Simba SC irekebishe upesi sana 'Mapungufu' ya hawa Wachezaji Watatu Inonga, Sakho na Morisson kwani yanaigharimu Timu

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,591
108,962
1. Henock Inonga
Nakiri ni Beki mzuri sana na nimekuja Kugundua pia kuwa kumbe ni Versatile na kwamba anaweza hata kucheza vyema tu Namba 6, Namba 8 na hata Namba 2.

Mchezaji huyu tokea aicheze vyema ile Kariakoo Derby na kupata Sifa nyingi nae ameshajaa Upepo kiasi kwamba sasa anajiona ndiyo Mchezaji mzuri Kikosini Simba SC kuliko wengine waliopo au aliowakuta.

Inonga amekuwa akipenda Kulaumu mno Wenzake Uwanjani huku muda mwingi akitaka Kuonekana kama Yeye ndiyo anacheza kwa Bidii kuliko Wenzake na hupenda sana Kucheza na Akili ya Kocha Pablo ili apendwe na aaminike zaidi Kwake.

Inonga aambiwe ukweli kuwa katika ile 'Kariakoo Derby' Kazi ya Kumkaba Mshambuliaji hatari na ninayemuogopa wa Yanga SC Fiston Mayele hakuifanya peke yake kama adhaniavyo bali alikabwa Collectively and Strategically na Mabeki Wenzake Wote na tena kama kuna Mtu ambaye Mimi GENTAMYCINE niliona ndiyo alimkaba vilivyo Mayele ni Beki Joash Onyango na siyo Yeye Henock Inonga.

2. Bernard Morrison
Huyu nadhani GENTAMYCINE nilishamsoma mno hapa JamiiForums na mpaka Kuutaka Uongozi wa Simba SC Kumkanya na Kumrekebisha ila naona Jana katika Mechi na Mlandege FC yamejirudia tena yale yale.

Uongozi wa Simba SC leo ngoja sasa niwapasulieni Ukweli wangu kwa Kuwaambia kuwa hakuna Mchezaji nisiyempenda Kikosini Simba SC na asiye na Faida Kwetu ( japo baadhi yenu hasa CEO Barbara Gonzalez ) mnamlea na Kumdekeza kama huyu Bernard Morrison.

Na nimepata Taarifa za Jikoni kabisa kutoka kwa Mmoja wa Kiongozi wa Simba SC na Mchezaji Mwandamizi Kikosini kuwa kumbe hata Kocha Mkuu Pablo Franco Martin nae si tu hamtaki bali hampendi kama ilivyo Kwangu ila anakingiwa Kifua.

Morrison ana Kiburi, Morrison Mjeuri, Morrison ana Hasira za Kipumbavu ( Kipopoma ), Morisson analazimisha Ufalme asioustahili kwa sasa ndani ya Simba SC, Morrison anapenda Kucheza sana na Jukwaa na ni mpenda Matukio yasiyo na Faida ama Kwake au hata kwa Klabu yetu pia, Morrison ana Dharau iliyopotiliza na isiyovumilika na mwisho kabisa nahisi Morrison ni Psychopath Case ila huenda Uongozi wa Simba SC bado haujaligundua hilo.

Akina Barbara Gonzalez ( CEO ), Mwenyekiti wa Bodi ya Simba SC Salim Abdallah Mhene 'Try Again', Mwenyekiti wa Simba SC ( Wanachama ) Murtaza Mangungu na Wewe 'Poti' wangu kabisa kutoka Mkoani Mara ( Musoma ) Kwetu Crescetius Magori ( Mshauri Mkuu wa Mwekezaji Mo Dewji ) na pia Mshauri wa CEO na Benchi la Ufundi la Simba SC endeleeni tu Kumlea na Kumdekeza huyu Mchezaji Bernard Morrison ila GENTAMYCINE nawaambia hapa hapa JamiiForums kuwa kuna Siku atatugharimu na ataigharimu pakubwa mno Simba SC yetu.

3. Pape Ousmane Sakho
Ni Mchezaji mzuri sana na mwenye Kipaji cha Kipekee kiasi kwamba kwa anavyocheza natabiri mapema kuwa huenda huko mbeleni Simba SC ikatajirika zaidi kwa Kumuuza Nje kwa Gharama za hata Kuwazidi akina Chama na Miquissone.

Hata hivyo pamoja na hizi Kongole ( Pongezi ) zangu Kwake Sakho nae ana Mapungufu yanayotakiwa Kurekebisha haraka kwani akiachwa namuona nae ana 'Elements' za akina Inonga na Morisson.

Sakho anapenda Kukurupuka, Sakho anapenda Sifa ( hasa Kucheza na Majukwaa ), Sakho ameshaanza Kuota Majipu Kwapani ( namaanisha Kuringa na kujiona ni kila Kitu sasa Kikosini ), Sakho anataka Kuulazimisha Ufalme wake sasa Simba SC wakati muda wake wa kuwa Mfalme nauona upo ndani ya miaka Miwili ijayo.

Sakho anataka kila Kitu cha Uwanjani awe anakifanya Yeye tu hata kama Kiufundi kwa Mazingira yaliyopo hapaswi kuyafanya Yeye, Sakho anapenda sana Kukaa na Mpira na Kupiga Chenga nyingi ( Over Dribbling ) kitu ambacho ni Hatari mno Kwake Kiafya kwani uwezekano wa Kuumizwa vibaya na kupata Majeraha makubwa mfano akikutana na Mabeki 'Wahuni' na 'Masela' akina Kelvin Yondan na Juma Nyosso ( ambao Wote sasa wako Geita Gold FC ) kwa Kocha Fred Felix Kataraiya Majeshi Minziro ni mkubwa.

Tafadhali waambiwe na wajitathmini!!!!
 
1. Henock Inonga

Nakiri ni Beki mzuri sana na nimekuja Kugundua pia kuwa kumbe ni Versatile na kwamba anaweza hata kucheza vyema tu Namba 6, Namba 8 na hata Namba 2...
Uyo Inonga anapenda sifa ambazo wala hana, hasira zake za kipumbavu cku moja zitamgharimu, Angekuwa anatoa ata asist kama yannik bangala si angewapanda watu kichwani kabisa
 
Ushauri mzuri sana... Hakika wachezaji wetu wazuri sana tatizo ni kulewa sifa na kujiona wanaweza sana.. lkn nawatahadhalisha siku wakivurunda ndo watajua rangi halisi za mashabiki wa simba
 
Jamaa umeongea kitu ambacho nilikua nacho akilin mwangu.

Sijui Simba Kuna mdudu gani anawatafuna hasa wachezaji .

Yaan akibahatisha mechi moja na kupewa sifa Basi mchezaji husika ataanza kuvimba kujiona mkubwa atacheza kwa kujiamini Sana.
Huyo Innonga kiukweli ameanza kulewa sifa na anajiamini kupitiliza Sana hata Jana kala njano kidogo atucost kwa upuuz wake .Mwambien apunguze sifa acheze mpira Simba Ni kubwa kuliko yeye na ataiacha.

Kuhusu Sako Ni kweli anapaswa wamtime maana nae ameanza kulewa sifa na kutaka kila kitu afanye yeye .Kona zake mbovu ,freekick mbovu alafu apunguze kukaa Sana na mpira ,kwenye lig ya bongo watamvunja kabisa.

Kuhusu Morrison hii ndio takataka kabisa Alafu et ndie mchezaj anayelipwa pesa nyingi hapo Simba.

Morrison Hana mpira wa kuamua matokeo ,Leo awe vzr kesho hovyo .

Wachezaj wengi wa Simba wanatabia ya kulazimisha ufather wakat hawana huo ufather ,na kulingana na ujinga wao washatucost Mara kadhaa ,hata kaizer alitutoa sabab hiyo hiyo ya kujiamin kupita kiasi.

Simba hata akipata goli mbili tu wanaanza show game Kama kawaida yao na Mara nyingi hufanya uzembe na kupigwa goli na kufuta clean sheet kwa upuuz wao wenyew.

Mfano Simba ikatokea ametanguliwa na timu yoyote kwenye lig hiyo mechi Simba lazima apoteze maana hawana spirit ya kujituma Kama walivyo watan zangu yanga ,yanga nawasifu kwa Hilo yaan ukimfunga goli Ni Kama unakua umekorofisha nyuki Ila kwa Simba hicho kitu hakipo kabisa.

Mwisho wa siku nasemaje hata huko shirikisho nayaona makosa yanaenda kujirudia Kama Yale ya kaizer na Galaxy sabab ya ujinga wa baadhi ya wachezaji.
 
Kila timu ina FOOTBALL analyst...ndie anapaswa kutoa ushauri wa kiufundi kila mechi.

Ni kweli kuna pressure za majukwaa mitandao na magazeti.
 
1. Henock Inonga

Nakiri ni Beki mzuri sana na nimekuja Kugundua pia kuwa kumbe ni Versatile na kwamba anaweza hata kucheza vyema tu Namba 6, Namba 8 na hata Namba 2.

Mchezaji huyu tokea aicheze vyema ile Kariakoo Derby na kupata Sifa nyingi nae ameshajaa Upepo kiasi kwamba sasa anajiona ndiyo Mchezaji mzuri Kikosini Simba SC kuliko wengine waliopo au aliowakuta.

Inonga amekuwa akipenda Kulaumu mno Wenzake Uwanjani huku muda mwingi akitaka Kuonekana kama Yeye ndiyo anacheza kwa Bidii kuliko Wenzake na hupenda sana Kucheza na Akili ya Kocha Pablo ili apendwe na aaminike zaidi Kwake.

Inonga aambiwe ukweli kuwa katika ile 'Kariakoo Derby' Kazi ya Kumkaba Mshambuliaji hatari na ninayemuogopa wa Yanga SC Fiston Mayele hakuifanya peke yake kama adhaniavyo bali alikabwa Collectively and Strategically na Mabeki Wenzake Wote na tena kama kuna Mtu ambaye Mimi GENTAMYCINE niliona ndiyo alimkaba vilivyo Mayele ni Beki Joash Onyango na siyo Yeye Henock Inonga.

2. Bernard Morrison

Huyu nadhani GENTAMYCINE nilishamsoma mno hapa JamiiForums na mpaka Kuutaka Uongozi wa Simba SC Kumkanya na Kumrekebisha ila naona Jana katika Mechi na Mlandege FC yamejirudia tena yale yale.

Uongozi wa Simba SC leo ngoja sasa niwapasulieni Ukweli wangu kwa Kuwaambia kuwa hakuna Mchezaji nisiyempenda Kikosini Simba SC na asiye na Faida Kwetu ( japo baadhi yenu hasa CEO Barbara Gonzalez ) mnamlea na Kumdekeza kama huyu Bernard Morrison.

Na nimepata Taarifa za Jikoni kabisa kutoka kwa Mmoja wa Kiongozi wa Simba SC na Mchezaji Mwandamizi Kikosini kuwa kumbe hata Kocha Mkuu Pablo Franco Martin nae si tu hamtaki bali hampendi kama ilivyo Kwangu ila anakingiwa Kifua.

Morrison ana Kiburi, Morrison Mjeuri, Morrison ana Hasira za Kipumbavu ( Kipopoma ), Morisson analazimisha Ufalme asioustahili kwa sasa ndani ya Simba SC, Morrison anapenda Kucheza sana na Jukwaa na ni mpenda Matukio yasiyo na Faida ama Kwake au hata kwa Klabu yetu pia, Morrison ana Dharau iliyopotiliza na isiyovumilika na mwisho kabisa nahisi Morrison ni Psychopath Case ila huenda Uongozi wa Simba SC bado haujaligundua hilo.

Akina Barbara Gonzalez ( CEO ), Mwenyekiti wa Bodi ya Simba SC Salim Abdallah Mhene 'Try Again', Mwenyekiti wa Simba SC ( Wanachama ) Murtaza Mangungu na Wewe 'Poti' wangu kabisa kutoka Mkoani Mara ( Musoma ) Kwetu Crescetius Magori ( Mshauri Mkuu wa Mwekezaji Mo Dewji ) na pia Mshauri wa CEO na Benchi la Ufundi la Simba SC endeleeni tu Kumlea na Kumdekeza huyu Mchezaji Bernard Morrison ila GENTAMYCINE nawaambia hapa hapa JamiiForums kuwa kuna Siku atatugharimu na ataigharimu pakubwa mno Simba SC yetu.

