Simba Sports Club (Wekundu wa Msimbazi) | Special thread

Simba SC is a Tanzanian football club based in Dar es Salaam. Their home games are played at two stadiums Uhuru Stadium and National Stadium. Simba SC is one of two biggest football clubs in Tanzania, their archrivals being the Young Africans. The club had several names during its history, when it was founded in 1936 it was called Queens, then changed to Eagles, Dar Sunderland and later, in 1971 changed to its actual name, Simba (that means Lion in Swahili).
Simba is the biggest also the most titled club in Tanzania.

The highest level of success that Simba SC achieved was getting to the final of the CAF Cup in 1993 where they lost to Stella Abidjan of Ivory Coast. It was the highest achievement on continental competitions reached by any Tanzanian team. One of the most memorable years for the club was 2003 when it knocked off the then reigning champions Egyptian giants Zamalek on its way to qualify for the group stages of the CAF Champions League. In the first round of that year's competition, Simba SC eliminated Santos of South Africa.

Nicknames: Msimbazi street boys ( Wekundu wa Msimbazi)

Simba Sports Club Official Website: www.simba.co.tz


Simba Sports Club Trophies:
Tanzanian Premier League: 20
1965, 1966 (as Sunderland)
1972, 1973, 1976, 1977, 1978, 1979, 1980, 1993, 1994, 1995, 2001, 2002, 2004, 2007, 2009/2010, 2011/12, 2017/18, 2018/19

Tanzanian Cup: 3
1984, 1995, 2000

Tanzanian Tusker Cup: 5
2001, 2002, 2003, 2005
2005 in Kenya

CAF Cup:
Finalist : 1993

CECAFA Clubs Cup: 6
1974, 1991, 1992, 1995, 1996, 2002

Performance in CAF competitions:
2002 - First Round
2003 - Group Stage
2004 - First Round
2005 - First Round
2008 - First Round

African Cup of Champions Clubs: 8 appearances
1974: Semi-Final
1976: Second Round
1977: Second Round
1978: Second Round
1979: Second Round
1980: Second Round
1981: First Round
1995: Second Round

CAF Confederation Cup: 4 appearances
2007 - Preliminary Round
2010 - First round 16

2011 - second round 16
2012 - Second round 16

CAF Cup: 2 appearances
1993 - Finalist
1997 - First Round

CAF Cup Winners' Cup: 3 appearances
1985 - Second Round
1996 - Second Round
2001 - Second Round
Kwa Nini usiupdate hizi TAARIFA mara Kwa mara ?
 
