Simba vs Yanga: Oct 03, 2012

Simba vs Yanga: Oct 03, 2012

alafu ikumbukwe kwamba: Bahanuzi style yake ya kucheza mpira ni kukaa nyuma ya Beki akisubiri atanguliziwe mpira; kwa wachezaji wazoefu kama wa Simba style hiyo ilikua ngumu kuwa applicable na ndo maana muda wote alionekana anaotea.
 
Ball possesion haiwezi kuwa hiyo mkuu waambie hao Kiss FM wataje ya ukweli, hao marefa utawasingizia tu kwamba waliibeba Simba, sehemu moja tu ambayo refa alitubeba nayo ni kutompa red Haruna hata jukwaani tulipokuwa tumekaa tuliona hilo na tukasema hapo refa katubeba, lakini ile njano aliyopewa Edward, Cannavaro alisukuma na ingekuwa penati, Cannavaro kamchezea rafu nyingi sana Sunzu mara zote wakati wanawania mpira alikuwa anamsukuma na mwisho refa alikosa uvumilivu akampa red, Mwasika naye alimuchezea rafu Kazimoto lakini mbali na kutopewa kadi hata faulo tu haikupigwa, siwezi kumlaumu refa labda alikuwa mbali na matukio au makosa ya kibinadamu tu lakini huwezi kusema kwamba aliibeba Simba. Wale wasaidizi kama ulikuwa makini kuangalia utaona Bahanuzi alikuwa anabaki peke yake akisubiri kupitishiwa kwa nini asiwe offside na ulitaka mwamuzi msaidizi amwache.

kuhusu kutawala kama dakika 10 za mwisho ilichangiwa na kutoka kwa Mkude na kuingia na kuingia Haruna Moshi, kiungo kilipoteana na baada ya rafu mbaya ambayo Haruna aliifanya nayo mchezoni, kama binadamu isingekuwa rahisi afanye ile faulo halafu aendelee kucheza vizuri hata ukiangalia picha vizuri amekita ule mkuu lakini usoni anaonekana kuumia kama vile yeye ndo alikanyagwa kwa hiyo hata yeye hakuifurahia hiyo faulo ilimtoa mchezoni kiukweli.

La ball possesion siyo la kwangu Mkuu,mi nimenukuu tu kuota kituo cha radio na television ambacho kilionyesha mchezo huo jana,wame'compute vipi wanajua wenyewe...lkn coming back to Mwamuzi na Msaidizi wake sikatai inawezekana ikawa kweli kuna maamuzi yaliyokuwa yanai'favour Yanga lkn hayo hayawezi kuwa zaidi ya yale yaliyokuwa yanai'favour Simba,nitakuambia machache tu:-
Kaseja alikuwa anapoteza muda sana from 1st half baada ya Simba kupata goli la kuongoza lkn hakuchukua hatua yeyote zaidi ya kumuonya kwa mdomo kama mara 3 hv,angalia offsides walizokuwa wanaamua...unajua Bahanuzi si kweli kwamba huwa anakaa nyuma ya mabeki hapana Bahanuzi huwa anasimama mbele ya mabeki na inapopigwa pasi ya kutanguliza ndo huwa anachomoka kuwapita mabeki na kuipokea,matukio kama ma'2 ma'3 hv yalikuwa ya aina hiyo lkn wale Mabwege(am sorry to identify them in this way) walikuwa wanaona offsides..kuhusu card ya Edo angalia vizuri ni kweli wakati anamchomoka Canavaro alifanya kama kumvuta hivi kidogo akajishtukia akamwachia na kunyoosha mikono na Dogo akaendelea na move mbele kidogo alivyoona ameshaingia kwenye penalt area ndo akajiangusha ndo maana ikaonekana dhahiri amejiangusha,angekuwa smart sana wkt alipovutwa kidogo angejiachia palepale lkn mwenyewe dizaini aliona haina faida ksbb ilikuwa nje kidogo ya penalt area
 
Mi naona wewe ndio unaongea kishabiki zaidi........Kimahaba zaidi......

Ball possession ni Yanga 52% na Simba 48% yet unasema Yanga walikuwa wanacheza physical zaidi.....Mabeki wa Simba walikuwa wanacheza offside trick ndio maana washambuliaji wa Yanga wameotea zaidi ya mara 10......Ona sasa unaaza na hadithi za 'angekuwepo Okwi angeisumbua beki ya Yanga'......Football ni nothing but a game of chance, ndio maana unaona hata baada ya Simon Msuva kutolewa kwa kadi nyekundu Yanga waliendelea kuwashambulia Simba, hii ni kwa sababu walikuwa wakitengeneza chance nyingi hasa eneo la kiungo ambalo liliimarika baada ya Frank Domayo kuingia....Simbaa mpira wamecheza dakika 30 za mwanzo baada ya hapo game ilibalance na dakika 10 za mwisho wa kipindi cha kwanza Yanga waliutawala mchezo.....Hata baada ya Kavumbangu kuingia Yanga waliendelea kuutawala mchezo kwa kutengeneza nafasi za kushambulia ambazo zilikuwa zikiishia kuwa offside kutokana na mbinu iliyotumiwa na beki ya Simba.....

All in all mchezo wa leo ulikuwa mzuri, timu zote mbili zimecheza vizuri na Yanga nawasifu zaidi kwani hata baada ya Simon Msuva kutolewa kwa kadi nyekundu hawakutetereka kwa kulinda goli/kufunga tela badala yake waliendelea kushambulia..............

Nini Tanzania, Buhanuzi ni the best striker in East Afrika.....The Top scorer in 2012 CECAFA Kagame Cup

Huyo best striker wa East Africa ameshindwa kuonesha makali yake kwa Mtibwa, mmekula tatu bila na yeye akiwemo. Mmeshindwa kuwafunga Prisons, mmeshindwa kuwafunga Simba jana wakiwa wamefixture Yosso.

I must admit defence ya Yanga inamuogopa Okwi kuliko unavyofikiri. Mchezaji yeyote ambaye ana go past defenders ni hatari usisikie. Waulize mabeki wa Yanga kwenye tano bila watakuambia Okwi ni nani, wewe huwezi kujua kwa sababu hukuwa unakabiliana nae.

Hebu jaribu kufikiria kabla ya game ya Simba na Yanga Simba alikuwa na record nzuri sana ya kutokufungwa hata mechi moja and yet Yanga ndio waliokuwa na confidence zaidi ya kushinda, the reason is simple, mtu wanaemhofia hakuwepo. Kumkaba Bahamuzi ni rahisi sana cos anasubiri apigiwe mpira na mabeki akimbie, it is not the case with Okwi.
 
Back
Top Bottom