Simpendi Guardiola na mimi siyo shabiki wa man city ila nawaombea kwa Mungu washinde

Machame Juu

JF-Expert Member
Jul 25, 2013
1,510
3,332
Katika historia ya Uefa champion's league mechi mbili tofauti ambazo zilivunja mioyo ya watu ni fainali 1999 Manchester united vs Bayern na nusu fainali mwaka jana 2022 Man City vs Real Madrid.

Ilivunja sana mioyo ya mashabiki wa Man City walipokuwa na uhakika kabisa wanaenda fainali kukutana na Liverpool lakini dakika za mwisho ndoto zao zika baada ya Real Madrid kuvuka hatua hiyo.

Licha ya Pep Guardiola kuwa mbaguzi namuombea kwa mungu timu yake anayoifundisha ishinde mechi yake ya leo na marudio iingie fainali na kubeba kombe. Nitafurahi sana.

Pia msimu ujao UCl naiombea PSG ichukue.

Pep anastahili hili kombe licha ya ubaguzi wake.
 
JOSEP "PEP" GUARDIOLA Hajawahi kummbagua mchezaji yoyote na pep sio mbaguzi...
anasimamia misimamo yake.
Mkuu Yahya Toure na Samuel Etoo wameweka wazi kabisa. Kumbuka hao wanamjua vizuri huyu mkatalan.

Hawa wachezaj wameondoka man city siyo kwa hiari yao. Vincent Kampany, Sterling, jesus, ferdandinho yahya toure

Kina zichenko Auguero etc wameondoka kwa hiari.
 
Mkuu Yahya Toure na Samuel Etoo wameweka wazi kabisa. Kumbuka hao wanamjua vizuri huyu mkatalan.

Hawa wachezaj wameondoka man city siyo kwa hiari yao. Vincent Kampany, Sterling, jesus, ferdandinho yahya toure

Kina zichenko Auguero etc wameondoka kwa hiari.

Kampany + Ndinho ni wastaafu, Sterling kiwango kilishuka mno na bado alipendwa na alikuwa regular starter, kumbuka fainali Uefa dhidi ya Chelsea hakuna mtu alitegemea Sterling angeanza ile mechi, matokeo yake kila mtu anajua,
Jesus G watu walifika bei, labda kwa Yaya.
 
Guardiola sio mbaguzi timu yake mbona ina weusi akina Akanji na Walker

Lakini kumbuka Abidal na Henry kipindi yupo Barca
 
Back
Top Bottom