Papy ndombe
JF-Expert Member
- Oct 24, 2020
- 3,762
- 4,516
Fact ya kunyanyaswa sio kigezo Cha kuzuia watu kutafuta maisha, Kama ni hivyo tuanze kuzuia watokao vijijini wanaokuja mijini kunyanyaswa na wake zetu hawa wasiojitambua na kuheshimu utu wa mtu.Na ukweli mwingine ambao tunajifanya hatuuoni ni kwamba, hawa ma-housegirl wananyanyaswa hata hapa kwao! Unyanyasaji unofanywa na baadhi ya Waarabu kule Arabuni unafanywa hata na baadhi ya Watanzania wenzetu waliopo Tanzania. Kuna Wasichana wengi tu wanachukuliwa mikoani na kupelekwa Dar kwa ahadi ya kufanya kazi za ndani lakini wakifika kule wanafanyishwa kazi ya ukahaba lakini tunajifanya hilo hatulioni!
Tumeshuhudia wakiwatukana,
Kuwapiga
Kuwabagua,
Kuwazulumu mishahara
Kuwanyima haki za ibada
Kuwaumiza kisaikolojia stress zote za familia ubebeshwa wao.
Mimi naona sisi waswahili ndo tunawanyanyasa Sana madada wa Kazi kuliko hata huko arabuni.