Simbachawene aagiza kukamatwa kwa Askari 5 wa Uwanja wa JNIA kwa uhalifu wa kusafirisha binadamu

HUYU WAZIRI NI KILAZA SANA. NI BORA UKAFE NA NJAA DUBAI KULIKO KUFA KIZEMBE BONGO.

FURSA ZOTE WAMEZIBA HAKUNA ANAYEPENDA KUJILIPUA HUKO UARABUNI.

NA SIO WOTE WANAOENDA UARABUNI WANATESWA HUO NI UONGO.

2016 PALE UBALOZI WA OMAN PALIKUWA PANASOMA KUNA WATANZANIA ZAIDI YA ELFU 4 WANAFANYA KAZI OMAN.

LEO HII HATA ELFU 10 WATAKUWA WAMEFIKA NA WOTE WANATUMA HELA NYUMBANI.
Na ukweli mwingine ambao tunajifanya hatuuoni ni kwamba, hawa ma-housegirl wananyanyaswa hata hapa kwao! Unyanyasaji unofanywa na baadhi ya Waarabu kule Arabuni unafanywa hata na baadhi ya Watanzania wenzetu waliopo Tanzania. Kuna Wasichana wengi tu wanachukuliwa mikoani na kupelekwa Dar kwa ahadi ya kufanya kazi za ndani lakini wakifika kule wanafanyishwa kazi ya ukahaba lakini tunajifanya hilo hatulioni!
 
Watanzania bwana, hivi mtu na akili zake timamu kabisa anaona ufahari gani kwenda kufanya kazi za uyaya Uarabuni? Hawa watanzania wakamatwe na kunyongwa tu, Uarabuni si sehemu ya kwenda kufanya kazi hata kidogo, waulizeni Wahindi wanaotumikishwa kule na kubakwa.
 
Waziri Simbachawene akiwa kwenye kikosi cha anga, alipata wasaha wa kuruka kwa helikopta kuzunguka sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam kwa takribani dakika 40 ambako mbali na kukipongeza kikosi hicho, alibainisha kuwa usalama kwa njia ya anga umeimarishwa na nchi ni salama.

SIasa katika ubora wake
 
Askari huwa wakipatikana wanakuwa wadogo hadi unawahurumia.. kuna mmoja alizinguana na dogo mmoja akamnasa vibao kwenye pub akaitisha na defender dogo akapelekwa... alivofika kaunta akaomba awasiliane na mzee wake wakamtupa ndani wanasemaga maagizo toka juu ilipigwa simu sasa toka jengo jeupe akapigiwa mkuu kabisa alitoka mkuku kwenda kumtoa jamaa aliemkamata kifupi alimuonea na kutumia ubabe tu.. jamaa alilia aisee kama mtoto na kumpigia magoti dogo akimuomba msamaha.. jamaa alipata ajali akadanja
 
Siku zote ugumu wa maisha huingiza watu matatani,Chawene wajali hao askari wako,hutosikia wakifanya maovu kama wafanyavyo.
Ni ushauri tu natoa, mimi kama raia wa nchi yangu Tz.
anajua vyema sana,ila anachofanya ni kile kile kama alichokifanya kangi.
 
Siku ungebahatika kufika chuo cha polisi na kujionea mafunzo wanayopewa,ungegundua tabia nyingine ya binaadamu(kubadilika).

chuo kinafundisha,mazingira ya kazi nayo yanatengeneza askari mwingine kabisa ambaye hajawahi kuhudhuria mafunzo.
 
Unakuta kamanda wa polisi mkoa anazungumzia moto ulioteketeza duka huku wataalamu wenyewe wakiwa hawapo na hata hajawapigia simu, hii ni nzuri.

*Waziri Simbachawene aliagiza Wakuu wa Polisi wa mikoa kutozungumzia masuala yahusuyo moto huku akiwataka askari wa kikosi hicho wanaopatikana kila mkoa kuwa wazungumzaji wakuu wa masuala hayo.
unaona hapa pia kakurupuka,hii ndio tatizo la siasa na taaluma za watu.

anashindwa kujua kwamba jukumu la kuutangazia uma hali ya usalama wa raia na mali zake ni la polisi nchini,si taasisi nyingine.

kwahiyo kutokumwona askari wa zimamoto nyuma ya rpc haina maana taarifa rpc kaziokota kwenye njiapanda,zimeletwa mezani kwake na watu wa zimamoto wamepeleka maelezo.
 
