Simbachawene: Kupata kitambulisho cha NIDA siyo mwarobaini wa kutokuulizwa uraia wako

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
103,781
2,000
Kwa maneno ya waziri maana yake suala la uraia wa mtu ni open ended question, hata uwe na aina gani ya ID muda wowote tunaweza kurudi tena kwenye swala la uraia.
Huyo akili zake na Ndugaye hazina tofauti
 
Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
103,781
2,000
Kwa nchi za wenzetu Simbachawene angepaswa kujiuzulu leo leo. Huo ni UPUMBAVU wa hali ya juu kwa kuwa Tanzania kabla ya vitambulisho vya NIDA ni sawa na Watanzania BAADA ya vitambulisho vya NIDA.

Ni upotevu wa Fedha za walipa Kodi wa Tanzania
Jiwe alikuwa anaweka watu wasiyo hitaji kutumia elimu na weledi ili wasimuhoji
 
E oxygen

JF-Expert Member
Feb 25, 2021
209
225
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene ameeleza kuwa kuwa na kitambulisho cha Utaifa (NIDA), hakuhalalishi mtu kuwa ni Raia wa Tanzania.

Pia soma > Mbunge :Wasiojua vema mashairi ya wimbo wa Taifa na Kiswahili wanaambiwa siyo raia wa Tanzania

Simbachawene ameeleza hayo leo Mei 4, Bungeni jijini Dodoma ambapo amesema kuwa Uraia wa Tanzania una Sheria yake ya Uraia na una mchakato wake hivyo kitambulisho hicho ni kwa ajili ya kuwatambua tu hutolewa hata kwa Wakimbizi na hata kwa Wahamiaji wakazi.

“Kwa sasa tunadhani pengine tukipata Vitambulisho vya Taifa ndio tumepata Uraia wa Tanzania, Uraia wa Tanzania una Sheria yake ya Uraia na una mchakato wake, kitambulisho hiki ni kuwatambua tu na vitambulisho hivi vinatolewa hata kwa Wakimbizi, vinatolewa hata kwa Wahamiaji wakazi,” amesema Simbachawene.

Simbachawene amesema mtu kupata kitambulisho hicho sio mwarobaini wa kutokuulizwa na iwapo itagundulika kuwa mtu sio raia basi atanyang’anywa kitambulisho hicho.

“Ukipata kitambulisho hiki sio mwarobaini kwamba wewe umeshamaliza sasa hutaulizwa hapana, utaulizwa na utanyang’anywa hicho kitambulisho kama tukigundua wewe sio Raia wa Tanzania” amesema Simbachawene.

Labda sawa lkn alikipataje?!!
 
Heavy Metal

JF-Expert Member
Feb 7, 2017
279
1,000
Point yake nini sasa hapa?! Kwamba mtu apewe kwanza halafu ataulizwa badae kuhusu uhalali wa uraia wake nchini?! Kwanini asiulizwe kwanza kabla ya kupewa icho kitambulisho?! Haoni ni upotevu wa pesa za serikali na kutokujipanga vizuri kwenye huo mchakato?!
 
OHA

Member
Aug 20, 2013
14
45
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene ameeleza kuwa kuwa na kitambulisho cha Utaifa (NIDA), hakuhalalishi mtu kuwa ni Raia wa Tanzania.

Pia soma > Mbunge :Wasiojua vema mashairi ya wimbo wa Taifa na Kiswahili wanaambiwa siyo raia wa Tanzania

Simbachawene ameeleza hayo leo Mei 4, Bungeni jijini Dodoma ambapo amesema kuwa Uraia wa Tanzania una Sheria yake ya Uraia na una mchakato wake hivyo kitambulisho hicho ni kwa ajili ya kuwatambua tu hutolewa hata kwa Wakimbizi na hata kwa Wahamiaji wakazi.

“Kwa sasa tunadhani pengine tukipata Vitambulisho vya Taifa ndio tumepata Uraia wa Tanzania, Uraia wa Tanzania una Sheria yake ya Uraia na una mchakato wake, kitambulisho hiki ni kuwatambua tu na vitambulisho hivi vinatolewa hata kwa Wakimbizi, vinatolewa hata kwa Wahamiaji wakazi,” amesema Simbachawene.

Simbachawene amesema mtu kupata kitambulisho hicho sio mwarobaini wa kutokuulizwa na iwapo itagundulika kuwa mtu sio raia basi atanyang’anywa kitambulisho hicho.

“Ukipata kitambulisho hiki sio mwarobaini kwamba wewe umeshamaliza sasa hutaulizwa hapana, utaulizwa na utanyang’anywa hicho kitambulisho kama tukigundua wewe sio Raia wa Tanzania” amesema Simbachawene.

