Labani og
JF-Expert Member
- Sep 15, 2020
- 23,011
- 32,907
KILA nikiwafikiria Mamelodi Sundowns [emoji1221] siombei wakutane na Simba kwenye Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Jamaa wanatisha balaa. Ni bora wakutane na kinara wa kundi A ambaye kuna uwezekano mkubwa akawa Wydad [emoji1173] au kinara wa kundi D ambaye kuna uwezekano mkubwa akawa ni Esperance [emoji1249]
Licha ya ubishi wote ambao umekuwepo, kwenye hili la Mamelodi nakataa, Jamaa kwanza wana bonge la timu halafu limeundwa na kundi kubwa la wachezaji wa nyumbani kwao lakini wengi wamekulia katika njia sahihi za kimpira maana kule Afrika Kusini kuna vituo vya soka la vijana vingi kuliko hata idadi ya timu zao.
Safu yao ya ulinzi sio tishio sana ila tatizo kubwa ni ile safu yao ya kiungo na ushambuliaji. Ina watu wana njaa kweli na kumpiga mtu nne, tano na hata sita kwao ni jambo la kawaida wakiongozwa na yule Mnamibia, Peter Shalulile.
Sawa Simba inaweza kupata bao au hata mabao dhidi yao lakini je kwa ile beki ya Simba inaweza kuwazuia wale wasifunge?
Source Shafii daudah
Nini maoni Yako...