Na ukweli mwingine ambao tunajifanya hatuuoni ni kwamba, hawa ma-housegirl wananyanyaswa hata hapa kwao! Unyanyasaji unofanywa na baadhi ya Waarabu kule Arabuni unafanywa hata na baadhi ya Watanzania wenzetu waliopo Tanzania. Kuna Wasichana wengi tu wanachukuliwa mikoani na kupelekwa Dar kwa ahadi ya kufanya kazi za ndani lakini wakifika kule wanafanyishwa kazi ya ukahaba lakini tunajifanya hilo hatulioni!
Kweli mkuu

Sent from my Infinix Zero 3 using JamiiForums mobile app
 
MH WAZIRI CONGS KWANZA AWALI YA YOTE UNGEDILI NA HAWA KWANZA
HII NDIO CHANNEL NZIMA YA JNIA TO UAE.DUBAI
1;OFISI YA WIZARA YA KAZI
HAWA VIIANA AWAJIKWABAHATI MBAYA WANADOCS ZA WIZARA YA KAZI

2;TOA WALE VIIJANA WALIOOPO WA WIZARA YA KAZI WALEE N VINUKA RUSHWA HAWANAKAZI PALE PEMBENI YA IMMIGRATION

3: BINAFSI NINGEHISHA BOSS WA IMMIGRATION
HAWAVIJANA HUINGIZWA CHUMBA CHA MABOSI KULIA CHA IMMIGRATION NA KAZI INAANZIA HAPO

4;WANAOFWATA N BADILISHA VIJANA WA USALAMA MARA KWA MARA WENGI WMEZOEA WANAJISAHAU
HAO WATOTO WAKIPANDA JUU KUSUBIRI NDEGE WANAHITIMISHA KUTOAPESA ZAO KWA POLISI NA...

HII CHA NEL N NDEFU MH G.S.CHAWENE
KAMPUNI ZINAZOSAFIRISHA NENDA PALE WIZARA A KAZI ZINAJULIKANA ZINGINE ZA WAH WALIOPITA
UKIFA NIIKIWA KUWABANA HAWA HATA FUKUZA FUKUZA HAITOKUWEPO MH WAZIRI CHANNEL N NDEFU SANA

HAO POLISI N BAADHI TU WAKOWENGI PALE .....
KILALAKHERI
 
Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene ameagiza kukamatwa kwa askari watano katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kutokana na kushiriki matukio ya kihalifu.

Agizo hilo linakuja siku chache baada ya kufukuzwa kazi kwa askari wanne wa jeshi hilo kutokana na ukiukwaji wa maadili ya Polisi kwa kushiriki matukio ya kiuhalifu ikiwamo kuomba rushwa na mwengine kuhujumu miundombinu ya umeme ya Shirika la Umeme Tanzania(Tanesco).

Waziri huyo ambaye anaendelea na ziara yake ya siku tatu kukagua shughuli mbalimbali za jeshi hilo, jana baada ya kutembelea Kikosi cha anga cha jeshi hilo, alifanya ziara JNIA ambako alitumia takribani saa moja kuzungumza na maofisa wa polisi uwanjani hapo na kisha kutembelea sehemu mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari uwanjani hapo, Waziri Simbachawene alisema kuwa askari hao watano wameunda mtandao wao kwa ajili ya kusaidia usafirishaji wa vijana wa kike na kiume kwenda nchi za kiarabu kufanya kazi za ndani.

Alisema serikali imeshapiga marufuku usafirishwaji wa watanzania kwenda kufanya kazi za ndani kwenye nchi hizo na kuwa askari na maofisa uhamiaji nchi nzima wanalo jukumu la kuhakikisha hakuna mtu anayekwenda kufanya kazi za ndani kwenye nchi hizo.

Alibainisha kuwa askari hao wamekuwa wakishiriki kuhakikisha mawakala wanafanikiwa kusafirisha Watanzania kwenda katika nchi hizo.

Pia alisema askari hao wamekuwa wakiwasumbua wageni wanaosafiri kutumia uwanja huo kwa kuwaomba fedha huku wakitishia kuwabambikia kesi mbalimbali.

Kwa mujibu wa taarifa za kiitelijensia ambazo waziri huyo alisema anazo, askari hao wamekuwa wakishirikiana na wabeba mizigo ya abiria uwanjani hapo.