SIMBA NA DAMU YA CLOVIS ACOSTA FERNANDES, TASWIRA YA O JOGO BONITO ROBO FAINALI AFRIKA 2019
.
Unamfahamu shabiki wa Brazil wakuitwa Clovis Acosta 'Gaucho da Copa' Aliesafiri nchi zaidi ya 60 kushuhudia mechi zaidi ya 150 za timu ya Taifa ya Brazil?? Mungu amlaze mahali pema, damu yake na spirit yake walikuwa nayo mashabiki wa Simba, usiku wa Machi 16,2019
.
Unaufahamu mchezo wa soka tamu na la kuvutia?? Napenda kuliita Freestyle football, Wareno wanaliita O Jogo Bonito, ndilo soka walilocheza Simba usiku ule dhidi ya AS Vita, falsafa yao ya siku zote Simbarcelona
.
Kuelekea usiku ule wa Kocha Patrick Aussems alikua anaenda kuingia kwenye daraja la Kocha Paul West Gwivaha huyu aliwapeleka Simba Nusu fainali Ligi ya Mabingwa 1974, aliku anaenda kujiweka daraja la Kibadeni Mputa na Enteneh Esheteh, hawa waliipeleka Simba fainali Shirikisho 1993
.
Nilitaka kumsahau Kocha Nabby Camara wa Guinea, mvumbuzi mkubwa wa vipaji 1975, Wazee wangu mnawakumbuka Abbas Kuka, George Best Kulagwa, Nico Njohole na Filbert Rubibira, nakumbuka usiku ule Aussems alituletea Rashid Juma 'Game Changer'
.
Binafsi Majira ya saa5 asubuhi kuelekea mechi ile nilisimama pembeni pale Ubungo Mataa, kushuhudia Wanasimba wakitiririka kwenye mabasi kuelekea Taifa, namkumbuka Traffic wa zamu akipata wakati mgumu kuruhusu magari kushika Mandela Road
.
Wakati naendelea kushangaa nilishuhudia Wahafidhina wa Ubungo wale wafia timu Wekundu wa Terminal wakijiandaa kuelekea Taifa, jezi zao za nakshi nakshi, majigambo yao na bendera mbele ya gari lao kuonesha ukubwa wa timu zao, kila mtu kauvaa uhusika
.
Ni mechi ya kisasi hii, ni mechi ambayo Haji Manara De Le Boss ameshatoa sumu za kutosha ni DO OR DIE, nilijishika tama na kuwatazama Wanyama wakiwa na vibe lao, nilipokumbuka miguu ya Francis Luamba Ngoma, Botuli Bompunga na Kazadi Kasengu nilizidi kushangaa
.
Lakini Mwanamama mmoja wakati nipo kwenye daladala kuelekea Taifa alikuwa anatoa darasa, alitukumbusha Ngurumo za Mnyama barani Afrika, alitukumbusha kichapo cha Zamalek na chupuchupu ya Stella Abdijan na Mehrar Kubra, aliamini Simba ni timu kubwa ya hatua kubwa
.
Vuvuzela zinapigwa njiani nami bado nipo kwenye tafakari kubwa, bado mawazo yangu nawaza zile bao 5-0 pale Congo ya Kinshasa, naikumbuka miguu ya Kazadi Kasengu, Ngoda Muzinga, Jean Makusu na ujuvi wa Fabrice Ngoma, bado naikumbuka Vita ilicheza fainali kombe la Shirikisho Afrika hapo nikazidi kuishiwa nguvu
.
Wakati nipo zangu jukwaa la buku tano, nimetulia kupitia kikosi cha Simba kilichomkosa Jonas Mkude, Aussems alikuja na 4-3-3 James Kotei "The Pitbull" na Mzamiru Yassin "Box to Box Midfielder" wakianza, Kiungo cha Vita wana Captain Nelson Munganga na Wangu Mbambu, nikizidi kupagawa
.
Bibi mmoja pembeni Mwenyeji wa Iringa huko Dabaga, aliniambia hii ni mechi kubwa lakini Simba tumeshawahi kufanya makubwa, Mg Will "sisi tulishinda kule Ivory Coast, sisi tulimvua ubingwa Zamalek, sisi tulimuangusha Ahly hapa Taifa, amini hii ni Simba, hapa tunatoka salama" alinipa moyo tu
.
Mechi imeanza, kwa kasi sana ila dakika ya 13 tu Kazadi Kasengu anaingia wavuni, lakini ajabu hakuna shabiki wa Simba alietulia, bado watu waliyaona maajabu ya 1993 na 2003, bado watu waliyaona maajabu ya Aussems kama yale ya West Gwivaha, dakika ya 36 Beki ya kushoto MO Hussein kwenye box wamo🙌