Hii kama siyo kitambulisho serekali inachezea kori zetu
 
white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
5,175
2,000
National Identity Card si ndio NIDA
National ni Taifa
Kwa hivi NIDA ni kitambulisho cha Utaifa
Utaifa ni Uraia au
Nationality ni Utaifa
Citizenship ni Uraia
*** NIDA ilianzishwa kwa lengo gani tuanzie hapa
***Kuna Resident Permit ni Mkaaji ( wakimbizi wageni wahamiaji etc)

Wizara mnajichanganya wenyewe
Huwezi kuwa mkimbizi ukapewa NIDA
Mtoto aliyezaliwa ukimbizini anaweza kuwa NIDA (kama sheria za nchi zinatambua hili kuzaliwa ukimbizini sio lazima uwe na utaifa wa nchi husika)
Ki ukweli hivi vitambulisho vya NIDA, watu wengi tu ambao sio raia wa Tz, wanavyo na hii ni kutokana na utaratibu mbovu/rushwa.wakitaka hili zoezi lije liwe lenye manufaa waliyokusudia wangeanzisha utaratibu pale mtoto tu anapozaliwa kinaandaliwa na kupewa hapo hapo.sio haya mtu anakuwa mtu mzima ndio akifuatilie.
 
Jiwe la kudumu

JF-Expert Member
Aug 17, 2018
290
250
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene ameeleza kuwa kuwa na kitambulisho cha Utaifa (NIDA), hakuhalalishi mtu kuwa ni Raia wa Tanzania.

Pia soma > Mbunge :Wasiojua vema mashairi ya wimbo wa Taifa na Kiswahili wanaambiwa siyo raia wa Tanzania

Simbachawene ameeleza hayo leo Mei 4, Bungeni jijini Dodoma ambapo amesema kuwa Uraia wa Tanzania una Sheria yake ya Uraia na una mchakato wake hivyo kitambulisho hicho ni kwa ajili ya kuwatambua tu hutolewa hata kwa Wakimbizi na hata kwa Wahamiaji wakazi.

“Kwa sasa tunadhani pengine tukipata Vitambulisho vya Taifa ndio tumepata Uraia wa Tanzania, Uraia wa Tanzania una Sheria yake ya Uraia na una mchakato wake, kitambulisho hiki ni kuwatambua tu na vitambulisho hivi vinatolewa hata kwa Wakimbizi, vinatolewa hata kwa Wahamiaji wakazi,” amesema Simbachawene.

Simbachawene amesema mtu kupata kitambulisho hicho sio mwarobaini wa kutokuulizwa na iwapo itagundulika kuwa mtu sio raia basi atanyang’anywa kitambulisho hicho.

“Ukipata kitambulisho hiki sio mwarobaini kwamba wewe umeshamaliza sasa hutaulizwa hapana, utaulizwa na utanyang’anywa hicho kitambulisho kama tukigundua wewe sio Raia wa Tanzania” amesema Simbachawene.

Mbona Mussa Assad alishawaongolea watu sampuli hii siku nyingi kuwa vilaza wapo wengi🤣🤣
 
imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
27,993
2,000
Kwahiyo Kitambulisho cha Kupigia Kura ndicho kimachomtambulisha Mtanzania au na chenyewe Wanapewa hadi Wakimbizi?
 
NewOrder

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
1,503
2,000
Viongozi wasiojua Taifa linataka nini ndio waliojaa kwenye baraza la Mawaziri.

Kabisa mkuu. Anamalizia kwa kusema mtu atanyang’anywa ikigundulika sio raia!! Hapo hapo akisema vitambulisho vhivo vinatolewa kwa raia, wakimbizi na wakazi wahamiaji.

Yaani tunakuwaje na watu wa namna hii wakiongoza?? Hiki ni kitambulisho cha utaifa. Huo mchakato tofauti hata hausemi na unaishia kupewa utambulisho kinaitwaje hasemi pia!!
 
imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
27,993
2,000
Waziri anamaanisha kuna wazamiaji ambao wanaweza kuwahonga wafanyakazi wa NIDA ambao sio waaminifu na kuwapa hivyo vitambulisho! Kwa hiyo ikigundulika Kama ulifanya udanganyifu utanyanganywa kitambulisho na hataua za kisheria dhidi yako zitachukuliwa pamoja na hao waliokupa hicho kitambulisho nao watawajibika!!
Acha kuspin amesema Vitambulisho vya URAIA hutolewa kihalali hata kwa Wahamiaji wakazi na Wakimbizi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom