Mstahiki Mea
JF-Expert Member
- Jul 13, 2018
- 6,137
- 11,400
Kuelekea mechi ya watani yanga nikama wanataka kuanza kushinda nje ya uwanja , drama wanazofanya kwa vyovyote vile zinadhoofisha maandalizi ya Simba , wanataka kuwin kwa simba kuchukulia mchezo wa watani kama mechi ya kawaida. Simba tubatakiwa kujipanga sana ili kupata walau alama kwenye huo mchezo. Yanga wana timu nzuri ya kuweza kupata matokeo kwenye mchezo wowote wa ligi hivyo tusiwachukulie poa hata kidogo , hawa jamaa wanajifanya hawatacheza ila mwisho wasiku wataleta timu iliyoimarika sana uwanjani. Hii ni taadhari nimetoa tu ukizingatia michezo yetu na yanga hivi karibuni imekuwa vigumu sana sisi kupata alama