Pep Guardiola ndio Kocha Bora kwa sasa Duniani

Nuoxian

Senior Member
Mar 15, 2020
169
237
Baada ya Arsenal kuchezea kichapo cha goli moja kwa bila dhidi ya Nottingham forest ni rasmi ubingwa wa ligi kuu uingereza msimu wa 2022/2023 unakwenda kwa manchester city ambaye anajumla ya point 85 huku anaemfuata Arsenal akiwa na point 81 na amebakiwa na mchezo mmoja mkononi ili kumaliza ligi wakati man city yeye akibakiza michezo miwili.

Ubingwa huu aliochukuwa man city chini ya kocha Pep Guardiola utakuwa ni ubingwa wao wa tatu mfululizo kuchukua chini na Kocha Pep Guardiola akifanya ivyo msimu wa 2019/2020, 2021/2022, 2022/ 2023 Wakati huo huo man city bado yupo kwenye mbio za kugombania makombe mengine fainali kombe la FA Ambayo atamenyana na Manchester United, fainali ya Uefa champion league dhidi ya Inter Milan, Kiufupi Guardiola ameshindikanika.

Licha ya makombe anayozidi kuyakusanya katika club mbalimbali pia guardiola ni kocha anayesifika kwa kufundisha mpira unaovutia kwa watazamaji mpira wa pasi nyingi, ikumbuke ile Barcelona ya akina Iniesta, Xavi na Lionel Messi, ilikuwa ni hatari mpaka Furgeson anatetemeka mikono . Kumbuka jinsi alivyoweza kuibadilisha Beyern Munich kutoka kwenye piga tukimbizane mpaka mpira wa pasi nyingi.

Haya ni baadhi ya makombe makubwa aliyowahi kuyachukua Mtaalam Pep Guardiola.

1. Uefa champion league..... ×2
2. Uefa Supercup....×3
3. Spanish (Laliga)......×3
4. England premier league.......×5
5. Bundersliga..........×3
6. Fifa club world cup......×3

images.jpg
 
Budget ya clubs anazofundisha huwa unaipitia? Ji kweli ni kocha bora sana, ila nae anakuwa na budget kubwa sana. Hata jana Mourinho alisema, una bench lenye 200m, wakati huo upo na quality ya hali ya juu ndani ya uwanja. Huwezi kulinganisha na hawa wanaopewa limited budget.
 
Budget ya clubs anazofundisha huwa unaipitia? Ji kweli ni kocha bora sana, ila nae anakuwa na budget kubwa sana. Hata jana Mourinho alisema, una bench lenye 200m, wakati huo upo na quality ya hali ya juu ndani ya uwanja. Huwezi kulinganisha na hawa wanaopewa limited budget.
Ishu sio Budget sababu zipo timu nyingi zilizotumia fedha nyingi zzaidi ya manchester city lkn bado hazifanyi vizuri, mfano kuna msimu manchester united alitumia pesa nyingi kusajili akina Magure, Sancho nk lkn wako wapi alikazalika chelsea, Nottingham forest
 
Back
Top Bottom