Dah
Mkuu umenikumbusha mbali sana. Story yako ina ukweli. Mwishoni mwa 1990s kabla daraja halijakamilika nilivuka hapo Rufiji river nikitokea Dar nikiwa na lika chini ya 16. Lengo lililkuwa kwenda Nangurukuru.
Tulifika hapo jioni kivuko hakifanyi kazi na ilikuwa lazima asubuhi niwe Nangurukuru. Ilibidi tupande mtumbwi wa kienyeji. Ilikuwa hatari sana kuvuka, kwani mamba unawaona na kuogerea sijui. Halafu mto upo speed kwani ilikuwa masika. Chakushangaza captain alikuwa haogopi kitu ndio kwanza alikuwa ananipa moyo kuwa tutafika ngambo salama.
Tulipovuka tu, kulia kulikuwa na guest house na kulikuwa na watu wengi balaa. Ufuska uliokuwepo pale Mungu tu ndio anajua. Sasa uwani kwa ile Guest kulikuwa na Mabafu mawili ambapo ukiwa bafu moja aliyekuwa anaoga bafu lingine unamwona. Sasa akaingia mdada wa makamo kuoga nikaanza kumchungulia mara akaniona. Kilichotokea hapo ni siri, lakini mbeya mmoja akaenda kumtonya mume. ile natoka tu mume huyo kafika na kuanza kumshtumu mke kwamba alikuwa na mtu. cha ajabu akunishtukia kutokana na kimo na lika langu. Ila sikufanya zambi zaidi ya kuchungulia na kubalishana maoni.
Kesho yake asubuhi tukapanda baiskeli kwenda Nangurukuru, baada ya ya dk 10 tunakutana na simba ana vitoto. Mzee akanambia nisikimbie akitusogera nichune. bahati nzuri yule simba alituangalia baadaye akapotelea porini. Nikaanza kuhisi kuwa ile zambi ya jana usiku ndio imesababisha kukutana na Simba. Mzee akaniambia kukutana au kuliwa na simba eneo hilo siyo story. Hakika nilipata uwoga ambao hadi leo siwezi kusahau.
Kimsingi ni kweli Bondo la Rufiji hasa upende wa lindi ilikuwa hatari wengi wameliwa sana na simba.
Naomba Mungu wa mbinguni mwenye huruma anisamehe na kunifutia zambi ile.