Mechi kati ya Simba na Mtibwa yasogezwa mbele

bullar

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
9,172
20,065
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), imetangaza kuahirisha mchezo kati ya Simba SC dhidi ya Mtibwa Sugar uliopangwa kuchezwa Februari 18, 2024 katika dimba la Jamhuri Morogoro.

Kwa mujibu wa taarifa ya TPLB, sababu za kuahirishwa kwa mchezo huo ni kutoa fursa kwa Simba SC, kujiandaa na safari yake ya kwenda Ivory Coast kuivaa Asec Mimosas kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) utakaopigwa Februari 23, 2024.

Tarehe mpya ya mtanange huo, itatangazwa.

My take: kwani TFF walikua hawajui kuna mechi za CAF? Pili kutoka tarehe 18 hadi 23 hakutoshi kumuandaa na mechi? Tatu, Mtibwa watalazimika kuingia gharama za ziada baada ya mechi kusogezwa mbele hio hasara nani analipa?

1708078469636.jpg
 
Wazee Wa Viporo Wanaogopa Pressure Ya League.

Dar Young Africans Tunaanza Mzunguko Wa Pili Kesho Hatukuwa Na Viporo Ndio Maana Game Zilikuwa Zimetubana Na Tumepata Matokeo.

Round Ya Pili Tuna Point Zetu 6 Za Uhakika Toka Kwa Simba Sc & Azam.
 
Kwani nyie mlishiriki AFL?Al Ahly wenyewe wanacheza kiporo cha CAFCL leo.BTW mbona Simba walipotaka kucheza na Coastal Union kupunguza viporo mlipiga kelele hadi TFF wakakataa?
 
Back
Top Bottom