Alisema wabeba mizigo hiyo wakifika kwenye eneo la magari ambapo kamera zimekuwa hazioneshi, askari hutokea na kutoa vitisho hivyo kwa wageni wakitaka kupewa fedha.

Alisema,"kwa taarifa nilizonazo na ambazo kwa muda wa mazungumzo yangu hapa uwanjani leo nimejiridhisha kuhusiana na uwepo wa matukio yasiyokuwa ya kiuungwana yanayoendelea mahala hapa, hivyo kwanza nimeagiza wakamatwe askari hao kwa mahojiano zaidi."

Pia Waziri huyo alisema kuwa utawekwa mfumo uwanjani hapo kuhakikisha kila anayetoka nje ya nchi anakaguliwa kwa ufanisi kwa kila hatua anatakiwa kukaguliwa kuliko hali ilivyo sasa ambapo askari anaweza kuamua nani wa kumkagua na nani asikaguliwe.

Alisema hali hiyo inashawishi mazingira ya rushwa . Alikemea polisi kuwawekwa muda mrefu abiria baada ya kuwakagua na kuwa askari atakayebainika kuendelea kufanya hivyo atachukuliwa hatua.

Waziri Simbachawene akiwa kwenye kikosi cha anga, alipata wasaha wa kuruka kwa helikopta kuzunguka sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam kwa takribani dakika 40 ambako mbali na kukipongeza kikosi hicho, alibainisha kuwa usalama kwa njia ya anga umeimarishwa na nchi ni salama.

Akiwa kwenye kikosi cha zimamoto mkoa wa Ilala, Waziri Simbachawene aliagiza Wakuu wa Polisi wa mikoa kutozungumzia masuala yahusuyo moto huku akiwataka askari wa kikosi hicho wanaopatikana kila mkoa kuwa wazungumzaji wakuu wa masuala hayo.

Alisema hiyo inatokana na utaalamu walionao askari wa zimamoto na kuwa kama wakitoa taarifa inakuwa na ufanisi na yenye utaalamu.

Alitaka uwepo ushirikiano mzuri kati ya Tanesco na Zimamoto hasa katika ukataji wa umeme kwa haraka pindi wakitakiwa kufanya hivyo na kikosi hicho.

Pia alikemea wanaopiga simu za kuhitaji msaada wa gari za kuzima moto lakini kunakuwa hakuna tukio la moto kwenye maeneo yao.

Akizungumzia kuhusu hali ya wakimbizi nchini, waziri alibainisha kuwa kwa sasa nchini kuna wakimbizi 275,000 na kuwa serikali inaendelea na mazungumzo na Shirika la Umoja wa Mataifa Linalohudumia Wakimbizi(UNHCR) kuhusu njia bora ya kuwarejesha majumbani wakimbizi wenye kustahili Kazi neema,
 
Kwanini vijana kwenda kusaka ajira nchi za kiarabu kuwe ni kosa Hali hatuwezi, tumeshindwa wapa ajira nchini.
Pili binadamu sio mbuzi umuwekee fenci asiiondoke,utamzuia hapa ataondokea nchi jirani na kwenda atakapo.
Muhimu ni kuwatengenezea mazingira wezeshi bora ya wao kwenda kufanya kazi salama.
 
Bado sijamwelewa waziri wangu. Ina maana hao askari ndio wanatoa passports na viza kwa hao wasafiri, au?! Tuseme mtu kenda zake uhamiaji, kapata passport, kisha anaenda ubalozi, nako anapata viza. Kwahiyo mtu kama huyo akifika pale airport hao polisi walitakiwa kumrudisha kwa sababu anaonekana anaenda kwenye hizo nchi, au?!
Labda waweke utaratibu kwanza waanzie uwanjani kupata ruhusa kwanza Kisha ndo wakakate pasipoti na viza kuliko kupoteza pesa kote huko then unazuiwa
 
Kama tumeshindwa hata kuwatengenezea mazingira ya ajira vijana wetu wa export hata nyanya nje,Basi tuexport madada wa kazi wakaleta pesa zisaidie familia zao, mshahara wa laki nane kwa mwezi mara miezi 3 akituma kijijini kwake wanajenga nyumba kubwa tu ya Bati huku akisomesha ndugu zake.
 
Back
Top Bottom