Simbachawene: Kupata kitambulisho cha NIDA siyo mwarobaini wa kutokuulizwa uraia wako

Kichuchunge

JF-Expert Member
Dec 2, 2020
338
891
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene ameeleza kuwa kuwa na kitambulisho cha Utaifa (NIDA), hakuhalalishi mtu kuwa ni Raia wa Tanzania.

Pia soma > Mbunge :Wasiojua vema mashairi ya wimbo wa Taifa na Kiswahili wanaambiwa siyo raia wa Tanzania

Simbachawene ameeleza hayo leo Mei 4, Bungeni jijini Dodoma ambapo amesema kuwa Uraia wa Tanzania una Sheria yake ya Uraia na una mchakato wake hivyo kitambulisho hicho ni kwa ajili ya kuwatambua tu hutolewa hata kwa Wakimbizi na hata kwa Wahamiaji wakazi.

“Kwa sasa tunadhani pengine tukipata Vitambulisho vya Taifa ndio tumepata Uraia wa Tanzania, Uraia wa Tanzania una Sheria yake ya Uraia na una mchakato wake, kitambulisho hiki ni kuwatambua tu na vitambulisho hivi vinatolewa hata kwa Wakimbizi, vinatolewa hata kwa Wahamiaji wakazi,” amesema Simbachawene.

Simbachawene amesema mtu kupata kitambulisho hicho sio mwarobaini wa kutokuulizwa na iwapo itagundulika kuwa mtu sio raia basi atanyang’anywa kitambulisho hicho.

“Ukipata kitambulisho hiki sio mwarobaini kwamba wewe umeshamaliza sasa hutaulizwa hapana, utaulizwa na utanyang’anywa hicho kitambulisho kama tukigundua wewe sio Raia wa Tanzania” amesema Simbachawene.

1620134110903.png

Simbachawene anataka kusema nini in a nutshell?

Kwamba hizi "CITIZEN IDENTIFICATION CARDs" sasa zinatolewa mpaka kwa wahamiaji haramu kwa sababu Wizara yake imejaa watu wazembe, wasiojari na wala rushwa wakubwa kiasi cha kutoa vitambulisho kihohela?
 
Tanzania chini ya ccm kamwe haiwezi kufanikisha jambo lolote la kimaendeleo.
 
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene ameeleza kuwa kuwa na kitambulisho cha Utaifa (NIDA), hakuhalalishi mtu kuwa ni Raia wa Tanzania.

Simbachawene ameeleza hayo leo Mei 4, Bungeni jijini Dodoma ambapo amesema kuwa Uraia wa Tanzania una Sheria yake ya Uraia na una mchakato wake hivyo kitambulisho hicho ni kwa ajili ya kuwatambua tu hutolewa hata kwa Wakimbizi na hata kwa Wahamiaji wakazi.

“Kwa sasa tunadhani pengine tukipata Vitambulisho vya Taifa ndio tumepata Uraia wa Tanzania, Uraia wa Tanzania una Sheria yake ya Uraia na una mchakato wake, kitambulisho hiki ni kuwatambua tu na vitambulisho hivi vinatolewa hata kwa Wakimbizi, vinatolewa hata kwa Wahamiaji wakazi,” amesema Simbachawene.

Simbachawene amesema mtu kupata kitambulisho hicho sio mwarobaini wa kutokuulizwa na iwapo itagundulika kuwa mtu sio raia basi atanyang’anywa kitambulisho hicho.

“Ukipata kitambulisho hiki sio mwarobaini kwamba wewe umeshamaliza sasa hutaulizwa hapana, utaulizwa na utanyang’anywa hicho kitambulisho kama tukigundua wewe sio Raia wa Tanzania” amesema Simbachawene.
Mtu asikufananishe na Mgogo. Yaani majibu yake, hayatofautiani na majibu ya Ndugai. Hawa jamaa walizowea kukaa barbarani kuomba. Sio kupewa nafasi za utawala.
 
Basi visitishwe kwasababu vinafuja pesa zetu za sis walipa kodi
Waziri anamaanisha kuna wazamiaji ambao wanaweza kuwahonga wafanyakazi wa NIDA ambao sio waaminifu na kuwapa hivyo vitambulisho! Kwa hiyo ikigundulika Kama ulifanya udanganyifu utanyanganywa kitambulisho na hataua za kisheria dhidi yako zitachukuliwa pamoja na hao waliokupa hicho kitambulisho nao watawajibika!!
 
Simbachawene anataka kusema nini in a nutshell?

Kwamba hizi "CITIZEN IDENTIFICATION CARDs" sasa zinatolewa mpaka kwa wahamiaji haramu kwa sababu Wizara yake imejaa watu wazembe, wasiojari na wala rushwa wakubwa kiasi cha kutoa vitambulisho kihohela?
Wala rushwa na Wazembe wapo kila sector! Na ndiyo wamesababisha Jembe letu kuondoka mapema kwa ukaidi wao!!
 
Kauli ya kipumbavu kabisa kutoka kwa mtu kama waziri wa mambo ya ndani. Sasa faida kitambulisho nini na gharama zote hizi kutengeneza vitambulisho fake? nchi zote duniani wanatoa vitambulisho vya uraia na kuna vya wageni na vinaandikwa wazi huyu mwananchi na huyu ni mkaaji tu. Nadhani wanaingiza siasa wanamwinda mtu huwezi kuweka sheria juu ya sheria. Sasa atuambie raia ni nani labda ni yeye tu na mgogo mwenzake Ndungai. jinga kubwa hili konda la bus.
 
National Identity Card si ndio NIDA
National ni Taifa
Kwa hivi NIDA ni kitambulisho cha Utaifa
Utaifa ni Uraia au
Nationality ni Utaifa
Citizenship ni Uraia
*** NIDA ilianzishwa kwa lengo gani tuanzie hapa
***Kuna Resident Permit ni Mkaaji ( wakimbizi wageni wahamiaji etc)

Wizara mnajichanganya wenyewe
Huwezi kuwa mkimbizi ukapewa NIDA
Mtoto aliyezaliwa ukimbizini anaweza kuwa NIDA (kama sheria za nchi zinatambua hili kuzaliwa ukimbizini sio lazima uwe na utaifa wa nchi husika)
 
Back
Top Bottom