Mashabiki kutokua na shukurani kwa wachezaji

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
9,159
33,389
Inasikitisha sana Kwa kweli Kwa mashabiki wengi wa timu kubwa nchini,hususan mashabiki wa Simba na Yanga.
Mashabiki Hawa wamekua hawana shukurani kabisa kwa wa chezaji waliopungua uwezowao,Mfano wachezaji wa Simba ambao ama Kwa umri wao ama Kwa nyakati Tu au sababu nyingine inapopelekea viwango vyao kushuka,mashabiki hao wamekua wakitoa maneno ya kashfa Kwa wachezaji hao ambao kwa kweli waliitumikia timu kwa jasho na damu.
Wamekua wakitoa maeno ya kutaka waachwe bila heshima.katika maisha watu wote wenye vipaji huinuka na vipaji vyao lakini baadae uwezo hushuka taratibu ama kutokana na umri ama sababu nyingine ambazo zinakua nje ya uwezo wachezaji hao,mfano baadhi ya wachezaji wa Simba.
Nachukizwa sana na maneno yanayotolewa kwa wachezaji Hawa.

mfano wachezaji kama.
Boko,Phir,Micqiison,baleke,Mohamed husein,Kapombe,Ntibasonkiza na hata walipoondoka kama onyango,Kagere na wenzake walikutana na kadhia hii, na wachezaji wengine.
Hao wachezaji wameifanyia Simba mambo makubwa mno,wameipigania kwa uwezo wao wote.tunachotakiwa sisi mashabiki ni kuwapongeza na kuwatia moyo kwa kazi nzuri walioifanyia Simba sio kiwasemea maneno ya kashfa.
Tisiwe watu tusio na shukurani.
Mfano John Boko ni mchezaji alieifanyia Simba mambo makubwa mno na amekua mfungaji Bora kwa miaka mingi,Leo unakuta mtu anasema hivi huyu Boko anabakiswa kwa Nini?
Boko kazeeka,Boko kafanya hivi mara vile.huu sio ustaarbu hata kidogo.
Njoo kwa mfano kwa kijana kama Moses Phiri,ingawa huyu hakukaa sana klabuni lakini Kwa sababu TU alipata majeraha lakini alishaonesha uwezo mkubwa sana wa kuweka mpira wavuni.lakini utakuta mtu anatoa kashfa bila kujali kijana kapitia kipindi Gani.
Ndugu zangu mifano ni mingi lakini naomba watu tuwe na shukurani sio kuwakatisha tamaa wachezaji wanaotarajiwa kuachwa na hata watakao Baki.

Tusiwe na tabia za kondakta wa daladala,anampenda abiria akiwa hajapanda daladala,ila akipanda TU anakua adui yake,abiria akitaka kushuka ndo balaa kabisa anaweza hata akamsukuma chini kwa sababu anaona anamchelewsha,ili tu apande mwingine,huyo ambae hajapanda atabembelezwa Huku akikumbatiwa.sasa huu sio uungwana.

Ama tusiwe na tabia za mpiga debe,atalisifia basi kabla halijajaa kwa sababu akilijaza TU atapata ujira wake,lakini likijaa TU analitolea kashfa kama vile "achana na basi bovu hilo" na kuanza kulisifia basi lingine "panda ndinga mpya hii"
Huu sio uungwana pia.

Tubadilike jamani wachezaji sio punda wala ng'ombe wa kilimo ama wa kubebea mizigo.
Hata wanyama hao mmiliki wao hua anawaheshimu sana wakati wakiwa na uwezo na hata baada ya uwezo kushuka kwa sababu wamemletea faida kubwa
 
Naunga mkono hoja yako Mkuu. Kuna watu wanataka wasiyoyaweza yatendwe na wengine. Hivi Leo Captain fantastic ni wa kunyahyapaliwa kama galasa asiyewahi kuifaidisha Simba Kwa lolote? Yanayoendelea yanafanya timu ikose legendary wa kweli wa timu. Wachezaji wakifikisha miaka 30 watataka kuondoka ili yasiwakute yaliyowapata wenzao.
 
Back
Top Bottom