Wanabodi, niko mahali, naangalia mechi, SS!, kusema ukweli, hizo kamera zinazotumika hapo, ziangalieni hivyo hivyo tuu, Tanzania hatuna hata kituo kimo cha TV chenye hata nusu ya quality ya kamera hizo!.
By the way , nimemuona mtangazaji binti kidoti wa SS na Florian Kaijage, kiukweli wako juu!.
Hapa nilipo, maeneo fulani ukanda wa Gaza (ya bongo), baada ya Simba kufanya mambo, ukumbi mzima ulishangilia as if wote hapa ni washabiki wa Simba!. Katikati ya ushangiliaji, kuna mwendawazimu mmoja akachomekea "nani CCM?", ukumbi wote kimya!, jee inawezekana Yanga ni CCM halafu Simba ni ..., no wonder kwa nini naipenda Simba!.
P.