DELETED ACCOUNT
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 9,805
- 15,475
Kuna video clip nimeiona jana ya mtu ambaye inasemekana ni Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Geita, anayejulikana kama Manjale akiitumia timu ya Simba na mafanikio yake kukinadi chama chake. Hii video inatia kichefuchefu maana huyu bwana anaongea kama vile yeye ni kiongozi pale Simba.
View: https://youtu.be/MYeHejL5V1c
Ni juzi tu nilitoa tahadhari kwa uongozi wa Simba wawe makini sana kutumika kwa klabu hii katika harakati za kisiasa. Hii video clip inatupa mwelekeo wa kule tunapokwenda na inaonyesha hatari iliyo mbele yetu.
Kama hawa wanasiasa wanataka wajimilikishe mafanikio ya Simba, wawe tayari pia kujimilikisha kushindwa kwa Yanga, Azam na Singida katika mashindano ya kimataifa msimu huu. Huyu bwana ameenda mbali hadi akaongelea sakata la derby na kwamba Simba ni ya chama chake na Yanga ni upande mwingine. Hili jambo halikubaliki katika ulimwengu wa football.
Bila kujali itikadi za kisiasa za mashabiki wa Simba, hili jambo halina afya njema kwa Simba SC hasa siku za mbeleni.
Viongozi wa Simba watoke hadharani na wakemee kutumiwa kwa klabu ya Simba katika majukwaa ya kisiasa. Kukaa kwao kimya kutaleta ishara kwamba wanabariki matamko haya na kwamba watakuwa tayari kubeba msalaba wa kile kitakachotokea mbeleni.