Kichuchunge
JF-Expert Member
- Dec 2, 2020
- 338
- 891
Desemba 28, mwaka 2021, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania(TPLB) iliamua kuahirishwa kwa mchezo namba 69 wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Kagera Sugar FC na Simba SC uliokuwa uchezwe siku hiyo Saa 10:00 Alasiri katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, kutokana na taarifa za kitabibu kuwa wachezaji 16 kati ya 22 wa Simba SC waliosafiri kwenda Bukoba kuonekana kuwa na dalili ya mafua na kukohoa hali inayochangiwa na mabadiliko ya hali ya hewa (Seasonal Influenza).
Simba ingeweza kulazimishwa kuchezesha wachezaji nane, iagize wachezaji wa Under 20, au la ipoteze pointi kwa mujibu wa Kanuni maana kuugua kwa wachezaji wao haikuwa kosa la Kagera kabisa ila Bodi ikatumia 'Busara' mechi ikaahirishwa.
Lakini jana Bodi hiyo ikashindwa kutumia 'Busara' hiyo hiyo kuahirisha mechi ya Azam na Kitayosce kutokana na baadhi ya wachezaji wa Kitayosce kutokidhi vigezo huku wengine, akiwemo golikipa wakiwa ni wagonjwa lakini wakalazimishwa wacheze hivyo hivyo wakiwa nane.
Je, hapa Bodi haikuona haja ya kutumia 'Busara' au inaonea timu ndogo?
Tujadili.