwenye risk kubwa ya kupasuka simu itakapoanguka chini ukilinganisha na flat screens hivyo watumiaji wamelalamika na kudai warudishiwe flat screen. Kwenye muundo Samsung Galaxy S22 Ultra ina boxy design kama unavyoiona kwenye picha kwa hiyo hata S23 Ultra itakuwa na boxy design hivyohivyo tena hiyo itakuwa ni zaidi.
Vioo curved pia vina advantage zake mojawapo ni kwamba zinasaidia kuboresha muonekano wa display kwa sababu simu inakuwa haina bezel kabisa.
Kitu kilichonivutia kwenye Samsung Galaxy S22 Ultra ni kwamba S Pen iko built-in kwenye simu yaani ukinunua unaikuta.
Hii ni tofauti na kampuni kama Xiaomi ambao wao smart pen zao huwa zinauzwa kivyake, huzikuti kwenye boksi la simu.
Pia siku hizi tumeona namna simu zenye curved display zilivyotrend hadi makampuni makubwa tofauti na Samsung yanatoa flagship zenye curved displays. Binafsi navutiwa na simu zenye curved displays kwa sababu appearance inakuwa kali sana..
Mfano wa simu za makampuni mengine makubwa ambazo zina curved displays ni
Google Pixel 7 Pro
Xiaomi 13 Pro
Oppo Find X5 Pro
Motorola Edge 30 Ultra
Vivo X90 Pro Plus
Acha mwaka uendelee, naona soon Samsung atakuja kutoa best phone in the world kwa muda kisha Xiaomi naye atatoa Xiaomi 13S Ultra na atamfunika Samsung naye iPhone atafanya hivyohivyo halafu mwaka utaisha