.
Ile 1-1 ilizidi kuwaamsha Mashabiki, wakati huo namtazama Yule Bibi kutokea Dabaga, alirudi tena kuniambia "Yule Zimbwe ni kama Mohamed Kajole Machela, aliwahi kupita Simba, wanafanana sana" nilianza kuingiwa na imaan, wakati huo Mashabiki wa Simba wameamsha mzuka jukwaani
.
Kipindi cha pili kimeanza ilimlazimu Aussems awe na akili nyingi alimtoa Immanuel Okwi na kumpa nafasi Haruna Niyonzima, Vita walijibu kwa kuwaleta Ducapel Moloko, Cesar Manzoki na Jeremie Mumbele, mpira ulianza kupigwa mwingi huku watu wakitazama matokeo ya Ahly dhidi ya JS Saoura
.
Bibi yule alinigeukia tena aliniambia "Maajabu ya Simba inahitajika Sub, kama ya George Kulagwa 'Best' tunahitaji winga kama yule, 1979 marudiano pale Zambia na wale Mufulira Wanderers alituwekea bao mbili kwenye ile comeback", Kocha atuletee winga ndani, Nilimuelewa tena wakati pira linapigwa jingi bado 1-1.
.
Dakika zikianza kucheza kwenye 70, huko Cairo National Al Ahly anaongoza 1-0 dhidi ya JS Saoura, bao walojifunga dakika ya 30 tu ya mchezo na Fateh Talah, huku mechi ya Simba ilikua lazima ashinde ili apite na sare ingembeba Vita
.
Dakika ya 78 anaingia Hassan Dilunga kuchukua nafasi ya Mzamiru Yassin, tena dakika ya 85 anatoka James Kotei anaingia Rashid Juma, niliwaza sana Simba hii sasa bila Kiungo Mkabaji, mbinu pekee ni kumiliki mpira na kushambulia ili wasishambuliwe
.
Wakati majukwaa yanaendelea kuamsha mizuka, nilitupa macho uwanjani, Mohamed Hussein na Zana Coulibaly wakawa wing backs kabisa, kisha nikamuona Haruna na Chama kama Perfect 8s, ama double 8 wakifanya kazi ya kuwarudisha Vita nyuma
.
Ghafla nilitaka kujua Dilunga ana kazi gani, nikagundua anacheza kama semi winger, Simba ikiwa kwenye transition ni 2-3-5🙌 huko pembeni Rashid Juma akicheza mzani sawa na Tshabalala kuwavuta Vita, mchezo wa hatari wa Space Exploitation
.
Bibi yule wa Dabaga alinitazama tena ila safari hii kwa tabasamu, alisema "Sasa tunaenda kuiona Simba ya 1979 pale dimba la Independence Lusaka" nilizidi kumuelewa, Simbarcelona wakaanza kuzihesabu pass, Sunderland Abijoo wanatakata, Haruna na mpira, Chama na akili kisha Rashid na kasi kama ya Thuwen Ally
.
Kwenye ukuta Erasto Nyoni kama George Magere Masatu na Pascal Wawa kama Fikiri Magoso, ndipo hapa nilishuhudia O Jogo Bonito, falsafa yao Simba ya soka tamu, jukwaani MO Dewji anavuta uradi, Mashabiki juu juu, Jonas Mkude na mashabiki wanaliamsha sana, watu wamevua mashati
.
Niyonzima anapiga pass huku anamfundisha Chama wapi pakukaa wametawala Golden Square, mpira mmoja mrefu kutoka mikononi mwa Manula kwake Haruna pembeni anagonga grasscutter pass kwa Bocco aliyesogea pembeni, haraka sana Haruna na Chama ndani ya box
.
Bocco analeta pass kisha Haruna anafanya dummy play anaupisha mpira, dakika ya 89!Chama one touch, Chama second touch, far post goal🙌🙌🙌 kilichobaki ni historia, siku nyingine na comeback nyingine tena
.
Allez SIMBARCELONA🙏❤
 
Kiungo Mshambuliaji Wa AL AHLY na timu ya taifa ya EGYPT Emam Ashour Ameteguka BEGA kwenye mchezo uliowakutanisha EGYPT dhidi ya NEW ZEALAND

Emam ameshahusika kwenye mabao 16 msimu huu kwa Ahly na ni wazi kumkosa nyota huyo si stori sahihi sana masikioni mwa Ahly na Kocha Marcel Koller

IMG-20240323-WA0036.jpg
 
Back
Top Bottom