Chasambi akataa milioni sita Yanga, asaini Msimbazi kwa milioni 2

franckkimm

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
440
852
Nyota wa klabu ya Mtibwa Sugar Ladack Chasambi amesajiliwa na kikosi cha Simba kwa dau la million 70 na mshahara wa Million mbili [2] kila mwezi kwa miaka mitatu [3].

Chasambi imeitupilia mbali ofa ya Yanga ambayo ilikuwa na dau la usajili la Million 70 na mshahara wa Million sita [6] kwa mwezi, sababu kubwa ya kuitosa Yanga ni ufinyu wa nafasi ya kucheza kwenye kikosi hicho tofauti na Simba inayojitafuta.

Mbali na ofa Yanga ambayo aliipiga chini, ofa nyingine ilikuwa inatoka Azam FC mahali ambapo hakufikiria mara mbili kutokana na dau lao kuwa dogo, lakini pia klabu ya AS Vita ilikuwa inaihitaji saini yake.

Ladack ni miongoni mwa nyota wawili [2] ambao usajili wao umekamilika ndani ya klabu ya Simba kati ya sita [6] ambao wanatarajiwa kusajiliwa na klabu hiyo kwenye dirisha hili dogo la usajili la mwezi January.

Chasambi atakuwa sehemu ya kikosi cha Simba kitakachoshiriki michuano ya mapinduzi yanayotarajiwa kuanza kurindima mwezi December.
 
Mbona kama ni chai hivi, yanga watoe milioni 6 mchezaji ndio kwanza anatoka mtibwa..

Ila angeenda huko huko utopoloni akawa anakunja m 6 kwa mwezi, huku akipambana kupenya kikosi cha kwanza,
Hata simba nafasi ni finyu kuna wachezaji kibao wanasugua.
Angetoa sababu za kimichezo, mfano labda simba wamemuonesha anavyohitajika, labda kocha ndio kamtaka kampa plans zake, kamuhakikishia namba na vile atakavyotumika. La sivyo hata simba akifanya ujinga atasugua.
 
Kama mchezaji lazima Kuna vitu kaangalia katika pande zote mbili zilizoainishwa hapo huenda Ni baadhi Kati ya nyingi

Pia ulizo ainisha ww zinaweza kuwa pia Ni sababu....ila mwisho wa siku yenye mwenyewe ndio anajua kwanini kaamua kusaini Simba na sio Yanga, Azam au as vita
 
Mbona kama ni chai hivi, yanga watoe milioni 6 mchezaji ndio kwanza anatoka mtibwa..

Ila angeenda huko huko utopoloni akawa anakunja m 6 kwa mwezi, huku akipambana kupenya kikosi cha kwanza,
Hata simba nafasi ni finyu kuna wachezaji kibao wanasugua.
Angetoa sababu za kimichezo, mfano labda simba wamemuonesha anavyohitajika, labda kocha ndio kamtaka kampa plans zake, kamuhakikishia namba na vile atakavyotumika. La sivyo hata simba akifanya ujinga atasugua.
Mwenyewe nimeshangaa sana mtu anawezaje kukataa mil 6 kisa benchi wakati yeye bado n dogo Tu anayejitafuta....

Maana hata Huko Simba Hana nafasi ya uhakika lazima apambane kupata nafasi
 
Na vipi kama maamuzi ambayo kachukua yakawa sahihi..Bado utakuwa na dout mkuu??

Mpira ni maisha, na yeye kaamua kuchukua maamuzi Kama sehemu ya maamuzi katika maisha yake, huenda akawa amepatia au amekosea tuache muda uongee

Pia hata yeye nafikiri kabla ya kufanya maamuzi hayo alifikiri na kuja na maamuzi aliyochagua, pia tusiangalie kwa Simba na Yanga vipi kuhusu Azam au as Vita??? .....mkuu tuache muda uongee Alafu tujeku judge baadae
 
Back
Top Bottom