Simba hamjatosheka kuua vipaji vya wachezaji vijana mmemgeukia na kwa Ladack Chasambi wa Mtibwa??

Majok majok

JF-Expert Member
Aug 3, 2023
618
1,565
Hii klabu kwa miaka ya hivi karibuni imekuwa bingwa wa kuua vipaji vya wachezaji vijana pindi inapowasajili, imekuwa na tamaa ya kuwasajili lakini wamekuwa wazito kuwatumia wachezaji husika!

Angalia David kameta(duchu) kabla hajaenda Simba alikiwasha sana wakamsajili akasugua benchi mpaka akatolewa kwa mkopo kwenda biashara kisha Geita na Mtibwa wakaona anakiwasha wakamrudisha ameishia kupiga picha za uzinduzi wa jezi kwa sasa!

Nenda kwa dogo Mohamed mussa kutoka Zanzibar walisajili kwa mbwembwe nyingi lakini sikumbuki amecheza mechi ngapi mpaka Sasa tokea asajiliwe na nasikia wanataka kumtoa Tena kwa mkopo dirisha dogo!

Nenda kwa wakina jimysoni mwanuke walikotoka walikuwa wanakiwasha wameenda Simba mda mwingine ata kukaa benchi tu hawakai!

Kuna orodha ndefu ya wachezaji vijana ambao wamekuwa wakipata wakati mgumu sana waliposajiliwa pale Simba. Nafikiri kuna tatizo kubwa kwenye scouting yao aidha hawamshirikishi Kocha husika ama wanasajili kisiasa tu wakisikia gazeti limeandika Yanga inamtaka fulani wao wanakurupuka kwenda kumalizana na mchezaji aliyetajwa matokeo yake anakuwa haendani na mfumo wa kocha anaishia kusugua benchi!

Sasa wamemgeukia LADACK CHASAMBI dogo wa Mtibwa, nasikia wamemalizana nae, swali ni je, watamtumia?

Kijana bado ni mdogo sana kiumri na wakienda kumpiga benchi ndio inakuwa wanaua kiwango chake bado anahitajika kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara ili kulinda kiwango chake!

Nafikiri na wasimamizi wa Hawa wachezaji awako makini ata kidogo wanachoangalia ni mpunga tu wakishapewa awaangalii kesho yake itakuwaje kwa kipaji cha mchezaji, Simba kwa sasa sio sehemu sahihi ya kumpeleka mchezaji kijana ni Bora wangemtafutia timu nyingine ya level za mtibwa ili kijana aendelee kupata nafasi ya kucheza tofauti na Simba ambayo inahitaji wachezaji waliokwisha komaa ndio wanaowaamini watawavusha!

Pamoja na fedha wanazovuna wasimamizi wa hawa wachezaji inatakiwa pia waangalie wanavyolinda vipaji vya wachezaji husika!
 
😁😁😁😁😁😁
Baada ya mechi kubuma ya Al Ahly, mehamia kwa Simba tena.
😁😁😁😁😁😁😁.
Kwa mkapa hatoki mtu lazima Al Ahly afungwe, sasa anawasubiria kwao mkale kichapo cha 3-0 tena😁😁😁😁😁
 
Timu inayojitahidi kuwapa nafasi vijana wengi wadogo wenye vipaji vikubwa ni Yanga tu. Ukienda Yanga na kukaza buti kama Dickson Job, Ibrahim Abdallah (Bacca), nk. Lazima ung'ae! Na matunda utayaona.
 
😁😁😁😁😁😁
Baada ya mechi kubuma ya Al Ahly, mehamia kwa Simba tena.
😁😁😁😁😁😁😁.
Kwa mkapa hatoki mtu lazima Al Ahly afungwe, sasa anawasubiria kwao mkale kichapo cha 3-0 tena😁😁😁😁😁
Tunaongelea mambo ya muhimu wewe unaleta akili zako za kibwege bwege za ukoloni uko!!
 
Hakuna timu inayosajili wachezaji iwaue. Mchezaji anajiua mwenyewe kwa kubweteka na kuridhika na maisha.
 
Hii klabu kwa miaka ya hivi karibuni imekuwa bingwa wa kuua vipaji vya wachezaji vijana pindi inapowasajili, imekuwa na tamaa ya kuwasajili lakini wamekuwa wazito kuwatumia wachezaji husika!

Angalia David kameta(duchu) kabla hajaenda Simba alikiwasha sana wakamsajili akasugua benchi mpaka akatolewa kwa mkopo kwenda biashara kisha Geita na Mtibwa wakaona anakiwasha wakamrudisha ameishia kupiga picha za uzinduzi wa jezi kwa sasa!

Nenda kwa dogo Mohamed mussa kutoka Zanzibar walisajili kwa mbwembwe nyingi lakini sikumbuki amecheza mechi ngapi mpaka Sasa tokea asajiliwe na nasikia wanataka kumtoa Tena kwa mkopo dirisha dogo!

Nenda kwa wakina jimysoni mwanuke walikotoka walikuwa wanakiwasha wameenda Simba mda mwingine ata kukaa benchi tu hawakai!

Kuna orodha ndefu ya wachezaji vijana ambao wamekuwa wakipata wakati mgumu sana waliposajiliwa pale Simba. Nafikiri kuna tatizo kubwa kwenye scouting yao aidha hawamshirikishi Kocha husika ama wanasajili kisiasa tu wakisikia gazeti limeandika Yanga inamtaka fulani wao wanakurupuka kwenda kumalizana na mchezaji aliyetajwa matokeo yake anakuwa haendani na mfumo wa kocha anaishia kusugua benchi!

Sasa wamemgeukia LADACK CHASAMBI dogo wa Mtibwa, nasikia wamemalizana nae, swali ni je, watamtumia?

Kijana bado ni mdogo sana kiumri na wakienda kumpiga benchi ndio inakuwa wanaua kiwango chake bado anahitajika kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara ili kulinda kiwango chake!

Nafikiri na wasimamizi wa Hawa wachezaji awako makini ata kidogo wanachoangalia ni mpunga tu wakishapewa awaangalii kesho yake itakuwaje kwa kipaji cha mchezaji, Simba kwa sasa sio sehemu sahihi ya kumpeleka mchezaji kijana ni Bora wangemtafutia timu nyingine ya level za mtibwa ili kijana aendelee kupata nafasi ya kucheza tofauti na Simba ambayo inahitaji wachezaji waliokwisha komaa ndio wanaowaamini watawavusha!

Pamoja na fedha wanazovuna wasimamizi wa hawa wachezaji inatakiwa pia waangalie wanavyolinda vipaji vya wachezaji husika!
Nako ni kajinga Kwa nini akubari sehemu ambayo hatocheza kisa Pesa?
 
Mohamed Hussein Zimbwe, Shomari Kapombe (Kabla ya kwenda Azam na Ufaransa) naKibu Denis, Emmanuel Anord Okwi ni mifano ya vijana waliosajiliwa miaka ya karibuni wakiwa na umri mdogo na kufanikiwa SSC. Hata Denis Nkane, Kibwana Shomari, Gift Fred na wengine wameshindwa huku kina Dickson Job na wengine wakitusua. Hata kwenye timu ndogo wapo Wanaofeli na kufanikiwa
 
SIMBA sc ni timu kubwa na namba 1 Tanzania,afrika mashariki na kati..sasa wanachezewa rafu na hizi timu ndogo kwasababu ya wivu na chuki dhidi ya mtu aliyefanikiwa,ndio maana Mungu akampa mwafrika ngozi nyeusi
 
Back
Top Bottom