Simba Bora akimbie mechi kama atapangwa na Mamelodi Sundowns

Simba Bora akimbie mechi kama atapangwa na Mamelodi Sundowns

Ni wale wale, baada ya Simba kupokea vichapo 2 kwenye kundi wakaanza kusema Simba ni mbovu na asahau kuvuka kundi.

Wakati Simba akipanga kushinda mechi 3 za kimkakati yaani Viper nje ndani na home wa Holoya wale wale walibeza vibaya sana na kufikia hatua kwamba Timu bora angeachiwa Mgunda.
Mpira hunadilika, Simba ikabadilika hadi kufikia kumchapa Holoya 7 mtungi, wale wale bila aibu wakasema Holoya ni timu dhaifu kwamba Simba kapangwa kundi hafifu.

Leo wamekuja tena kusema Simba akipangwa sijui na na..ni yaleyale.

Simba mwendo mdundo, timu bora pekee Tanzania, Africa Mashariki na Africa nzima

Hongera wachezaji, hongera uongozi madhubuti na hongera Mashabiki.
Mnajitahidi mkuu....
 
Hao Mamelodi Sundowns wana nini cha ziada? Shida ya watanzania wengi ni malimbukeni tu.

Bora kupangwa na hao mamelodi kuliko waarabu kwenye hatua ya mtoano.

Udhaifu wa mamelodi ni safu ya ulinzi, wanaingilika tu.
Ngoja tuone
 
Hiyo Mamelod yenyewe msimu wa 5 huu inaishia robo fainali, mwaka jana mliijaza hivihivi mkisema itachukua kombe lakini ikaja kutolewa na Atletico Petroleos kwenye hatua ya robo fainali.
Petro atletico walikuwa wamoto sana
 
Kacheza na Al hilal kule South Africa Mamelod akashinda moja tena kwa shida.

Marudiano pale Khartoum walitoka sare ya kufungana.

Sasa Simba na Al Hilal kwenye rank Simba ipo juu ya Al Hilal.

Lolote linawezekana mkuu.
Tuombe iwe hivyo
 
Uzuri ni kwamba michuano yenyewe inahusisha MABINGWA barani Afrika, kwahiyo hakuna cha kuhofia ligi ni ya mabingwa wataonyeshana ubora wao uwanjani na yoyote anaweza kupata matokeo.
 
Kukimbia ni kutokujielewa kama wewe. Fikiria kwanza Simba haiwezi kuendelea kukua au kuwa kubwa Africa kama hajakutana na hiyo miamba iliyoko juu yake.
Simba ingeendelea na ujinga wa kukutana na Zalan Fc, Real Bamako, Monastir isingekuwa kubwa Africa kama ilivyo Sasa. Hao Zalan Fc, Real Bamako, Monastir sio saizi za Simba kwa Sasa. Huko Tanzania Kuna timu ambazo ni saizi ya timu nilizotaja hapo juu lakini sio Simba.
Level za Simba kwa Sasa ni Al Ahly, Esperance de Tunis, Mamelody na Raja. Famasiala nini. Ukibisha nimekaa paleee.
 
Mpira haupimwi hivyo rafiki.. 😀 😀
 
Waletwe hao Mamelod Sundowns hao wawili wengne ndio wabaya sitaki kukutana nao kwa hatua hii ya robo
 
Uzuri ni kwamba michuano yenyewe inahusisha MABINGWA barani Afrika, kwahiyo hakuna cha kuhofia ligi ni ya mabingwa wataonyeshana ubora wao uwanjani na yoyote anaweza kupata matokeo.
Sio kigezo kutoelewa kuwa Simba ni underdog pale
 
Kukimbia ni kutokujielewa kama wewe. Fikiria kwanza Simba haiwezi kuendelea kukua au kuwa kubwa Africa kama hajakutana na hiyo miamba iliyoko juu yake.
Simba ingeendelea na ujinga wa kukutana na Zalan Fc, Real Bamako, Monastir isingekuwa kubwa Africa kama ilivyo Sasa. Hao Zalan Fc, Real Bamako, Monastir sio saizi za Simba kwa Sasa. Huko Tanzania Kuna timu ambazo ni saizi ya timu nilizotaja hapo juu lakini sio Simba.
Level za Simba kwa Sasa ni Al Ahly, Esperance de Tunis, Mamelody na Raja. Famasiala nini. Ukibisha nimekaa paleee.
Sawa mkuu
 
Mpira sio alfabeti kwamba ikitoka a lazima ifuate e, kinacho kupa sababu ya kusema hivyo ni mechi ya mamelod na Al ahly, lakini mpira siku zote hua una matokeo ya kushangaza Sana tuache dakika 90 zitaamua nani ni mshindi
Unataka kusema Simba anaweza kumpiga mamelods
 
Back
Top Bottom