3. Pape Ousmane Sakho

Ni Mchezaji mzuri sana na mwenye Kipaji cha Kipekee kiasi kwamba kwa anavyocheza natabiri mapema kuwa huenda huko mbeleni Simba SC ikatajirika zaidi kwa Kumuuza Nje kwa Gharama za hata Kuwazidi akina Chama na Miquissone.

Hata hivyo pamoja na hizi Kongole ( Pongezi ) zangu Kwake Sakho nae ana Mapungufu yanayotakiwa Kurekebisha haraka kwani akiachwa namuona nae ana 'Elements' za akina Inonga na Morisson.

Sakho anapenda Kukurupuka, Sakho anapenda Sifa ( hasa Kucheza na Majukwaa ), Sakho ameshaanza Kuota Majipu Kwapani ( namaanisha Kuringa na kujiona ni kila Kitu sasa Kikosini ), Sakho anataka Kuulazimisha Ufalme wake sasa Simba SC wakati muda wake wa kuwa Mfalme nauona upo ndani ya miaka Miwili ijayo.

Sakho anataka kila Kitu cha Uwanjani awe anakifanya Yeye tu hata kama Kiufundi kwa Mazingira yaliyopo hapaswi kuyafanya Yeye, Sakho anapenda sana Kukaa na Mpira na Kupiga Chenga nyingi ( Over Dribbling ) kitu ambacho ni Hatari mno Kwake Kiafya kwani uwezekano wa Kuumizwa vibaya na kupata Majeraha makubwa mfano akikutana na Mabeki 'Wahuni' na 'Masela' akina Kelvin Yondan na Juma Nyosso ( ambao Wote sasa wako Geita Gold FC ) kwa Kocha Fred Felix Kataraiya Majeshi Minziro ni mkubwa.

Tafadhali waambiwe na wajitathmini!!!!
Mimi sina la kusema ndugu yangu, umeongea ukweli na acha ukweli ukuweke huru.
1.INONGA
Anataka kubeba hata kisicho chake, anafokea hadi nahodha wake badala ya kumshauri. Back passes za ovyo na kujiamini kulikopitiliza hadi anaharibu. Mechi aliyojisifu kumdhibiti Mayele ni kweli tuhesabu matukio ambayo Mayele aliyodhibitiwa na Onyango kulinganisha na yake.
2.MORRISON
Huyu ni mchezaji mzuri anayetoa faida anapopenda yeye. Hana uchungu na timu, kwake sifa binafsi ni muhimu kuliko sifa ya timu. Ile faulo iliyompa kadi Jana dhidi ya Mlandege ilikuwa na faida gani zaidi ya kuendeleza ubabe usio na faida?
3.SAKHO
Mcheza na jukwaa maarufu, kila akifanya kitu anageukia jukwaa kuliamsha limshangilie. Ni aina ya SAID SUED "SCUD". Aache umaarufu umfuate, akiufuata utamwangamiza.
 
Inonga anapenda Sifa, Yes ( kama ilivyo kwa binadamu wote).
Kupenda kwake sifa, ndio kunamfanya ajitume zaidi ( Anapenda sifa lakini hajawahi tuchomesha).
Kuhusu kugombeza kila mtu, nadhani inonga ni experienced player kuliko wengi walioanza jana ( hasa beki za pembeni, zina makosa mengi mno) hivyo wanapofanya tofauti wacha warekebishwe.....
Mchezaji wangu bora kwa sasa, Ni Inonga baka " Varane". Mechi zote anacheza kwa performance ileile ya hali ya juu......
Hakuwahi cheza chini ya kiwango.
 
Inonga yupo vizuri ila mkude, mzamiru na wawa wajifunze kuweka mpira chini na kupiga pasi za macho, mipira yao mirefu mingi inapotea. Mkude na mzamiru wanapenda sana kurudisha mpira nyuma badala ya kupeleka mbele tatizo ambalo pia analo mwenda. Back pass zimekuwa nyingi
 
Back
Top Bottom